The Official Azam FC Thread

The Official Azam FC Thread

March 22, 2013
Dar-es-Salaam, Tanzania

JK aziponda Simba, Yanga

RAIS Jakaya Kikwete amezipiga ‘kijembe’ klabu kongwe hapa nchini, Simba na Yanga, kutokuwa na maendeleo kisoka na kuiacha Azam FC, ikiwapiga kumbo kila idara huku wao wakiendekeza ushirikina mbele na migogoro.

Kikwete aliyasema hayo jana, wakati akiweka jiwe la msingi la klabu ya Azam iliyoko Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Rais aliipongeza Azam kwa hatua ambayo imefikia, licha ya kuwa na uchanga katika soka na kuzipita klabu za Simba na Yanga.

Alisema endapo Azam inataka kupiga hatua na kuifikisha nchi mbali kwa kulitangaza jina la Tanzania, ifanye mambo yake bila kuzifuata timu kongwe na kudai kuwa itafika mbali kitaifa na kimataifa pia.

“Naamini mna uwezo wa kufika mbali katika ulimwengu wa soka, ila msiwe karibu na hizi timu, mtajikuta mnaishia hapahapa; wao mechi mechi moja wanatolewa,” alisema Kikwete na kuwafanya watu walioshuhudia hafla hiyo kuvunjika mbavu.

Aidha Kikwete alisema kutokana na mafanikio ambayo Azam wameyapata hadi sasa, ikiwemo uwanja na mambo mengine, imeonekana kama wao ndio vigogo na kusababisha kuogopwa na jamaa ambao wanajifanya wakubwa.

“Mpaka sasa haionekani nani mkubwa, maana kuwa na wanachama wengi sio ishu na nyie nina imani mnaweza kulileta hili Kombe la Shirikisho nyumbani, najua timu kubwa zikiwa na mechi na nyie zinakuwa na wasiwasi, hivyo basi mpaka sasa nyie ndio mtasaidia soka la Tanzania kukua,” alisema Kikwete.

Alikwenda mbali zaidi na kuwataka Azam, kuacha kufuata vivuli vya hizo timu na kujisimamia wenyewe, kwa kuwa timu mbili kongwe zina wanachama wanaopiga kura kwa kuhongwa, sambamba na kutumia muda mwingi kulumbana, wakati hawana kitu wanachoingiza katika timu.

Alisema timu kubwa zikiambiwa kutumia Uwanja wa Chamazi, zinaanza kuleta maneno ya ajabu na kuongeza kuwa ushirikina haufai katika soka, cha muhimu ni kucheza mpira na sio kazi ya kuandaa kamati za ufundi na kushindwa kutazama benchi la ufundi ili kujenga timu.

“Ingekuwa mpira ni ushirikina, basi Afrika tungekuwa mabingwa kila mwaka, kama timu inaona uchawi dili, basi ikusanye wachawi wote dunia nzima ikae nao klabuni kwao tuone!” aliongeza Kikwete.

Aliwataka Azam endapo watakuwa na shida yoyote, wasisite kumjulisha na kudai kuwa ombi lao la kupunguziwa VAT katika bidhaa zao za kisoka, atawasiliana na wahusika ili aweze kulipatia ufumbuzi.

Naye Mkurugenzi wa Azam, Yusuph Bakhressa, alishukuru sana kupata nafasi ya Rais kuzindua mradi wao maalumu, ambao lengo lake ni kukuza na kuendeleza mpira wa miguu nchini.

Alisema hadi sasa wametumia sh bilioni 3 katika mradi huo.

Katika hafla hiyo, Rais aliambatana na mkewe Mama Salma Kikwete, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara, Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Mecky Saidi Sadick, na viongozi mbalimbali.

source: JK aziponda Simba, Yanga

DSC09364.JPG

Rais Jakaya Kikwete akizindua jiwe la msingi la uwanja wa Azam Complex wa Klabu ya Azam FC huko Chamazi, jijini Dar-es-Salaam (Picha kwa hisani ya Habari Mseto blog)
 
DSC09448.jpg


DSC09439.JPG

Picha kwa hisani ya Habari Mseto blog na kwa picha zaidi gonga linki hii: Balilemajuto .
 
