Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 301,221
- 1,172,274
MSHAMBULIAJI nyota majeruhi wa Manchester City, Gabriel Jesus, anatarajiwa kurejea uwanjani haraka licha ya kuumia vibaya.
Jesus, aliweka picha kwenye mtandao ikimuonyesha akiwa na kifaa maalum cha matibabu ya mguu kwenye mashine.
Man City inaweza kumtumia Jesus mapema tofauti na matarajio ya wengi baada ya kufungwa kifaa ambacho kitamponya haraka.
Jesus alimwaga chozi uwanjani, baada ya kuumia uvungu wa goti katika mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Crystal Palace Januari Mosi.
Wanasayansi na madaktari wametumia kifaa hicho kuhakikisha mchezaji huyo anarejea katika ubora wake.
Man City ina matumaini mchezaji huyo atarejea uwanjani baada ya wiki sita, lakini itategemea kifaa hicho kitafanya kazi kwa ufanisi gani.
Taarifa za maofisa wa Man City zimedokeza Jesus anaweza kupona haraka katika mazingira yote kuhakikisha anakuwa fiti.
Jesus anashika nafasi ya tatu kwa ufungaji Man City akiwa na mabao 10, lakini Pep Guardiola amemuweka katika kikosi cha kwanza akiwa na matumaini ya kurejea katika Ligi ya Mabingwa Ulaya mwezi ujao.