The Official Azam FC Thread

azam tumetoka kizembe japokuwa walikuwa wanabebwa..
 
Refa hawezi kulaumiwa katoa penati kote kote, FAR wamepata bao lao Azam wamekosa.
Kiukweli binafsi sioni sehemu ya kumlaumu refa, amejitahidi kuwa fair, kama kuna makosa kafanya basi wataalamu zaidi ndo watagundua, mimi kwa maoni yangu naona kachezesha vizuri, kadi zote ni halali na hata penati alizotoa ni halali pia.

Azam pamoja na kufungwa mmejitahidi sana, hongereni, jipangeni kwa ajili ya mwakani.
 

hii game kaka wachezaji wa azam wamebug wenyewe tu maana walikuwa hawaforce hata kidogo pili wamekosea kuingia na mind ya waarab wanabebwa ndio iliyo tucost zaidi..
 
azam tumetoka kizembe japokuwa walikuwa wanabebwa..
Lakini si haba, hapo mlipofika kocha akikaa na wachezaji wakaongeza nidham na kujituma mwakani mnaweza kufika mbali, kwa ujumla timu yenu ni nzuri.
 
Hongera Azam, hongera timu changa yenye kuleta matumaini kwa watanzania...mjitahidi next time mtavuka. Enzi za Simba na Yanga zinafikia mwisho kama hamtajiingiza kwenye siasa mkacheza soka tu
 
Kuanzia sasa tutasikia mengi mfano: Azam yafa kiume, Azam yawatoa jasho waarab lakini yatolewa, Azam ilifia Dar yacheza soka la kusisimua Morocco n.k.

