The Manchester City (The Citizens) | Special Thread

Ndio maana wapenzi wa Arsenal huwa tunampa heshima zake Wenger pamoja na mapungufu yake
 
Mshukur Mungu upepo umemkalia vizur epl la sivyo msimu huu angetoka tena mikono mitupu timu ya makombe manne hahahahahaha
 
mnapenda kukimbia kauzi kenu ha ha ha ha🙂🙂🙂🙂🙂🙂🙂
 
Man city daima haina mashabiki,hawa walioko humu ni wakwepa majukumu ya timu zao mbovu kama arsenal na chelsea. Sasa Klopp anawatafuta mrudi kuwajibika kwa maamuzi yenu. Huku pia mmeachwa uchi kabisa,kumbukeni mnamiliki QARABAO peke yake hadi sasa
 
Liverpool imefika katika nusu fainali yao ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa kwa miaka 10 baada ya kujikokota na kuishinda Manchester City kwa kupata ushindi wa mabao 2-1 yaliyoleta ushindi wa jumla wa Liverpool 5-1 Man City.
City walianza vizuri wakati walipojaribu kulipa deni la 3-0 walizofungwa katika mechi ya kwanza. Ilikuwa dakika ya pili tu ya mchezo ambapo Raheem Sterling alimwanzishia Gabriel Jesus aliyeitumia nafasi hiyo kupachika bao la kuwapa matumaini Man City. Hata hivyo baada ya tukio la vurugu kabla ya muda wa mapumziko lililoisha kwa Meneja Pep Guardiola kuondoshwa katika eneo la benchi la ufundi, City hawakuweza kuyafikia matamanio yao.

Tukio lenyewe lilianzia pale ambapo Bernardo Silva alikuwa amepiga mkwaju kuelekea lango la Liverpool, huku Liverpool ikiwa katika shinikizo zito, mpira ukamkuta Leroy Sane ambaye aliukwamisha wavuni na kuwafanya City kudhani wamefanikiwa kupata goli la pili.
Lakini hali ilikuwa tofauti kwani mwamuzi Antonio Mateu Lahoz alilikataa goli hilo kwa madai kuwa limepatikana katika mazingira ya kuotea yaani offside, jambo ambalo limemkera Pep Guadiola aliyeingia uwanjani kumkabili mwamuzi Antonio Mateu Lahoz, na hivyo meneja huyo wa City kuambulia kufukuzwa katika eneo lake la ufundi hali iliyomfanya kulazimika kuitizama kipindi cha pli akiwa katika viti vya mashabiki.

City wakijaribu kupambana katika mazingira ambayo mwalimu wao yuko mbali, wakapoteza mwamko na kuwapa nafasi wageni Liverpool kupitia Mohamed Salah akajipatia bao lake la 39 la msimu baada ya mbio za nguvu kutoka kwa Sadio Mane mnamo dakika ya 56.
Goli zuri la Robert Firmino dakika 13 kabla ya kumalizika kwa mchezo, limekuwa msumali wa mwisho katika jeneza la Man City na hivyo kuwahakikishia Liverpool kusonga mbele.
Sasa Liverpool wanasubiri kuwajua wapinzani wao katika nusu fainali wakati droo itakapochezeshwa Ijumaa [12:00 BST] huko Nyon, Uswisi.
 
Watani poleni sana
The good thing mtatwaa EPL weekend hii
Mna timu nzuri sana ila fatigue imewacost
 
Kayeke kakimbia jukwaa aisee siju nae ni shabik wa kukodi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…