The Official Azam FC Thread

The Official Azam FC Thread

Azam FC TV wanaonyesha kombe la Charity Cup 2012 (Kombe la Hisani) walilolipata hivi karibuni nchini DRC- Congo Kinshasa baada ya mwaliko maalum na kuibuka mabingwa wa Charity Cup.

Viongozi wa Azam FC, Katibu Mkuu wa Nassoro Idrissa na Meneja wa Timu 'jemedari' Saidi wakitupa taarifa za kina kuhusu ziara yao DRC- Congo na mechi zao dhini ya Dragon Fc, Real Kinshasa, Sharks Fc ( imejikamilisha kwa miundo mbinu kama Azam Fc) n.k za jijini Kinshasa. Mwaliko huo ulipatikana baada ya timu ya Vita ya DRC- Congo iliyoshiriki ktk kombe la Kagame Cup pamoja na viongozi wa shirikisho cha soka Congo DRC kuvutiwa na soka la Azam Fc, endelea kupata habari zaidi....:

video kwa hisani ya Antony John AZAM FC TV EPs 13 wa youtube
 
Last edited by a moderator:
Fainala ya Mapinduzi Cup, kurushwa Live na Star TV

Kampuni ya kutengeneza vyakula na vinywaji ya SSB ambayo pia ni wadhamini na wamiliki wa klabu ya Azam FC wameingia kandarasi na kituo cha televisheni cha Star TV kurusha matangazo ya mchezo wa kesho wa fainali ya Mapinduzi Cup Fainali hiyo ambayo itawakutanisja mapingwa wa Kenya Tusker FC na Mabingwa watetezi wa Mapinduzi Cup Azam FC itachezwa kwenye uwanja wa Amaan usiku wa kesho kuanzia saa mbili na nusu Katika mchezo wa Kesho, mbali na wachezaji waliopo Ethiopia na timu ya Taifa, pia Azam FC itawakosa wachezaji wake sita muhimu wanee wakiwa na majeruhi na wawili wakitumikia adhabu baada ya kupewa kadi nyekundu kwenye mechi ya nusu fainali. Wachezaji watakaokosekana ni Aishi Manuala (Timu ya Taifa) Waziri Salum (majeruhi) Ibrahim Mwaipopo na Jabir Aziz (Kadi Nyekundu) Abdulhalim Humud na Abdi Kassim (Majeruhi) Salum Abubakar na Hamis Mcha (Timu ya Taifa) John Bocco na Kipre Tchetche (Majeruhi) Pichani Juu Wachezaji wa kimataifa wa Azam FC wakifuatilia mpambano kati ya Miembeni na Tusker FC, Kutoka kushoto ni Brian Umony, Katikati ni Kipre Bolou na kulia ni Humphrey Mieno
 
Januari 12, 2013

Uwanja: Amani
Mjini: Zanzibar
Mashindano: Mapinduzi Cup
Timu: Tusker Fc toka Kenya, mabingwa wa ligi ya Kenya KPL na Azam FC ya jijini, Dar-es-Salaam
Makocha: Stewart Hall (kocha msaidizi Kalimangonga Ongala) wa Azam FC na Robert Matano wa Tusker Fc
Waamuzi: Ramadhani Ibada (Mwamuzi mwenye beji ya FIFA)

Mechi live baina ya Azam Fc Vs Tusker Fc kupitia link hii ya STARTV Radio Free Africa Tanzania-|- STARTV LIVE
High-lights:
Dakika ya 90 za kawaida: Azam Fc 1 - Tusker 1 wafungaji
Dakika za ziada 30:
Dakika 93 Gaudence Mwaikimba aipatia Azam bao la pili hivyo Azam 2 - Tusker 1
Dakika ya 105 dakika za ziada mapumziko Azam fc 2 - Tusker 1
Dakika ya 123 Azam 2 - Tusker 1
Dakika ya 128 Azam 2 - Tusker 1
Dakika ya 130 mpira umekwisha Azam Fc 2 - Tusker 1

Azam yafanikiwa kuwa Mabingwa wa Kombe la Mapinduzi cup kwa mara ya pili mfululizo na kuchukua Mapinduzi Cup pamoja na kitita cha Tshs. 10 millioni. Kocha wa Tusker amelaumu kiwango kidogo walichoonyesha waamuzi kati mechi ya leo. Pia aina ya rangi za taa katika kiwanja cha Amani zilipunguza ubora wa picha kupitia matangazo-live kwa njia ya televisheni STARTV na hata kwa wapiga picha za kamera.

Timu zote za Azam Fc na Tusker zilikosa kuwatumia wachezaji kadhaa kutokana na wachezaji hao kutumikia timu za taifa za nchi zao yaani Tanzania- Taifa stars na Kenya - Harambee Stars.

Januari 12, 2013

Uwanja: Amani
Mjini: Zanzibar
Mashindano: Mapinduzi Cup
Timu: Tusker Fc toka Kenya, mabingwa wa ligi ya Kenya KPL na Azam FC ya jijini, Dar-es-Salaam
Makocha: Stewart Hall (kocha msaidizi Kalimangonga Ongala) wa Azam FC na Robert Matano wa Tusker Fc
Waamuzi: Ramadhani Ibada (Mwamuzi mwenye beji ya FIFA)

Mechi live baina ya Azam Fc Vs Tusker Fc kupitia link hii ya STARTV Radio Free Africa Tanzania-|- STARTV LIVE
High-lights:
Dakika ya 90 za kawaida: Azam Fc 1 - Tusker 1 wafungaji
Dakika za ziada 30:
Dakika 93 Gaudence Mwaikimba aipatia Azam bao la pili hivyo Azam 2 - Tusker 1
Dakika ya 105 dakika za ziada mapumziko Azam fc 2 - Tusker 1
Dakika ya 123 Azam 2 - Tusker 1
Dakika ya 128 Azam 2 - Tusker 1
Dakika ya 130 mpira umekwisha Azam Fc 2 - Tusker 1

Azam yafanikiwa kuwa Mabingwa wa Kombe la Mapinduzi cup kwa mara ya pili mfululizo. Kocha wa Tusker amelaumu kiwango kidogo walichoonyesha waamuzi kati mechi ya leo.

Timu zote za Azam Fc na Tusker zilikosa kuwatumia wachezaji kadhaa kutokana na wachezaji hao kutumikia timu za taifa za nchi zao yaani Tanzania- Taifa stars na Kenya - Harambee Stars.

safi sana wameshaiona hiyo..
 
Aka Mapenati fc

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
hatariiiiiiiiii
553136_510373072336387_1856151725_n.jpg
 
Official- Zahoro Pazi kaelekea leo South Africa kwenye majaribio na B. Celtic ya south kwa siku 10
 
Azam FC imeanza safari ya kuelekea Nairobi nchini Kenya, ikiwa huko itacheza mechi tatu za kirafiki, Mungu ibariki Safari yetu!
 
Friendlies Game
AFC Leopards 2 - 1 Azam FC
 
Back
Top Bottom