P h a r a o h
JF-Expert Member
- Mar 25, 2024
- 785
- 1,413
Dunia ni uumbaji unao ishi na kupumua, uliozungukwa na nguvu zisizoonekana,
nguvu hizo ndizo zinaifanya dunia iendelee kuishi, na kuruhusu uhai na kuifanya iendelee kua hivi tunavyoiona kwa mamilioni ya miaka.
nguvu ya usumaku au ya uvutani wa dunia ( Earth's Magnetic field ) hutumiwa na ma elfu ya aina mbalimbali za wanyama, angani, baharini hata chini ya ardhi kama muongozo wa uelekeo. kwa kujua au kutokujua.
Lakini je ni vipi kuhusiana na Binadamu?
Tuna uhusiano wowote na nguvu hii ya asili uvutano?
Au hatuna kabisa uwezo wa kuitambua?
Dira, hiki kifaa kilichogunduliwa zaidi ya mamia ya miaka iliyopita, kinatumia nguvu ya uvutano wa dunia kuweza kutambua uelekeo, (Kaskazini na Kusini )
Lakini je huu ndio uhusiano pekee na muunganiko wetu na nguvu hii?
ingawa binadamu anaonekana mwenye uwezo mkubwa zaidi wa akili kuliko viumbe vyote duniani, lakini si binadamu pekee mwenye uwezo wa kutumia nguvu hii kujua uelekeo, hata ng'ombe tu wanaweza pia
Tafiti zinaonyesha kwamba n'gombe na wanyama wa jamii yao wanapokua katika maeneo makubwa ya wazi huelekea upande wa (kaskazini - kusini,) wakiendana moja kwa moja na nguvu hii ya uvutani ya dunia
wataalamu wa tabia za wanyama wanasema
"Huenda N'gombe hujikuta wapo katika uelekeo huo bila kujua au wao kujiweka wenyewe ( subconsciously ) lakini kua katika uelekeo huo huwasaidia katika mmeng'enyo na shughuli mbalimbali mbali za kimwili,
pia hujihisi salama zaidi wakiwa katika uelekeo huo"
chini ya ardhi, wakandarasi hawa wa asili mchwa, wanajenga nyumba zao kuendana na nguvu ya uvutani wa dunia
vichuguu vinavyoweza kusimama hadi urefu wa futi 30 kwenda juu, huku vikiwa vimejengwa na wadudu wadogo kabisa.
vichuguu ni moja ya majengo yaliyojengwa kwa ujuzi wa hali ya juu zaidi katika majengo yote yaliyojengwa na viumbe wa sayari dunia ( hata binadamu akiwepo)
vichuguu vya mchwa vina mifumo mbalimbali ya kudhibiti joto, hewa unyevu n.k katika kiwango cha juu sana cha udhibiti. kwa kutumia vitu vya asili tu.
bila A.C bila Umeme bila maji ya dawasa, bawasa etc... bali kwa kutumia nature tu!
wataalamu wa wadudu wanasema
"vichuguu vinajengwa kuendana na nguvu ya uvutani wa dunia
(Earth's Magnetic Field ) ambayo ni moja ya kitu kinachofanya majengo yao yawe na udhibiti mzuri wa hali ya hewa,
lakini ni kwanamna gani wanaweza kufanya hivi ?
hili ni swala ambalo binadamu ndio wanaanza kulielewa"
Juu angani, ndege wanao hama na kusafiri safari ndefu,
hata safari za kuhama bara moja kwenda jingine,
wanawezaje kusafiri kwenye mstari ulio nyooka?
kwenda wanapotaka na kurudi kwa usahihi mkubwa kiasi hiki?
Binadamu hutumia GPS au google Map katika mambo ya aina hii ila wao hawajui lolote kuhusu GPS.
"Ndege wana uwezo mkubwa wa kuhisi nguvu hii ya asili ya uvutani inasadikika pia wanauwezo hata wa kuiona nguvu hii, kitu ambacho kinawawezeaha kusafiri umbali mrefu hata kuhama bara bila kupoteza uelekeo na bila kutumia teknolojia kama ambavyo binadamu anavyotumia GPS"
Lakini hao ni baadhi tu ya wanyama wachache kati wa wengi, samaki na aina mbali mbali za wanyama wa kwenye maji wanaweza kuondoka mbali na makazi yao kwa muda mrefu na bado wakawa na uwezo wa kurudi hapo hapo bila kukosea hata kidogo
Tafiti zinaonyesha baadhi ya seli kwenye ubongo wa binadamu zinaweza kuhisi nguvu hii, ila uwezo wa binadamu ni mdogo mno kumuwezesha kuutumia katika mambo mbalimbali kama wanyama wanavyoweza,
"Baadhi wa watu hudai kuhisi Ladha ya chuma wanapokua kwenye mashine za MRI,
majaribio yanaonyesha binadamu anapokua katika nguvu kubwa mno ya usumaku huona mwanga kwenye macho ukiwaka na kuzima kama radi.
hii inaonyesha kua binadamu pia ana uwezo wa kuitambua nguvu hii endapo itapokua kwa ukubwa.
lakini nguvu ya uvutani wa dunia haijafikia kiwango cha kutambulika kwenye ubongo wa binadamu"
inatambulika pia kia nguvu hii sio kwaajili ya kutambua uelekeo tu, kama inavyotumiwa na wanyama wengi bali pia ndio hutukinga na mionzi mibaya,
huzuia mionzi yenye madhara kutufikia duniani,
nguvu hii bado ni fumbo, bado kuna mengi sana ya kujifunza juu ya uhusiano wake na viumbe hai, ikiwemo binadamu.
Kuanzia wadudu wadogo kama mchwa hadi wanyama wakubwa zaidi duniani kama papa,
kuanzia ndege wa angani, samaki na viumbe wa baharini, wote wana uhusiano wa moja kwa moja na nguvu hii ya asili.
ingawa binadamu hatuwezi kutumia nguvu hii moja kwa moja kwa kujua kama ndege au viumbe wengine, lakini mahusiano yetu na nguvu za asili kama hii inadhihirisha kua sisi ni moja kati ya uumbaji wa asili wenye uhusiano wa moja kwa moja
Kadiri tunavyo endelea kujifunza kuhusiana na mafumbo haya yaliyopo duniani maswali yanazidi kujitokeza, vitu gani vya ziada ambavyo bado hatuvijui kuhusiana na nguvu hii inayotuongoza ?
na je hii inadhihirisha vipi muunganiko wetu wa ndani kabisa kama viumbe hai ambao wote tumejikuta tupo kwenye sayari hii tukiunganishwa kwa pamoja na uhai tulio nao?