The Manchester City (The Citizens) | Special Thread

Nyie mashabiki wa kukodi ina maana hamuoni kinachowatokea pale etihad? Thread imepoa kama uji wa mgonjwa aliebadilika hali ghafla!
 
Numbisa tafadhali wajuze hawa watu,FT manc 2v 3 manu. Ubingwa kwenu hadi mtoe jasho game mbili zaidi kama mtabahatika. Huu wakati wa kutoboka ovyo nilijua utafika tu ila sikutegemea siku kama ya leo halafu nyumbani
 
Kama kukutana na Manchester united beki wetu ametoka hivi je tukikutana na spurs si ndio atapasuka kabisa!
 
Madogo mlishangilia sana mechi ya kwanza tumewanyoosha hapo hapo kwenu mkubwa ni mkubwa tu
 
Ndugu zanguni hongereni kuwa mabingwa wa EPL lkn tukija kwenye mashindano ya wanaume ya UCL hamuwezi mtoa Liverpool!
Game ilimalizwa na Mane dakika ya 30,lkn mwakani mkipata beki nzuri za kati mnaweza mkawa wazuri zaidi kwenye mashindano ya wanaume UCL
 
Mkuu wa zamani wa waamuzi England Keith Hackett haelewi ni kwa nini Martin Atkinson hakumfukuza wuanjani beki wa Manchester United Ashley Young wakati wa mechi yao dhidi ya Manchester City. Amesema vitendo vya Atkinson ni thibitisho tosha ya kuonesha ni kwa nini waamuzi wa England waliachwa nje ya michuano ya Kombe la Dunia mwaka huu. (Telegraph)

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amesema pendekezo la Manchester City kwamba klabu hiyo inaweza kutumia uwanja wake wa mazoezi kwa maandalizi ya mechi ya marudiano ya robofainali Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Jumanne lilitolewa kwa kuchelewa.

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amesema huenda ndiye anayefaa kulaumiwa kwa klabu hiyo kulazwa na Liverpool na Manchester United. Hata hivyo amesema kutomakinika mbele ya lango kuna maana kwamba timu hiyo bado haijatosha kushindana katika ligi kuu bara Ulaya. (Times)
 

Leo mazoezini
Habari mbaya sana kwa Man City
Mnyama Salah kafanya mazoezi leo dakika zote!
Man City kazi mnayo aisee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…