Hapo mr przooo kaongea kweli, kama uchawi unge kuwa inshu basi lazima sumbawanga wangekua na timu ligi kuu ya bara. Kwakweli hata mimi nazichukia sana hzi timu kongwe (Simba na Yanga) kwakuwa hazipo kiushindani wa soka bali wenyewe wamejipanga kiushindani wa majungu tu. Azam ndio mkombozi wa soka letu hapa bongo
 
3e7eKikwete-greets-Azam-FC-players.jpg

President Jakaya Mrisho Kikwete greets Azam FC players when officiating at the opening of the club's newly constructed Stadium dubbed ‘Azam Complex' located at Chamazi in Dar es Salaam on 22nd March 2013. On his right is Azam vice-chairman Said Mohamed. (Photo by Yusuf Badi) source: Azam get presidential accolades | 24 Tanzania News
 
699218353.jpg

Pichani Aden Rage, Mwenyekiti wa klabu ya Simba

March 22, 2013

Aden Rage aipongeza Azam FC
Mwenyekiti wa klabu ya Simba SC Aden Rage ameipongeza klabu ya Azam kwa kufanya ufunguzi wa kujenga kiwanja kipya cha kisasa cha mpira wa miguu kilicho funguliwa Leo na rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete.



Picha ya tukio: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho kikwete akitakata utepe kuzindua ujenzi wa kiwanja cha kisasa cha soka cha azam complex chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es salaam

Mwenyekiti wa Simba SC ameongeza kuwa litakuwa somo kwa klabu ya Simba na Yanga kwani japokuwa na ukongwe wa vilabu hivyo hata majengo/viwanja yao yaliyopo mitaa ya Jangwani/uwanja Kaunda (Yanga) na Msimbazi (Simba) katika hali mbaya.

Mwenyekiti wa klabu kongwe ya Simba SC , Aden Rage ambaye anarejea kesho kutoka Nchini India alipokwenda kufanyiwa matibabu amesema pindi atakapofika atazungumza na waandishi wa habari kuhusu mustakbari wa klabu hiyo yenye makao yake makuu msimbazi jijini Dar es salaam.


Source: K-SPORT.COM
 
Muonekano wa Azam Sports Complex miezi michache iliyopita katika mfumo wa 3D (picha 'engo zote za complex'), tembelea-kielezo (virtually) kupitia clip hii uone mwenye mandhari halisi:


source: antony john wa youtube
 
Last edited by a moderator:
Azam yafanya bonge la usajili cheki hapa sasa...

602076_546369182070109_1837194184_n.jpg

Huyu tayari ni mchezaji halali wa Yanga, wengine ni Paul Kagame (Rwanda), Yoweri Museveni (Uganda), Joseph Kabila (DRC), Keneth Kaunda (Zambia) na Nelson Mandela (South Africa). Azam walie tu!
 
March 25, 2013

PRISONS WAJIPANGA KUISIMAMISHA AZAM FC NYUMBANI KWAO CHAMAZI

Na Baraka Mpenja
Maafande wa jeshi la magereza, Tanzania Prisons kutoka jijini Mbeya wamejigamba kuwatandika wana lamba lamba, klabu ya Azam fc katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara utaopigwa kesho kutwa (Machi 27) uwanja wa Azam Complex, Mbande nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza leo hii, Katibu mkuu wa Prisons Sadick Jumbe amesema maandalizi yanakwenda vizuri na kocha mkuu Jumanne Chale anamalizia programu yake ya mazoezi kabla ya kuwavaa Azam nyumbani kwao.

Jumbe alisema kikosi chao kipo safi kwa asilimia zote kwani mpaka sasa hakuna mchezaji ambaye yupo hatarini kuukosa mchezo huo.

