Naona wengi wenu mmekuwa na hisia zaa "ukabila" zaidi kuliko ambacho nilitaka nimaanisahe hapa.Labda kama tunatofautiana hisia na uelewa, kuataja, kusifia kabila fulani sidahni kama ni ukabila!.
Binafsi sitetei ukabila na pia kutokuwa mkabila haimanjisni sina kabila na kuwa taifa haina maana dhana ya kuwa wa kabila fulani inafutika vinginevyo tusingeongea lugha za makabila wala kujitambulisha asili zetu za kikoo, kitamaduni, mila na desturi za kule tutokako.
Ipo historia mzuri kabisa kuhusu "makabila ya kitanzania na mengine ya Afrika kwenye vitabu na kumbukumbu za kale kama vile kiatbu cha "Zamani Mpaka Siku hizi" . Katika maandhish hayo, unasoma kusifiwa au kukashfiwa kwa makabila fulani kutaoka na aina za utamaduni na maisha waliyoishi enzi hizo. Hata hivyo maandishi hayo, haya maanishi ukabila bali kuelezea hali halisi ya kabila husika. Tukisema kwa mfano wahaya wanapenda sana kuongea lugha ya kwao, hii haimannisha wahaya ni wakabila kwani wasipofanya hivyo, hawawezi kuitwa tena wahaya, kwani wanaitwa wahaya kutokana na hilo kabila.
Kwa mfano tukiseme kabila la Wahehe, Wanyamwezi na Wangoni ndiyo yenye msimamo mkali zaidi katika makabila yote Tanganyika kwa kurejea vita dhidi ya kutawaliwa na Mjerumani, haimaanishi kutaja makabila hayao ni ukabila, hii ni hali halisi kwa mujibu wa historia ya Makabila husika na ukweli huu hauwezi kufutikwa millele hata Taizania ikiwa nchi yenye kabila moja!.
Turudi kwenye mada na kuelewa mantiki, sina dhamira ya ukabila hapa bali ni kuangalia kama upo uwezekano wa kila kabila kutunza kumbukmbu zake katika kizazi hiki kama ilivyokuwa zamani na wote tumezikuta hizo histioria na ndizo zatufanya leo tujiite "sisi ni wakabila fulani" na tuliwa pamoja kama hap kwenye JF twasema sisi ni wataifa fulani (utaifa na ukabila ni sawa) . Makabila ni tofauti na ukabila, Makabila ndi yanajenga "Taifa"na badaae "Mataifa".