The Manchester City (The Citizens) | Special Thread

Aisee, Pep akubali tu kwamba UEFA sasa basi. Atukomalie tu PL.
Waarabu wataendelea kumvumilia ?

Yawezekana wakaachana nae wakatafuta kocha mwingine.

Toka ameondoka Barcelona anaishia robo finali tu havuki hatua hii anachomolewa akiwa Bayern katolewa mara tatu,Man city hii ya tatu pia.

Bado anajipya la kuwaambia waarabu ?
 
Bebwalona ile hata kama wewe ungekuwa kocha ni lazima ungebeba makombe tu, UEFA ni ya Wanaume mkuu. Pep atjipumzikie tu kufundisha mpira kwa matarajio ya kubeba kikombe cha UEFA atanenepa pia
 
Bebwalona ile hata kama wewe ungekuwa kocha ni lazima ungebeba makombe tu, UEFA ni ya Wanaume mkuu. Pep atjipumzikie tu kufundisha mpira kwa matarajio ya kubeba kikombe cha UEFA atanenepa pia
Haha alishindwa kuutwaa akiwa na Bayern ya moto ile kina Muller, Lewandoski,Thiago, Ribbery na Roben.
 
Pep anakimbilia kununua wachezaji tu.

Angalia atakavyoingia sokoni kwa hasira.
 

Binafsi sielewi tatizo ni nini kwa Pep, na wakimtimsha watapata kocha gani wa kuwapa UEFA?

Accuracy ya Barca kipindi cha Pep ilimbeba sana jamaa kuchukua UEFA.

Nahisi kutopata wachezaji wa caliber ya Xavi, Iniesta na Messi kutaendelea kumtesa sana. Kwa hii City, kwenye huo utatu namwona KDB peke yake.
 
Hana wachezaji threat kwa timu pinzani pamoja na vipaji vyao lakini wanadhibitiwa kirahisi sana.

Kwenye timu yake anahitaji wachezaji watatu au wanne wenye calibre ya Kelvin De Bruyne alikuwa nao lakini watatu wawili wameshaondoka Silva na Company.

Atafute watu wanaoweza kubeba timu katika mechi kubwa.

Kwa sasa ana group la vijana wajanja wajanja tu.

Klop katengeneza timu ambayo collectively inatisha sana lakini pia wachezaji individually wanatisha sana.
 
Bado hamuamini pa1 na Pep kuweka rekodi za kutwaa makombe ya ligi za Bundesliga na EPL lakini bado anaendelea kuwa kocha dhaifu sana.

Tukiweka chuki na ushabiki pembeni Pep aliikuta Buyern Munich ikiwa bora sana chini ya yule kocha Babu aliyestaafu baada ya kuchukua nayo ubigwa wa UEFA dhidi ya Borussia Dortmund. Ile timu isingekuwa Pep, ingeendelea kuwa tishio sana Ulaya kuliko baada ya Babu kustaafu na kuchukuliwa na Pep.
 

Kama ulivyosema, timu nzima amebaki KDB peke yake.

Aguero majeruhi na umri umeshamkataa, ingawa pia hakuwahi kuwa extra ordinary, ila alikuwa anafit sana.

Tusubiri kuona adjustments atakazozifanya.
 

Pep kwangu bado ni one of the best coaches, top 3 kama siyo top 5.

Swala la kutochukua UEFA akiwa na timu nzuri halisababishi mimi nimtoe kwenye makocha wazuri.

Shida moja inayombana ni flexibility, anataka kutuprove tofauti kuhusi tik tak yake, lakini muda unaenda na hapati ile exact fit ya kujaza puzzle yake.

Ni swala la muda, anaweza kupata pieces za kujazia puzzle akashinda UEFA, au akaamua kuwa flexible kwenye style yake ya mpira akachukua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…