"Tunaenda kupambana na Azam fc ambao wametoka kushinda ugenini kombe la shirikisho dhidi ya Barrack Young Controller II ya Liberia, hii imewapa morali kubwa, lakini tutapambana kufa na kupona ili kupata ushindi wa ugenini". Jumbe alisema.

Katibu huyo wa Prisons aliongeza kuwa, kikosi chake kimekaa maeneo ya Ukongo kwa zaidi ya wiki moja kikitokea mjini Arusha ambako kilifungwa 1-0 na wapiga kwata wenzao JKT Oljoro, mchezo wa ligi kuu.

Jumbe alisema wakiwa Ukonga wamecheza mechi za kujipima uwezo na African Lyon na kuwafunga 1-0, wakacheza na timu ya wizara ya ndani na kutoka nayo sare ya 2-2 na wakashuka dimbani dhidi Ukonga united.

"Tunakumbuka mchezo wa mzunguko wa kwanza tukiwa nyumbani Sokonne, tulilazimisha suluhu na Azam Fc, lakini safari hii tunahitaji kuwadhihirishia watanzania kuwa uwezo wa kuwafunga tunao". Jumbe alitamba.

Akizungumzia suala la mchezaji wao wa zamani, David Mwantika, anayekipiga Azam kwa sasa kuukosa mchezo huo kutokana na kuoneshwa kadi nyekundu mchezo uliopita dhidi ya Polisi Moro uliomalizika kwa sare ya 1-1, alisema ni nafasi nzuri kwao kwani nyota huyo anawafahamu sana washambuliaji wao.

Wakati huo huo Azam fc imeingia kambini rasmi leo hii baada ya nyota wake kurejea wakitokea kuitumikia timu ya taifa hapo jana dhidi ya simba ya Milima ya Atlas, timu ya taifa ya Morroco na kushinda 3-1.

Akizungumza leo Afisa habari wa Azam fc, Jafar Idd Maganga amesema wanamshukuru mungu kwani mpaka leo hii hawana mchezaji majeruhi baada ya mlinzi wao Hajji Nuhu kupona.

Maganga alisema wanatarajia mchezo huo kuwa wa vuta ni kuvute , lakini wanajiandaa vizuri kuhakikisha wanashinda na kujiweka vizuri katika mbio za kuwania ubingwa wa ligi kuu msimu wa 2012/2013
Source: Shaffih Dauda in Sports.: PRISONS WAJIPANGA KUISIMAMISHA AZAM FC NYUMBANI KWAO CHAMAZI

Dua la kuku halimpati mwewe
 
Timu ya Azam FC kesho itashuka kwenye uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi kukwaana na Tanzania Prisons katika mfululizo wa ligi kuu ya Vodacom Azam FC yenye pointi 37 itahitaji kushinda katika mchezo wa kesho ili kujiimarisha katika nafasi ya pili na kuweza kuiwakilisha tena nchi kwenye michezo ya Kimataifa ambao hadi sasa ina ushindi wa 100% kwenye mechi za kimataifa baada ya kucheza mechi tatu na kushinda zote Tanzania Prisons ambayo inapambana kuhakikisha inasalia kwenye ligi kuu itakuja uwanjani kwa nia ya kushinda ikiongozwa na kocha wake mtundu mwenye mbinu nyingi Jumanne Charles Wachezaji wate wa Azam FC akiwemo Brian Umony wapo katika hali nzuri tayari kwa mchezo huo isipokuwa David Mwantika anayetumikia adhabu ya kukosa mechi tatu kutokana na kupewa kadi nyekundu mchezo uliopita na Haji Nuhu aliye majeruhi Timu ya Azam FC iliingia kambini jana jumatatu jioni kujiandaa na mchezo huo kwa habari zaidi The Official Website of Azam Football Club | Tucheze pamoja kwa furaha

