P h a r a o h
JF-Expert Member
- Mar 25, 2024
- 785
- 1,413
waliweza kuliangalia kwa takriban dakika 15 bila kuumia macho,
waliokua wanaliona walisema lilikua linatoa mwanga kwa rangi tofauti tofauti, pia lilionekana kama linazunguka,
huku likionekana kuisogelea dunia na baadae likarudi katika umbali wake wa kawaida.
Ilikuaje takriban watu 70,000 wakusanyike siku hiyo kuliangalia jua ?
- kila kitu kilianzia kwa watoto watatu:-
Jacinta Marto,
Fransisco Marto,
na binamu
yao Lúcia dos santos
Hawa watoto ni ndugu, Jacinta alikua na miaka 07, kaka yake Fransisco 09, na binamu yao Lucia 10.
siku moja walipokua wanachunga tarehe 13 may 1917 waliona kitu kilicho washangaza...
mkubwa wao ( Lucia ) akawaambia wasiende kutangaza wakirudi nyumbani.
walipofika nyumbani yule mdogo ( Jacinta) akashindwa ku kaa kimya akamwambia mama yake...
leo tulivokua tunachunga tulimuona bibi mzuri anang'aa, mzuri amevaa nguo nyeupe
ametuambia tuwe tunasali Rozali na atakua anakuja kila mwezi.
kama ilivyokua kawaida ilikua ni kitu ambacho hakiingii akilini unapo ambiwa habari kama hiyo, na ikizingatiwa ni watoto ndo wanaoleta hadithi hizo, mama yao aliwapuuzia,
tarehe 13 june 1917 wakaenda tena pale kama walivyo ambiwa yule bibi yao walio muona siku ile ( Bikira Maria )akawatokea tena kama alivyo waahidi waje siku hii,
hii siku akawaonyesha maono jinsi Jehanamu palivyo
aka ahidi kuwachukua wale ndugu wawili, Jacinta na Fransisco Marto ( wote wawili wakafariki miaka miwili baadae )
akamwambia Lucia atabaki duniani muda mrefu ili kusambaza ujumbe wake ( Lucia aliishi hadi mwaka 2005 )
hizi habari zilivyozidi kusambaa, hawa watoto wakapata umaarufu zaidi na upinzani pia vitisho n.k... kutoka kwa wasio amini
Tarehe 13 july 1917
Bikira maria akawatokea tena hii siku akawaambia kuhusu vita ya kwanza ya dunia na kuwaambia wasali zaidi Rozari kuombea amani na vita ya kwanza itaisha muda sio mrefu
( kipindi hiko vita ya kwanza ya dunia ilikua ikiendelea )
pia akawaambia watu wasipo mrudia Mungu itatokea vita kubwa zaidi ya hiyo ( vita ya pili ya dunia ) ambayo pia kabla haija anza dunia itapewa ishara.
Tarehe 13 August 1917
walikua gerezani siku hii, walifungwa ili wahojiwe kwasababu habari hizi zilisambaa mno, kwahiyo waliwekwa ndani kwa muda wakiwa wanahijiwa
Tarehe 13 September 1917
siku hii watu wengi waliwafuata ili na wao wakamuone Bikira Maria atakapo watokea,
lakini Bikira Maria alikua anaonekana na wale watoto watatu,
wengi wao hawakuweza kumuona
Bikira Maria akahaahidi kujidhihirisha kwa watu wote mwezi ujao yaani tarehe 13 October 1917
kwa miezi hiyo mitano habari zikikua zimeshasambaa sana watu wa karibu na wengine wa mbali walikuja ili kuisubiri tarehe 13 mwezi wa 10
Tar 13 October 1917
zaidi ya watu 70,000 waliokusanyika wakimsubiri Bikira Maria,
wakaanza kushuhudia Jua likifanya mambo yasiyo ya kawaida,
Jua lilishuhudiwa kwa takriban dakika 15 likizunguka, likitoa miale ya rangi tofauti likishuka kuikaribia dunia na baadae kurudi lilipokua.
muda wote huo watu waliweza kuliangalia bila kuumia macho.
kushuhudiwa huko na maelfu ya watu kukafanya tukio hilo lijulikane kwa kasi dunia nzima.
April, 4 1919 - Fransisco Marto alifariki
February, 20 1920 - Jacinta Marto alifariki
Mwaka 1930 baada ya tafiti za kanisa Catholic, kanisa likautambua rasmi huo muujiza na kuanza harakati za kuwatangaza Jacina na Fransisco kua watakatifu,
Mwaka 1938 January 25 hadi 26 Jua lilikua likitoa rangi ya tofauti ( aurora borealis )
kitu kilicho ibua hofu kwa watu wengi sana siku mbili mfululizo
1939 vita ya pili ya dunia ikaanza wakakumbuka ule mwanga wa jua ulikua ni ishara waliyoambiwa watapewa ( hii vita ya pili ilikua kubwa sana ikahusisha hadi matumizi ya mabomu ya atomic yaliyo lipua Hiroshima na Nagasaki )
Baada ya kanisa kuwatambua:-
September 12, 1951 walitaka kuhamisha mabaki ya miili yao kwenda kuizika upya Kanisani,
waliikuta miili yao ipo vile vile kama ilivyozikwa miaka 32 iliyopita. haijaharibika kabisa.
Lúcia dos Santos alifariki February 13, 2005
Muujiza wa Jua ndio muujiza ulioshuhudiwa na watu wengi zaidi tariban 70,000 hadi 100,00 wanakadiriwa kushuhudia siku hiyo,
ukishuhudiwa na waandishi wa habari, watu wasio amini na wanao amini,
umebaki kuwa Supernatural phenomenal iliyo ripotiwa mara nyingi zaidi.