ndetichia
JF-Expert Member
- Mar 18, 2011
- 27,767
- 6,575
Sikiliza ndetichia Hii sheria inaanza next season kufanya kazi 100% ila kuna jambo wengi hawalielewi UEFA hawazuii timu kupata pesa kupitia wadhamini ili kupunguza madeni yake pamoja na deficits (spending>incomes) unawasema Chelsea wao si wajinga kutokana na sheria hii wame renew mkataba na Samsung kuwadhamini T-shirts kwa miaka mitatu ijayo na watavuna pound 15 millioni kwa kila msimu,bado ukumbuke wameingia mkataba na kampuni ya Gazprom mabayo inahusika na uuzaji na usambazaji wa gesi,ongeza pound 47 milioni walizopewa kama zawadi ya kushinda UCL....na timu ya Manchester City wao mwaka jana walijua itawakuta hii deficit then wakasaini mkataba na kampuni ya ndege ya ETIHAD airways kwa pound 400 millioni ili kupunguza Hasara waliokuwa wameitengeneza msimu uliopita ya pound 197 millioni katika kununua wachezajina mishahara
Man utd wanasemekana kuwa na deni linalofikia pound 445millioni (kama sijakosea figures) ila wao walikwenda zao marekani wakauza Hisa kule Newyork stock exchange kwa mara ya kwanza (initial public offering) na wamefanikiwa kupata kiasi kikubwa cha fedha kupunguza deni na bao hapo hapo wametengeneza faida kubwa kuliko club yeyote duniani kwa mwaka jana na ukizingatia wamenunua wachezaji kwa pesa isiyozidi pound 40 millioni (RVP,KAGAWA,BUTTNER,POWELL, na Fernadez)...na ukumbuke mkataba wao na Chevroet unawaingiazia pesa sawa?
hizi timu 23 zinadeni linalozidi pound 45 millioni kwa sasa na baadhi hawajalipa mishahara,kodi n.k...kuanzia msimu huu timu inaruhusiwa kutozidisha deficit ya 45 millions poud ilaitaenda inapungua mpaka kufikia hasara isiyozidi pound millioni 8 mwaka 2018 ndo mambo yako hivyo...UEFA hawajamuonea yeyote waliyoona mambo yatakuwa magumu kwao kama AC milan wameuza nyota wao karibu wote kupunguza mishahara mikubwa na kupunguza madeni ili kuendana na sheria hizi, ebu itazame ishu ya David silva pale Man city amekataliwa mkataba mpya wa pound 200,000 kwa wiki na uwezekano wa kusepa baada ya huu kuisha ni mkubwa hata Chelsea wamemgomea Ashley Cole mkataba wa miaka 2 kwani unakuwa na gharama kubwa wakamwambia ni mwaka mmoja kama hawezi atafute pakwenda (hata Drogba hali ilikuwa hivi hivi)
Timu kama LIverpool imetangaza kuwa inauza Stadium naming right yake ya ANFIELD kama mwekezaji atakuja na pesa nzuri basi uwanja wao utakuwa na jina jipya ili wapate mapato mapya mengine..nadhani unaona Britania stadium,Dw stadium,Etihad stadium,emirats stadium na hata newcastle nasikia umeuzwajina toka st. james's park
Sheria hii itadhibiti timu kutfirisika kama Portsmouth,rangers,Leeds utd na malaga....na Transfers za pesa nyingi zitasahaulika siku si nyingi kw3ani sioni tena club ya kumnunua mchezaji kwa poud 80 milioni tena kwa sheria hizi...ukumbuke kuwa timu hazitotofautiana sana mishahara kiasi timu ndogo zitaweza ku hold on kwa wachezaji wao nyota
Ebu fikiria Timu yako kumuuza Adebayor (pound 170,000 per week) na De Jong na Adam Johnson, ambao probably walikuwa na mshahara mzuri mpaka kuwaleta scott sinclair, jack Rodwell, garcia mabao bado hawatalipwa kama hao waliosepa..hapo ndipo wanabana Matumizi
hapo nimekupa kaka mkubwa maana nilijua wanataka kudhibiti timu ambazo zinataka kuwa na mafanikio kama timu kubwa kumbe wameona wenga anawapiga bao nini kwa ubahili wake..