sosi: facebook azam fc
 
March 25, 2013

PRISONS WAJIPANGA KUISIMAMISHA AZAM FC NYUMBANI KWAO CHAMAZI

Na Baraka Mpenja
Maafande wa jeshi la magereza, Tanzania Prisons kutoka jijini Mbeya wamejigamba kuwatandika wana lamba lamba, klabu ya Azam fc katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara utaopigwa kesho kutwa (Machi 27) uwanja wa Azam Complex, Mbande nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza leo hii, Katibu mkuu wa Prisons Sadick Jumbe amesema maandalizi yanakwenda vizuri na kocha mkuu Jumanne Chale anamalizia programu yake ya mazoezi kabla ya kuwavaa Azam nyumbani kwao.

Jumbe alisema kikosi chao kipo safi kwa asilimia zote kwani mpaka sasa hakuna mchezaji ambaye yupo hatarini kuukosa mchezo huo.

“Tunaenda kupambana na Azam fc ambao wametoka kushinda ugenini kombe la shirikisho dhidi ya Barrack Young Controller II ya Liberia, hii imewapa morali kubwa, lakini tutapambana kufa na kupona ili kupata ushindi wa ugenini”. Jumbe alisema.

Katibu huyo wa Prisons aliongeza kuwa, kikosi chake kimekaa maeneo ya Ukongo kwa zaidi ya wiki moja kikitokea mjini Arusha ambako kilifungwa 1-0 na wapiga kwata wenzao JKT Oljoro, mchezo wa ligi kuu.

Jumbe alisema wakiwa Ukonga wamecheza mechi za kujipima uwezo na African Lyon na kuwafunga 1-0, wakacheza na timu ya wizara ya ndani na kutoka nayo sare ya 2-2 na wakashuka dimbani dhidi Ukonga united.

“Tunakumbuka mchezo wa mzunguko wa kwanza tukiwa nyumbani Sokonne, tulilazimisha suluhu na Azam Fc, lakini safari hii tunahitaji kuwadhihirishia watanzania kuwa uwezo wa kuwafunga tunao”. Jumbe alitamba.

Akizungumzia suala la mchezaji wao wa zamani, David Mwantika, anayekipiga Azam kwa sasa kuukosa mchezo huo kutokana na kuoneshwa kadi nyekundu mchezo uliopita dhidi ya Polisi Moro uliomalizika kwa sare ya 1-1, alisema ni nafasi nzuri kwao kwani nyota huyo anawafahamu sana washambuliaji wao.

Wakati huo huo Azam fc imeingia kambini rasmi leo hii baada ya nyota wake kurejea wakitokea kuitumikia timu ya taifa hapo jana dhidi ya simba ya Milima ya Atlas, timu ya taifa ya Morroco na kushinda 3-1.

Akizungumza leo Afisa habari wa Azam fc, Jafar Idd Maganga amesema wanamshukuru mungu kwani mpaka leo hii hawana mchezaji majeruhi baada ya mlinzi wao Hajji Nuhu kupona.

Maganga alisema wanatarajia mchezo huo kuwa wa vuta ni kuvute , lakini wanajiandaa vizuri kuhakikisha wanashinda na kujiweka vizuri katika mbio za kuwania ubingwa wa ligi kuu msimu wa 2012/2013
Source: Shaffih Dauda in Sports.: PRISONS WAJIPANGA KUISIMAMISHA AZAM FC NYUMBANI KWAO CHAMAZI

bora umeliona hilo..
 
