PSG ni timu bora. Na wanastaili pongezi. Sijawahi kuwa mfuatiliaji wa soka hapo nyuma ila niliingia ktk sika kipindi mancity anamtandika man u goli 6 kwa moja. Ila kwa mpira wa psg walioucheza na man u jana. Mpaka kuichabanga man u goli mbili kwa nunge, ingenguwa ni man city tungelala pia tena kwa goli nyingi zaidi. Maana man city angecheza kwa kujiamini kuwa watashinda ila kwa mchezo wa jamaa jana ingekula kwetu. Mbappe anaspidi ya ajabu sana. Ila man u aliingia akijua kabisa atapigwa kwahiyo alicheza kujahami akacheza kila aina na mpira mpaka kupata red card.
Ila sisi kama city tumejifunzia kwao. Hiyo siku ya fainali maana itakuwa kati ya city na psg. Tutawabwaga.
Ila namuomba Pep asiweke wachezaji wenye hasira. Tutakula red.