Kitumba_
Member
- Aug 21, 2018
- 30
- 21
Kikubwa na cha muhimu zaidi kuzingatia, sio yale ya nyuma yalopita bali yajayo na Tanzania yetu hii. Hakuna la kuficha tunaishi kwenye wakati mgumu sana na mambo hayaendi kuwa mazuri huko mbele. Kuendekeza kusifia sifia na uchawa ili kujipatia utajiri, ulinzi wa mali na uhuru wa kifedha KAMWE! Sio chaguo sahihi, viongozi wetu na wafanyabiashara wakubwa sidhani kama wanalitizama hili kwa jicho la tatu.
Juma asaivi ni wa tofauti sana ukizingatia maisha yake miaka miwili mitatu nyuma iliyopita. Alikua akijitafuta huku na kule na akiitafuta maana ya yeye kuishi hapa Duniani. Alifikia mpaka kulima bustani ya mboga za majani kando ya mto wa maji machafu pale Savei na degree yake. Alikua mpiga ‘winga’ wa limao na tangawizi wakati ule wa janga la COVID 19. Alijengeka na kuwa mjasiliamali.
Aliisaka kazi usiku na mchana aweze kuisapoti familia yake. Kutoboa kwa kutegemea ajira kwenye taifa letu hili imekuwa mtiti. Tanzania ya mwaka wa kufosi nimemuona Juma akitoka kwenye gari lenye plate namba ‘STL’. Aliukacha ujasiliamali na kuwa hodari wa kuunga juhudi za viongozi na wafanyabiashara wakubwa. Kumbe alikua ana kipaji cha uchawa.
Zaidi ya asilimia 60% ya watanzania ni vijana kama Juma. Kati ya hao kwa haraka haraka ni asilimia 10% pekee ndio imeajiriwa kwenye mifumo rasmi. Tuseme mifumo isiyokuwa rasmi (wajasiriamali kama alivyokuwa Juma hapo mwanzo) inaajiri 5% ya vijana. Tanzania yetu ya leo inawataka asilimia zote hizo zilizobaki za vijana wakawe machawa! Viongozi na wafanyabiashara wakubwa wanawatunuku machawa kama Juma kila leo.
Kila mmoja wetu hapa anatamani kuwa MTU, tena kuwa Mtu wa Maana kabisa kama wasemavyo, lakini leo hii sio kila mtu anatamani ama anasapotiwa kwenye mchakato wa kuwa MTU.
Mchakato wa kufanikiwa ndio umfanye mwanafunzi kuwa Mwalimu. Mchakato wa kufanikiwa ndio uumfanye mwajiriwa kuwa BOSS. Mchakato wa kufanikiwa ndio uumfanye mtu asiyejulikana kuwa mtu maarufu. Mchakato wa kufanikiwa ndio uumfanye masikini kuwa tajiri na kuwa mtu wa maana…. Kama maisha ya leo yanatufanya kupendelea matokeo mazuri badala ya kupenda michakato yakutengeneza hayo matokeo hapo ndio shida ilipo.
Ukosefu wa ajira Mara zote hutumika kama kipimio cha afya ya Uchumi wa taifa fulani. Ukosefu wa ajira unakumba karibu kila makundi ya umri lakini ‘incidence’ kubwa hutokea kwa vijana. Watu wazima wana fursa nyingi ukilinganisha na vijana. Vijana wakikosa kazi ndipo uhuni, ukabaji, uvutaji bangi na mihadarati, maandamano, nakila aina ya disturbance utaiona. Vijana ni moja ya resource muhimu sana ambapo kama taifa na wafanyabiashara wakubwa inabidi wawekeze ili kukua kwa uchumi na maisha bora.
Kijana mwenye Nguvu, Uchu, Ari na aliye na vigezo ana uwezo wa kuleta mabadiliko makubwa katika jamii imzungukayo na taifa kiujumla. Kijana asapotiwe kwa ule uchu wake wa kufanya jambo fulani. Viongozi, mashirika na wafanyabiashara wakubwa wanapaswa kusapoti jitihada na michakato ya vijana kujikwamua na wimbi la umasikini na sio kuwapa dezo kwa kigezo cha kujiangalia wao, eti wamesifiwa.
Asaivi makampuni makubwa yamewekeza nguvu kwenye ‘Machawa’ ili kuijenga ‘efficiency’ ya wanachozalisha ama wanachohudumia jamii. Lau wangeweka asilimia kadhaa kwenye bunifu, mafunzo, na tafiti & maendeleo wangejihakikishia ukuaji wa kampuni yao na kupanuka kimataifa, kutengeneza ajira nyingi kwa vijana na kukuza uchumi wetu na hivyo maendeleo.
.
Nitoe rai tu, hili sio andiko kama maandiko mengine mliyosoma hapa Jamii Forum, hii ni “Master Class in System Leadership, MCSL’. Ukiwa kwenye mfumo, kiongozi pahala Fulani ama mfanyabiashara mkubwa kuliko kupandisha bei za bidhaa unazozalisha/sambaza ili kufidia gharama ya fedha unazotoa kwa Machawa eti unakuza Soko fuata hii Dira ya ‘Professional Development’ kama nyenzo ya kujijengea utajiri, usalama wa mali zako na uhuru wa kifedha.
Picha na Mtandao.
Makosa mengi yamefanyika na yanaendelea kufanyika, lazima tuangalie mbele. Tukiifuata hii MCSL haihitaji kiongozi fulani kubwata mbele ya hadhara kuipata ‘Fame’ ya kutatua matatizo yetu mengi tuliyonayo, mfumo wenyewe utatatua kero zetu kila engo na kuyapata maendeleo endelevu.
Mchoro hapo juu unaweza kutazamwa. Naomba kuwasilisha.
#Ndarihoranye.

Upvote
2