Wednesday March 27, 2013
Dar-es-Salaam, Tanzania

Results Azam 3 Tanzania Prisons 0

Azam fc leo waliwakaribisha Prinsons katika uwanja wake wa azam complexs katika muendelezo wa michezo ya ligi kuu ya vodacom uliomalizika kwa azam fc kuibuka na ushindi wa goli 3-0.
Prinsons waliuwanza mchezo wa leo vyema kwa kuwazuia azam fc kutopata goli la mapema lakini walitepeta katika dakika ya 19 kufuatia kazi nzuri ya kiungo Khamis Mcha aliyemtengea Kipre Tchetche na bila kufanya agizi Tchetche aliiandikia goli la kwanza azam fc.
Kuingia kwa goli hilo kulipelekea Prisons kurejea nyuma na kupeleka mashambulizi ya kushtukiza ambayo yalikuwa yanaishia kwa kipa Mwadini Ally na kupelekea kwenda mapumziko wakiwa nyuma kwa goli 1-0.
Azam fc walirejea kipindi cha pili na kucheza kwa tahadhari kubwa uku wakiendelea kutawala mchezo na mnamo dakika 75 John Raphael Bocco aliiandika azam fc goli la pili kwa shuti kali akitokea pembeni.
Azam fc walimpumzisha Khamisi Mcha, Humphrey Mieno na Salum Aboubakary na nafasi zao kujazwa na Abdallah Seif, Abdi Kassim na Ibrahim Mwaipopo, mabadiliko yaliyoendeleza mchezo kuwa chini ya azam fc.
Katika dakika ya 85 alikuwa Kipre Tchetche aliyeizawadia azam fc goli la la 3 na kupelekea mchezo kumalizika kwa azam kushinda 3-0.Azam fc leo: MWADINI ALLY, HIMID MAO, WAZIRI SALUM, JOACKINS ATUDO, LACKSON KAKOLAKI, MICHAEL BOLOU, KIPRE TCHETCHE, SALUM ABOUBAKARY /IBRAHIM MWAIPOPO, JOHN BOCCO, HUMPHREY MIENO/ ABDI KASIM NA KHAMISI MCHA/ ABDALLAH SEIF

Source: Azam Fans Club
 
kudos lads kwa ushindi mnono huku star tv wakionesha mtanange huo..
 
[TABLE="width: 650, align: center"]
[TR]
[TD="class: headline, bgcolor: #FFFFFF"]ATUDO: Jembe jipya ndani ya Azam[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: headline, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: storyheader, bgcolor: #FFFFFF, align: left"] [TABLE="width: 51%, align: left"]
[TR]
[TD="align: center"]
15715.jpg
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: mwanacss, bgcolor: #B47C01, align: left"][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
DORIS MALIYAGA
LIGI Kuu Bara ina mabeki wengi, lakini Mkenya wa Azam FC, Jockins Otieno Atudo anatofautiana nao kwa mambo kadhaa.

Amejengeka kimazoezi na ana mwili mkubwa ambao unabebwa na kipaji kuhimili nafasi yake ya beki wa kati. Ni beki mwenye uwezo wa kipekee wa kulinda timu yake na mara kadhaa kupachika mabao.

Kimuonekano ni mweusi, mrefu na ana umbo lililojengeka na mkakamavu. Ni miongoni mwa mabeki waliosainiwa na kocha Mwingereza Hall Stewart kwa ajili ya michuano ya kimataifa.

Alitua Azam FC akitokea Tusker ya Kenya na amekuwa mstari wa mbele kuimarisha ukuta wa Azam akishirikiana kwa ukaribu na beki mwenzie David Mwantika.

Katika staili ya uchezaji wake anatumia zaidi akili na nguvu hali inayowafanya mastraika wasumbufu washindwe kumpenya.
Atudo ni mzuri katika kufunga mabao ya kichwa.

Panapotokea mipira ya adhabu yoyote kama kona na krosi lazima uwe makini naye.

Tangu asajiliwe kwenye dirisha dogo kwa ajili ya mzunguko wa pili tayari amewafungia mabao sita katika michuano mbalimbali.

Kati ya mabao hayo moja amefunga kwenye ligi mechi dhidi ya Mtibwa Sugar, matatu katika michuano ya Kombe la Mapinduzi wakawa mabingwa na mawili walipokuwa kwenye mashindano ya Kombe la Hisani huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ambako walitwaa ubingwa.

