The Manchester City (The Citizens) | Special Thread

Tetesi

Manchester City inatarajiwa kutia saini kandarasi yenye thamani ya £45m kwa mwaka na kampuni ya Puma. Kandarasi yao na kampuni ya Nike ina thamani ya £18m kwa mwaka. (Sun)

Fifa imepanua uchunguzi wake kuhusu iwapo Manchester City ilivunja sheria kuhusu usajili wa wachezaji.

Klabu hiyo huenda ikaadhibiwa na marufuku ya uhamisho iwapo itapatikana na makosa. (Telegraph)
 
Wakuu kesho nadhani ndo kutafanyika droo mungependa tupangwe na team gani? Team gani ambao hampendi tukutane nao?
Napenda tupangiwe Madrid au Sevila kwanza kabisa madrid ni timu inayocheza kwa mzuka na kikosi chao hakina ubora wowote msimu huu, pili Sevila wana viungo wazuri kama Barnega na Nzonzi. Sasa hii vita ya hawa viungo pale kati najua itakua kali na yakuvutia sana japo ni lazima tuwatoe kutokana na kwamba hawana ukuta mzuri sana kutuzuia au forwad kali kutufunga.

Timu sitamani kukutana nazo ni Barca na Buyern, kwanza kabisa historia pia barca ndio kama chuo au chimbuko la soka tunalicheza sisi kwa sasa pia wanawachezaji wenye uzoefu na ubora wa hali ya juu kabisa kama Mess na Iniesta.... kwakweli kwajinsi beki zetu zilivyo sioni jinsi tunaweza kumzuia Mess pia ata eneo la viungo kuna watu mahiri kama Busquet na Raktic wapi vizuri sana.

Pili buyern nao imekua ni timu tishio sana huko kwao Germany yani hawakamatiki hawa jamaa na wanawachezaji wazuri sana ukimuangalia mchezaji mmoja mmoja unaweza kata tamaa ata kabla ya game

All in all yote yanawezekana hayo ni mawazo yangu tu. Mungu ibariki City
 
Inavikombe vingapi? Imevichukuw mwaka gani na mwaka gani? Wew naona unajuw historia yake vizuri.
Historia ya City naijua kwa kuwa si kuubwa sana.
City kuanzia mwaka 1894 mpaka mwaka 2018 ime chukua makombe 14
Lakin kuanzia mwaka 1894 mpaka 2008 ilichukua makombe 7
Akaja mwarabu
Kuanzia mwaka 2009 mpaka mwaka 2018 imechukua makombe 7.
Na kuanzia mwaka huo ndio The oil money came in.
 
Tema mate chini
Bora mkutane na timu yyte kwa sasa ila si Madrid.
 
Wew si ndo ulisema imeanzishwa 2009? Au alikuw mwingine?
 
Ni mabingwa watetezi.
Pia wana rekod nzuri UCL

Kama Wigan, Liver, Shakhtar, Basel waliwafunga kwa nn Madrid washindwe?
V. real, girona,R. betis, espanyol, tot na barca wamewafunga kwann Man city washindwe?
 
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]
Nikisema chelsea imeanzishwa 2004 unadhani namaanisha exactly?

Its just Litelary tuu. Mafanikio ya City yameanza mwaka huo.
Mwaka huu city kapata mafanikio gani mkuu?
 
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]
Nikisema chelsea imeanzishwa 2004 unadhani namaanisha exactly?

Its just Litelary tuu. Mafanikio ya City yameanza mwaka huo.
Mkuu naomba nijuw we ni team gani?
 
Kachukua Kombe la EFL
Yuko Robo final ya UCL
Ni bingwa mteule wa EPL
Probably atakuwa timu ya kwanza kumaliza ligi kwa point 100 na zaidi.
Kwa vigezo hivyo sasa hukutakiwa kusema kwamba city wameanza kupata mafanikio mwaka huu kwa sababu uliyolist hapo hakuna geni ata moja kwa City
[emoji460]Kama hyo EFL tumeshachukua sana hii ni mara ya 5 sasa kama sikosei.

[emoji460]Robo final UCL sio mara ya kwanza kuingia tulishaingia tukiwa na Pellegrin msimu wa 2015-16 kama sikosei..

[emoji460]Bingwa uteule siwezi kusemea maana bado huo uteule hatujapewa na haitakua mara ya kwanza kuchukua kombe la EPL

[emoji460]Kufikisha points 100 na zaidi pia siisemei sababu bado hatujafikisha na sina uhakika na hilo kama litatimia

Labda ungesema mwaka huu cty wapo kwenye ubora zaidi ndio ingeleta maana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…