Stewart kuisafiria Al Nasir Juba kabla ya kukutana
Siku chache kabla ya kucheza mechi za Kombe la Shirikisho Afrika, kocha wa Azam FC yupo katika maandalizi ya kuelekea nchini Sudan Kusini kuangalia mechi chache za wapinzani wao timu ya Al Nasri Juba.
"Nimepanga kwenda Sudan hivi karibuni, kucheza bila kumjua mpinzani wako inakuwa ngumu, nitatumia muda huo kuwajua wapinzani wetu ili kupata picha ya mchezo utakavyokuwa pamoja na kuiandaa timu yangu" amesema Stewart.
[h=5]Azam FC
[/h][h=5]Beki wa Azam FC, Samih Haji Nuhu amepata majeraha kwenye uti wa mgongo wakati wa mchezo wa kirafiki kati ya Azam FC na Simba siku ya Jumatatu, atakaa nje ya uwanja kwa zaidi ya mwezi mmoja na nusu...
Get Well Soon brother, tunakuombea!
[h=5]Wachezaji wote wa Azam FC wapo na afya njema tayari kuikabili Al Nassir ya Sudani ya kusini isipokuwa Haji Nuhu na Waziri Salum pekee walio na majeruhi...[/h]
Azam vs Alnasir Uwanja wa Taifa, Jumamosi Tarehe 16 kuanzia saa kumi jioni. kabla ya mechi kuanzia saa sita mchana kutakuwa na burudani kibao toka kwa wasanii wa Bongo Fleva wakiongozwa na wakali wa TMK Sir Juma Nature na Inspector Haroun Babu.
Viingilio Green & Blue 2,000/-, Orange 5,000/-, VIP C & B 10,000/-, na VIP A 20,000/-
Imesimamiwa na Prime Time Promotion na kudhaminiwa na Azam Cola
[h=5]Azam FC
[/h][h=5]"Tumejipanga vizuri zaidi, tunategemea kupata matokeo mazuri kama tulivyopanga, Mungu atatusaidia" anasema Haji Nuhu (kushoto).
"Tumepata uzoefu wa kutosha kwa kuwa tumecheza mechi za kirafiki Congo, Zanzibar, Kenya na mechi za ligi, tunaomba kila mchezaji awe salama ili tufanikishe lengo letu ambalo ni ushindi" anasema Gaudence Mwaikimba (kulia).