"Sababu ya kufanya vizuri ni kutambua majukumu yangu katika kazi, kujituma na ushirikiano wangu na wenzangu," anasema Atudo anayevutiwa na soka la Thomas Vermaelen beki wa kati wa Arsenal na Ubelgiji.

"Napenda kujifunza kila siku na kufuata maelekezo ya yoyote nitakayopewa na kocha. Uwepo wangu Azam nimevutiwa na mipango ya timu,"anasema Atudo ambaye pia ni shabiki wa Arsenal.

"Baada ya kucheza nyumbani kwa kipindi kirefu, nimeona nitoke kwa ajili ya kutafuta njia nyingine ya mafanikio, unajua unapocheza nyumbani tu hupati changamoto kama unapotoka na kuja sehemu kama Tanzania."

"Tangu nimefika maazimio yetu ni kutwaa ubingwa wa ligi jambo ambalo tutalikamilisha lakini pia tunataka kuweka historia katika michuano ya kimataifa kutokana na kiwango cha juu tutakavyokionyesha,"alisisitiza.

Anavyoizungumzia Azam
"Azam ni timu nzuri na ina ushindani wa hali ya juu. Ushindani uliopo ni baina ya wachezaji wenyewe kwa wenyewe kila mmoja akitafuta namba ya kucheza,"anasema Atudo.

"Sina uzoefu na timu hii lakini nimeona wapo wachezaji wazuri wenye bidii na heshima wanaoweza kuipeleka Azam mahali popote. Nimegundua hili kwa mara ya kwanza nilipofika kwani pamoja na ugeni wangu sikuhisi tofauti na niliishi kama mwenyeji,"anasisitiza Atudo.

Kuhusu michuano ya kimatifa na mechi za ligi, Atudo anasema klabu yao itafanya vizuri kwa sababu maandalizi ni mazuri.

"Azam ni wageni katika michuano ya kimataifa lakini mategemeo yangu tutafanya maajabu msimu huu kwa sababu maandalizi tunayofanya ni mazuri.

"Na si michuano hiyo tu hata kwenye ligi mambo yatakuwa mazuri,"anasisitiza mchezaji huyo, ambaye timu yake sasa ipo raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho.

Tofauti ya Kenya na Tanzania
"Mpira wa Kenya na Tanzania ni tofauti hasa katika uchezaji. Mpira wa Kenya ni nguvu na vurugu hupati nafasi ya kutamba kirahisi, lakini Tanzania si sana,"anasema Atudo.
"Mpira wa Tanzania mwepesi na una kasi hata hivyo nimeshakuwa mzoefu sasa."


Nje ya soka
"Natumia muda wangu mwingi kukaa na familia yangu nyumbani hata hapa Tanzania huwa natulia tu nyumbani, sipendi kuzunguka bila sababu."
Atudo anasema kitu kinachomvutia zaidi Tanzania ni ukarimu wa wenyeji: "Watanzania ni wakarimu na watu wa kusaidiana katika maisha yote tofauti na sehemu nyingine."

Historia
Kipaji chake cha soka tangu akiwa mdogo na alianza kufanya vizuri shule ya msingi alikuwa anasoma Sonny. Umaarufu wake uliongezeka zaidi akiwa Sekondari ya Pe-hill alikosoma hadi kidato cha nne.

Pamoja na kufanya kwake vizuri katika soka lakini Atudo aliona elimu ndiyo jambo muhimu kwake akamua kuendelea na masomo na kusoma kidato cha tano na sita katika sekondari ya Kisumu.

Mara baada ya kumaliza, hapo ndipo Atudo akajiingiza rasmi kucheza soka la ushindani na alisajiliwa na klabu ya Sonny Sugar 2005 kucheza Ligi Kuu.
Akiwa na Sonny aliichezea miaka mitatu akahamia Tusker FC klabu aliyoichezea kwa mafanikio makubwa na muda mrefu kutoka 2008-2012 aliposajiliwa na Azam.

