The Manchester City (The Citizens) | Special Thread

The Manchester City (The Citizens) | Special Thread

Naona man city wamerud kwenye level term! Good work by Yaya Toure!!
 
Suarez kaharibu furaha ya Man City!! Its liverpool 2 man city 1
 
Comentator kanifurahisha sana...anaanza Geraaaaaad, wakat hata Gerad mwenyewe hajaachia mnduki!! Hawa kumbe huwa wanakariri!!
 
Huyu sketi mbona anauza timu?
Damn! Hawa noisy shitty neighbours wataleta shida hapa mtaani.
 
X7c7qtqY0mxOQlJvjig04f3mEu3yXslKnu0gT7VfwVhys+f8GX1C1uEbENAcAAAAASUVORK5CYII=


Scott Sinclair ameihama klabu ya ligi kuu ya Premier ya Swansea, na kujiunga na Manchester City, kwa kutia saini mkataba wa miaka minne.

Klabu hiyo ya Wales awali ilikataa pauni milioni 6.2 kutoka kwa Man City, lakini hatimaye baada ya nyongezanyongeza, hatimaye kwa jumla Man City ikafikisha pauni milioni 8.
Sinclair, mwenye umri wa miaka 23, hivi majuzi aliichezea Uingereza katika mashindano ya Olimpiki, na huenda akawa katika kikosi cha meneja Roberto Mancini ambacho kitapambana na Queen Park Rangers siku ya Jumamosi.
"Ninafurahi sana kwamba yote yametulia, na sasa mimi ni mchezaji wa City....ni vigumu hata kusubiri," alielezea Sinclair.
"Kulikuwa na nyakati ambazo nilifikiria hayo hayatawezekana, kwa hiyo nimeridhika kwamba hatimaye nimefika hapa."
"Kucheza ukiwa na baadhi ya wachezaji maarufu zaidi ulimwenguni ni jambo ambalo linasisimua. Wakati unapotizama ratiba na kuona mechi mbili dhidi ya Real Madrid katika ligi kuu ya klabu bingwa, basi unahisi ukweli wa yote haya."
Meneja wa Swansea, Michael Laudrup, alisema "Scott anaelekea kwa klabu kubwa ambayo ina wachezaji maarufu. Yeye ana maarifa mengi, lakini itabidi ashindanie nafasi ya wachezaji 11 watakaokuwa uwanjani mara kwa mara."
Sinclair zamani alikuwa akiichezea timu ya is England ya vijana chini ya umri wa miaka 21, na alianzia Bristol Rovers, kabla ya kujiunga na Chelsea.
Lakini baada ya kutoweza kushirikishwa katika mechi mara kwa mara katika uwanja wa Stamford Bridge, alihama kwa mkopo katika timu ya Plymouth, na pia kuzichezea QPR, Charlton, Crystal Palace, Birmingham na Wigan, kabla ya Swansea kuamua kumchukua mwezi Agosti, mwaka 2010, kwa pauni 500,000.
Sinclair alicheza mechi 82 chini ya klabu ya Swansea, na alifunga magoli 28
 
Maicon, aliyeiwezesha Inter Milan kupata vikombe vitatu muhimu mwaka 2010, na ambaye hivi majuzi aliandamwa na majeraha mengi, sasa ataichezea Man City.
120831153147_maicon_304x171_bbc_nocredit.jpg
Maicon ni kati ya wachezaji kadha wapya watakaoichezea Man City msimu huu


Wengi wanaamini siku zake za kung'aa zimepita, lakini kuna baadhi wanaofikiria kwamba Maicon ni kati ya wachezaji bora zaidi wa ulinzi ulimwenguni.
Meneja wa City, Roberto Mancini, aliweza kumfunza Maicon, mwenye umri wa miaka 31, alipokuwa meneja wa Inter kati ya mwaka 2006 hadi 2008.
Mchezaji huyo wa Brazil alianza kuichezea klabu ya Cruziero, kabla ya kuisakatia gozi Monaco, na kisha kuelekea Inter, aliposhiriki katika mechi 235 za ligi ya Serie A.
Maicon atajiunga hivi karibuni na wenzake katika timu ya Man City, mara tu baada ya kipindi kifupi cha mechi zijazo za kimataifa.
Ingawa hucheza nyuma, ana sifa za kushambulia ghafula, na alifanikiwa kuifungia Inter magoli 20, na ameichezea timu ya taifa ya Brazil mechi 70.
Mchezaji huyo mpya wa Man City sasa atakutana na wachezaji wengine waliosajiliwa hivi karibuni katika klabu hiyo ya uwanja wa Etihad, kama vile Scott Sinclair, kutoka klabu ya Swansea, na mlinda lango Richard Wright.
Wachezaji wengine ambao huenda wakasajiliwa na Man City ni kiungo cha kati Javi Garcia na kutoka Benfica ya Ureno, na Matija Nastasic, mlinzi wa klabu ya Italia, Fiorentina
 
there players out there that i respect alot especially those who dont get lured by the richness of other clubs...cavani de rossi wangetaka hela ungekuta wako man city leo..but wamekataa hela na kubaki na team wanazozipenda..well done
 
there players out there that i respect alot especially those who dont get lured by the richness of other clubs...cavani de rossi wangetaka hela ungekuta wako man city leo..but wamekataa hela na kubaki na team wanazozipenda..well done

brother we mnafiki alafu una ushabiki wa kitoto sijaona JF...we si ndo ulikuwa unampondo Alan Shearer kuikataa Man United kwamba alipishana na Medals? Huyo De rossi na Cavani wamebakia waliko kwa kuwa huko waliko wanathaminiwa sana wameshinda Medals ngapi?

David Ginola,Giafranco Zola,Shearer,Gascouine,Les Ferdinand Hawakuhamia timu kubwa EPL na Sasa wanaheshimika kuwa manguli wa vilabu vyao...

Jamaa una unazi wa manchester utd mpaka nahisi utakuja kudata...ulivyo glory hunter mkiingia kwenye kipindi cha Downfall (kila kilicho juu uanguka) kama madrid mwaka 2003 mpaka 2007 utakimbia JF...POLE SANA MNAZI
 
Kashengo taratibu bana utaacha jamaa akimbie tupo kwenye sports hapa khe khe keh kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee

Nani anashinda kipute cha leo .... .... ..
 
Back
Top Bottom