The Official Azam FC Thread

[h=5]WAWAKILISHI wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho la Soka Afrika, (CAF), Azam FC wameanza na sare ya 1-1 dhidi ya Dragons ya hapa katika mchezo wa Kundi B kuwania Kombe la Hisani kwenye Martyrs mjini hapa.
Hadi mapumziko, wenyeji walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililotiwa kimiani na mshambuliaji wao hatari, Nkate Jason dakika ya 24.

Nkate alifunga bao hilo baada ya kuwazidi ujanja mabeki wa Azam, ambao walichanganyana na kipa wao, Mwadini Ally. Pamoja na kufungwa, Azam walicheza vizuri katika dakika 45 za kwanza na zaidi walikosa mipango tu ya kumalizia.

Hata hivyo, mashambulizi ya pembeni ya wapinzani wao yalilitia misukosuko ya kutosha lango la Azam katika ngwe hiyo.

Kipindi cha pili Azam walirudi na kikosi kile kile, lakini walibadilika kiuchezaji na iliwachukua dakika nne tu kukomboa bao, kupitia kwa Nahodha mpya, Jabir Aziz aliyeunganisha pasi ya Abdi Kassim ‘Babbi'.

Baada ya bao hilo, Azam waliendelea kushambulia lango la wapinzani wao, lakini safu ya ulinzi ya Dragons ilisimama imara kudhibiti mashmbulizi hayo.

Katika dakika ya 76, kipa Mwadini alipangua kwa uhodari mkubwa mkwaju wa penalti wa Mukinzi Mawesi, baaada ya mchezaji huyo huyo kuangushwa kwenye eneo la hatari na Ibrahim Mwaipopo.

Baada ya hapo Azam walihamia langoni mwa Dragons, ambao safu yao imara ya ulinzi iliwanusuru adhabu hii leo.
Azam ilicheza mechi ya leo bila makocha wake wote wawili, Waingereza Stewart Hall na Msaidizi wake, Kali Ongala ambao wamebaki Nairobi, Kenya pamoja na Daktari Mjerumani Paulo Gomez na wachezaji Kipre Balou na Kipre Tcheche kutokana na kukosa viza za kuingia DRC.

Azam ambao ni washindi wa pili wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame na Ligi Kuu, wamepangwa katika Kundi B pamoja na Dragons na Shark FC, ambayo watacheza nayo Desemba 17.

Ikifuzu kwenye kundi lake, Azam itaingia Nusu Fainali moja kwa moja, ambazo zitachezwa Desemba 25 na Desemba 26 itakuwa Fainali na mechi ya kusaka mshindi wa tatu.
Kundi B, lina timu za DC Motema Pembe, Diables Noirs, FC MK na Real De Kinshasa.

Kikosi cha Azam leo kilikuwa; Mwadini Ally, Himidi Mao, Waziri Salum, Luckson Kakolaki, David Mwantika, Jabir Aziz, Ibrahim Mwaipopo, Abdi Kassim, Gaudence Mwaikimba, Abdallah Seif/Humphrey Mieno na Uhuru Suleiman/Zahor Pazi. Habari kwa hisani ya Blogu ya Binzubeiry
[/h]

 
Azam FC Katika kukiimarisha kikosi chake kwa ajili ya mzunguko wa pili na mashindano ya Afrika Azam FC imefanya usajili wa wachezaji nane wapya katika kipindi hiki cha dirisha dogo Azam FC ambayo ilikuwa na wachezaji wanee wa kimataifa kufiatia George Odhiambo kuondolewa mapema kutokana na utovu wa nidhamu pia iliwapunguza wachezaji Ibrahim Shikanda na Joseph Owino na hivyo kuwa na nafasi tatu za kimataifa Azam FC imejaza nafasi hizo kwa kuwasajili Jockins Atudo, beki wa kati wa Harambee Stars na klabu ya Tusker FC, Kiungo mshambuliaji wa Harambee Stars na Sofapaka Humphrey Mieno pamoja na mshambualiaji na mchezaji bora wa mashindano ya CECAFA Challenge Cup Brian Umony. Pia Azam FC imemsajili kinda anayeshika nafasi ya pili kwa kufunga magoli ligi kuu akiwa na magoli sita nyuma ya Kipre Tchetche na Didier Kavumbangu wenye magoli nane kila mmoja Seif Rashid Abdallah toka Ruvu Shooting Stars Kama hiyo haitoshi Azam FC ambayo ilikuwa na uwakilishi mkubwa zaidi kwenye mashindano ya CECAFA Challenge Cup mwaka huu kwa kuwa na wachezaji 11, imemewarudisha walinzi Malika Ndeule na Omary Mtaki waliocheza katika vilabu vya African Lyon na Mtibwa Sugar katika mzunguko wa kwanza. Katika kuimarisha safu yake ya ulinzi pia imemsajili mlinzi wa kati wa Tanzania Prisons David Mwantika. Na kumsajili kwa mkopo winga wa Simba Uhuru Selemeani. Usajili huu umesimamiwa na mwalimu Stewart Hall mwenyewe ambaye anaamini maboresho haya yatakiongezea nguvu kikosi cha Azam FC katika mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom inayotarajiwa kuanza januari 20. Azam FC ipo jijini Kinshasa DRC ikijiandaa na mzunguko wa pili na mashindani ya kimataifa kwa kusaka uzoefu wa kucheza nje ya nchi na imeshacheza michezo miwili na timu za Dragons and FK Sharks ambapo ilitoka sare 1-1 mchezo wa kwanza na kufungwa mchezo wa pili 0-2. Azam FC inatarajia kurejea nchini December 26 ambapo itaelekea visiwani Zanzibar moja kwa moja kushiriki mashindano ya Mapinduzi Cup ambayo inayashikilia.
 
[h=3]ACADEMY WATINGA NUSU, KUCHEZA NA MTIBWA IJUMAA[/h]
Azam academy wametinga hatua ya nusu fainali ya uhai cup (koabe la vikosi B vya VPL) baada ya kuwafunga goli 1:0 JKT Ruvu katika mchezo wa robo faieali ulichezwa mapema leo.

Madogo hao wa azam sasa watawakabhli Mtibwa sugar siku ya ijumaa

 
[h=5]

Azam FC Leo imetinga nusu fainali baada ya kuifunga Real De Kinshasa 2-1. Sasa inasubiri mpinzani wake ambaye itakwaana naye ijumaa hii
[/h]
 
Uhai Cup Semi Final Results

Azam academy v Mtibwa sugar U20

azam academy wameingia final kwa mikwaju ya penati..
 
azam academy v mtibwa sugar U20 penati 4 - 3
 
Toka kongo

Azam FC 2 - 1 Sharks wafungaji ni KC10 na Mwaikimba

wakubwa wameingia fainali na academy imeingia pia fainali kwenye uhai cup
 
[h=5]Azam FC jioni hii imetwaa kombe la Congo Charity Cup baada ya kuifunga Dragons kwa penati 4-2 kufuatia sare ya 1-1. Golikipa Mwadini Ally alidaka penati mbili. Hongera Azam FC, Hongera Taifa Stars.[/h]source: Azam FC | Facebook
 
azam wanakosa kabisaa nafasi za wasi hapa..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…