Ujio wake Azam ni baada ya kuonwa na kocha, Stewart Hall akicheza ligi ya Kenya. Hall alikuwa Kenya mara baada ya kuachana na Azam kwa muda akenda kuifundisha Sofapaka ya nchini humo.

Juu ya maisha yake kifamilia, Atudo anasema wako watano na yeye ndiyo wa kwanza. Ndugu zake wengine ni Collins, Midred, Felix, na Zaina ambao wanafanya shughuli zao wenyewe.

Atudo ni baba wa familia yenye mke (hakutaja jina lake) na mtoto mmoja wa kiume anayeitwa, Neville (1.4).


JOCKINS OTIENO ATUDO
Kuzaliwa: Agosti 8, 1988
Mahali: Migori, Kenya
Klabu: Sonny Sugar 2005-2008,
Tusker 2008-2012, Azam FC 2012-
Taifa: Kenya[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

sosi:ATUDO: Jembe jipya ndani ya Azam
 
[TABLE="width: 650, align: center"]
[TR]
[TD="class: headline, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: headline, bgcolor: #FFFFFF"]Kipre Tchetche amuweka benchi Kavumbagu[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: headline, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: storyheader, bgcolor: #FFFFFF, align: left"] [TABLE="width: 51%, align: left"]
[TR]
[TD="align: center"]
15734.JPG
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: mwanacss, bgcolor: #B47C01, align: left"][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
DORIS MALIYAGA
STRIKER wa Azam FC, Kipre Tchetche amemuambia mpinzani wake kwenye msimamo wa mabao kwenye ligi, Didier Kavumbagu wa Yanga akae benchi aone mabao yanavyopigwa.

Amesisitiza kwamba anataka kuvunja rekodi ya Mrisho Ngassa na John Bocco 'Adebayor' kwa kumaliza msimu wa Ligi Kuu Bara akiwa amefunga mabao 20.

Tchetche raia wa Ivory Coast ndiye anaongoza safu hiyo ya mabao baada ya kufikisha 12 akifuatiwa na Mrundi wa Yanga, Kavumbagu mwenye mabao tisa. "Malengo yangu msimu huu ni kumaliza ligi nikiwa nimefunga mabao 20 hapo roho yangu itatulia. Sikuwa na wakati mzuri katika mechi zilizopita kutokana na kusumbuliwa na majeruhi ndiyo maana kasi yangu ya kupiga mabao ikapungua,"alisema Tchetche.

"Hata hivyo naamini nitafanikiwa kwa sababu mechi tulizobakiwa nazo sita bado ni nyingi kama nitatilia mkazo kwa bidii na Mungu anilinde na majeruhi naamini nitakamilisha idadi hiyo bila tatizo."

Tofauti ya mabao matatu na wenzake inamweka mahali pazuri, Tchetche na kama atafikisha mabao 20 atakuwa ameingia rekodi mpya iliyowekwa zaidi ya miaka zaidi ya 10 kupita.

Mohamed Hussein 'Mmachinga' ndiye anashikilia rekodi ya kufunga mabao mengi katika msimu wa ligi akifikisha 25, wafungaji bora wa misimu ya karibuni wamekuwa wakiishia mabao chini ya 20. Bocco alikuwa kinara msimu uliopita baada ya kufikisha mabao 18.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

sosi:Kipre Tchetche amuweka benchi Kavumbagu
 
[h=5]Azam FC leo wanajitupa kiwanjani tena kusaka alama ntingine tatu muhimu. Leo tuko Mlandizi kupambana na Ruvu Shooting ya Pwani. Mechi itapigwa kwenye uwanha wa Mabatini kama kawaida. Wachezaji wote wako timamu ukiondoa mlinda mlango namba moja Mwadini Ali anaesumbuliwa na mafua, Abdulhalim Humudi alieko majaribio Jomo Cosmos na David Mwantika ambaye anatumikia kadi nyekundu. Faraja ni kurejea kikosini kwa Brian Umony ambaye ameyashinda majeruhi yaliyokuwa yanamsumbua.
[/h]
 
Back
Top Bottom