The Manchester City (The Citizens) | Special Thread

MSHAMBULIAJI nyota majeruhi wa Manchester City, Gabriel Jesus, anatarajiwa kurejea uwanjani haraka licha ya kuumia vibaya.
Jesus, aliweka picha kwenye mtandao ikimuonyesha akiwa na kifaa maalum cha matibabu ya mguu kwenye mashine.
Man City inaweza kumtumia Jesus mapema tofauti na matarajio ya wengi baada ya kufungwa kifaa ambacho kitamponya haraka.

Jesus alimwaga chozi uwanjani, baada ya kuumia uvungu wa goti katika mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Crystal Palace Januari Mosi.
Wanasayansi na madaktari wametumia kifaa hicho kuhakikisha mchezaji huyo anarejea katika ubora wake.
Man City ina matumaini mchezaji huyo atarejea uwanjani baada ya wiki sita, lakini itategemea kifaa hicho kitafanya kazi kwa ufanisi gani.

Taarifa za maofisa wa Man City zimedokeza Jesus anaweza kupona haraka katika mazingira yote kuhakikisha anakuwa fiti.
Jesus anashika nafasi ya tatu kwa ufungaji Man City akiwa na mabao 10, lakini Pep Guardiola amemuweka katika kikosi cha kwanza akiwa na matumaini ya kurejea katika Ligi ya Mabingwa Ulaya mwezi ujao.
 
Gunners wamekubali kumpoteza Alexis uhamisho wa Januari na wameshaitaarifu City kuwa wanataka kiasi kisichopungua £35m kwa ajili ya mchezaji huyo wa Chile.
City hawapo tayari kutoa kiasi hicho lakini vyanzo vimeiambia Goal kuwa vinara hao wa Premier League wanaamini wataweza kuepuka kumkosa kama ilivyotokea majira ya joto kwa kumfunga kwa mkataba wa muda mrefu kabla ya kufungwa dirisha la usajili mwisho wa mwezi huu.

Vyanzo vilivyo karibu na Alexis vimeainisha kuwa kuna uwezekano mkubwa dili litafanikiwa, na kwamba mchezaji huyo anatamani kuhama haraka iwezekanavyo.
Mkurugenzi wa michezo wa City, Txiki Begiristain amekuwa kwenye mazungumzo na Gunners Ijumaa na Jumapili akitafuta namna ya kufanikisha mchakato ho.
Vyanzo vya Etihad vinadai kuwa wanaamini wataweza kufanikisha uhamisho huo kwa takribani kiasi cha £25m.

Kuna hofu kuwa Arsenal wanaweza kujaribu kuchelewesha dili, kama walivyofanya majira ya joto. Lakini wanatambua kuwa mchezaji huyo anataka kuondoka na wasipomuuza sasa ataondoka bure mwisho wa msimu.
Alexis Sanchez aliachwa kwenye kikosi kilichofungwa na Nottingham Forest Jumapili, ambapo Gunners walinyukwa 4-2. Hiyo inaweza kumruhusu kuichezea City kwenye Kombe la FA, ikiwa dili litakubaliwa.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Chile anaweza pia kuingizwa kwenye kikosi cha Ligi ya Mabingwa. Klabu inaweza kusajili mchezaji mmoja tu ambaye amewahi kucheza Ligi ya Europa hatua ya makundi kuelekea hatua ya mtoano Ligi ya Mabingwa.
Maendeleo ya sasa ya City kuhusu usajili wa Alexis ni miongoni mwa sababu zilizowafanya kuanza kupotezea mpango wa kumsajili beki wa kati wa Real Sociedad Iñigo Martinez.
Martinez ambaye pia amecheza Ligi ya Europa angeweza kuingia kwenye kikosi cha City kwenye kampeni za Ulaya kama watamsajili Januari, lakini Blues wanaona ni heri kumuingiza Alexis kwani wanaamini ataleta mabadiliko makubwa zaidi katika muda uliobaki msimu huu.
 
Arsenal na Manchester City wanataka kumnunua beki wa West Brom Jonny Evans.
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger anaaminika kuwa tayari kuomba klabu yake kutoa £25m kumnunua mchezaji huyo wa miaka 30 kutoka Ireland Kaskazini.
Arsenal wana nafuu kidogo kwani West Brom wanamtaka beki wa kushoto Mathieu Debuchy, 32, ambaye anatafuta fursa ya kuchezwa kikosi cha kwanza.

City wanataka mchezaji wa kujaza nafasi ya nahodha Vincent Kompany ambaye ameumia tena.
Klabu nyingine za Ligi ya Premia pia zinamtaka Evans lakini haziwezi kushindana na klabu ambazo zinacheza soka ya Ulaya.
Evans alijiunga na West Brom kutoka Manchester United kwa £6m Agosti 2015.
 
Tetesi
Kiungo wa kati wa Shakhtar Donetsk na Brazil Fred, 24, anasema anasubiri simu kutoka kwa meneja wa Manchester City Pep Guardiola. (GloboEsporte, kupitia Manchester Evening News)
 
Tetesi

Man City kumnasa Alexis Sanchez wiki hii

Uhamisho wa Alexis Sanchez kutoka Arsenal kwenda Manchester City unaweza kukamilika mapema wiki hii, kwa mujibu wa Express .
City wameonyesha nia ya kumsajili mchezaji wa zamani wa Pep Guardiola akiwa Barca mwezi Januari, na klabu hizo mbili zipo kwenye mazungumzo.
Vinara hao wa Ligi Kuu Uingereza wanataka kukamilisha usajili huo haraka iwezekanavyo, na wanatumai kumsajili Alexis kwa ada ya uhamisho ya £30 milioni.
 
Manchester City wanatarajiwa kutoa ofa mpya kwa mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez, 29, na wanaamini kuwa Arsenal watamruhusu raia huyo wa Chile kuondoka mwezi huu.

Sanchez yuko tayari kurejesha kima cha pauni milioni 25 kuhakikisha kuwa amejiunga na Manchester City mwezi huu. (Sun)

Arsenal watamruhusu Sanchez kuondoka ikiwa watapokea hadi paui milioni 30 na wanataka shughuli hiyo kukamilika mapema ili kuwawezesha kumtafuta mchezaji ambaye atachukua mahala pake. (Mirror)
Taarifa zinasema kuwa Sanchez huenda akajiunga na Manchester City kwa muda wa wiki moja inayokuja. (Independent)
 
Man City yateta na


Manchester City wamefanya mazungumzo na beki wa zamani wa United Jonny Evans kuhusu uhamisho wake kutua Etihad kwa mujibu wa Daily Mail.
Evans, 30, amebakiwa na miezi 18 katika mkataba wake West Bromwich Albion na pia ameivutia Arsenal katika dirisha la uhamisho wa mwezi huu.
 
Pep Guardiola right now [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

 
Nilisema Game ngumu wazee pale unfield sio sehemu salama kwa cty, ila nawapongeza kupunguza idadi ya magoli mana ingekua aibu ile
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…