Na ndivyo inavyokuwaga. Nchi inapokosa mwelekeo, watu hupima unafuu kwa ubaya. Yaani mwenye kufanya ubaya wenye nafuu ndiyo anaonekana kama shujaa. Magufuli aliharibu sana na mengi ya mabaya tunayopitia sasa hivi yako related na utawala wake. Suluhisho ni mfumo kubadilishwa tu na preferably tuwe na waziri mkuu mtendaji na rais mwenye majukumu limited, lakini la muhimu ni uhuru wa kuchagua na kuchaguliwa.
Mkuu 'Macho...', ninakusoma sana.
Hili la "muhimu ni uhuru wa kuchagua na kuchaguliwa", ni gumu sana kuliongelea kivingine isipokuwa uzuri wake tu basi!
Nami uamini wangu umekuwa hivyo wakati wote, hadi hivi karibuni nikaanza kuingiwa na wasiwasi juu yake.
Haya mazingira yetu katika hizi nchi za kimaskini hizi, ni bahati bahati tu kupata fursa ya namna hiyo na kuitumia ipasavyo bila ya kuingiliwa kwa njia moja au nyingine; kuingiliwa toka ndani kwa ndani au hata toka nje.
Kwa miaka ya hivi karibuni hasa baada ya kuona CCM ilipo tufikisha, nimejikuta nikitamani tumpate dikteta wa kwelikweli, kama yule wa Singapore enzi zile asiyetaka mchezo kuhusu maswala ya nchi, lakini pia asiyeonea watu kwa sababu za kipumbavu kama Magufuli.
Chia hawana hii demokrasia tunayo imbishwa, lakini mambo yao yanakwenda tu, chini ya chama chao cha Kikomunisti.
Nadhani inafaa tufike mahali tuanze kupanua mawazo yetu kuhusu hizi nyimbo tunazo imbishwa kila mara na hawa wanaotaka tufuate 'values' zao, hata mahali zisipo kuwa na maana kwetu.
Sitakulaumu ukinistaajabu nikitamuka waziwazi hapa kwamba kwa sasa "Naiombea Tanzania, impate 'a Benevolent Dictator.'"
Kwa hali hii iliyopo hapa nchini kwa sasa, silijutii kabisa wazo hili.