[h=3]AZAM FC YAFA KIUME RABAT, BOCCO AKOSA PENALTI MUHIMU, MABEKI WAWILI WATOLEWA NJE KWA KADI NYEKUNDU[/h]
[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]Kipa wa AS FAr Rabat, Ali Grouni akimfariji mshambuliaji wa Azam FC, John Bocco baada ya kukosa penalti ambayo ineipa Azam tiketi ya kufuzu Kombe la Shiriksiho jioni hii kwenye Uwanja wa Prince Moulay Abdellah, Rabat. Azam imefungwa 2-1. [/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Na Mahmoud Zubeiry, Rabat
SOKA ni mchezo wa bahati wakati mwingine. Naam sadakta, usemi huo umedhihirika leo kwenye Uwanja wa Prince Moulay Abdellah baada ya Azam kulala 2-1 mbele ya wenyeji AS FAR Rabat na kutolewa katika Raundi ya Tatu ya Kombe la Shirikisho Afrika, licha ya kupata nafasi nzuri ya kusonga mbele dakika ya 81.
"Tumekosa penalti dakika ya 81, siwezi kumlaumu refa ikiwa tumekosa penalti zimebaki dakika tisa," alisema kocha wa Azam FC, Muingereza Stewart Hall baada ya mchezo akizungumza na BIN ZUBEIRY.
Azam ilihitaji sare yoyote ya mabao ifuzu na ilikaribia kuipata dakika ya 81 ilipopata penalti ikiwa nyuma kwa mabao 2-1, lakini fundi wa upigaji wa michomo hiyo, John Raphael Bocco alikwenda kugongesha mwamba mpira huo.
Dakika ya 88, kona nzuri iliyochongwa na Khamis Mcha ‘Vialli' iliunganishwa vizuri kwa kichwa na Bocco, lakini beki mmoja wa Rabat akaiwahi kwenye chaki na kuiondosha kwenye eneo la hatari.
Katika mechi hiyo iliyochezeshwa na refa Abib Charef Medh aliyesaidiwa na Mahmoud Bitam na Mohamed Mekous wote kutoka Algeria, hadi mapumziko, Rabat walikuwa mbele kwa mabao 2-1.
Azam ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika ya sita, mfungaji John Raphael Bocco kwa mpira wa adhabu, baada ya beki mmoja wa Rabat kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.
Boko alipiga shuti zuri ambalo liliupita ukuta wa Rabat na kumpoteza maboya kipa wao, Ali Grouni na kutinga nyavuni.
Mashabiki wa Rabat walianzisha fujo baada ya bao hilo na kujikuta wakipambana na Polisi. Idadi ya Polisi iliongezwa uwanjani ili kuwadhibiti mashabiki hao ambao walikuwa wakivunja viti na kuwatupia Polisi.
Iliwachukua dakika sita tu Rabat kusawazisha kupitia kwa Abdelrahim Achchakir kwa mkwaju wa penalti, baada ya beki David Mwantika kumchezea rafu mchezaji wa Rabat.
Refa Abib Charef Medh alimtoa nje kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja Achchakir kwa kumchezea rafu Brian Umony dakika ya 35.
Hata hivyo, Azam walishindwa kutumia mwanya wa Rabat kucheza pungufu na kujikuta wakifungwa wao bao la pili.
Mustafa Allaoui alipiga vizuri shuti la mpira wa adhabu umbali wa mita 25 na kumtungua Mwadini Ally dakika ya 42.
Baada ya bao hilo, wenyeji waliendelea kulisakama kama nyuki lango la Azam licha ya kucheza pungufu.
Viungo wa Azam walionekana kabisa kuzidiwa na viungo wa Rabat ambao waliifanya timu hiyo itawale mchezo. Azam haikufanya shambulizi la kushitua tangu wafungwe bao la pili.
Kipindi cha pili, mchezo ulizidi kuwa wa kasi na mashambulizi ya panede zote mbili, lakini kilianza vibaya kwa Azam, baada ya beki wake David Mwantika kutolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 56 kwa kumchezea rafu mchezaji wa Rabat.
Mwantika leo hakuwa katika ubora wake- kwani hata faulo alizocheza na kusababisha penalti ilikuwa ‘si ya lazima' na hata kadi nyekundu pia angeweza kuiepuka kama asingemsukuma hadi kwenye lami mchezaji wa Rabat.
Kutokana na Azam kubaki pungufu, Rabat walizidisha mashambulizi langoni mwa wageni na Kaddioui Yuossef alikuwa mwiba kwa timu ya Stewart.
Waziri Salum alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 75 baada ya kumchezea rafu Kaddioiu Yuossef.
Ajabu baada ya kadi hiyo, Azam walizinduka na kuanza kulishambulia kama nyuki lango la Rabat na ndipo dakika ya 81 beki mmoja wa Rabat alipounawa mpira kwenye eneo la hatari na refa akamuru penalti ambayo Bocco alikosa.
Wakati mashabiki wachache wa Tanzania waliokuwa uwanjani wakishangilia kwa kuamini Bocco anafunga, aligongesha mwamba mpira na kuinyima nafasi muhimu Azam.
Baada ya mchezo huo, kocha Stewart alisema kwamba wamefungwa kwa sababu ya makosa ya safu ya ulinzi. "Kweli refa alikuwa wa upande mmoja, bao la pili (la Rabat) halikuwa sahihi, aliotea. Kadi ya Waziri haikuwa sahihi, walikuwa wanapambana (wachezaji), lakini bado siwezi kumlaumu ikiwa aliipa timu yangu penalti zimebaki dakika tisa,"alisema.
Azam sasa imetolewa kwa jumla ya mabao 2-1, baada ya awali wiki mbili zilizopita kutoka sare ya bila kufungana Dar es Salaam na Waarabu hao.
Rabat sasa watamenyana na moja ya timu zilizotolewa katika Ligi ya Mabingwa kusaka tiketi ya kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shikrikisho.
Katika mchezo huo, kikosi cha Azam FC kilikuwa; Mwadini Ally, Himid Mao, Waziri Salum, David Mwantika, Joackins Atudo, Kipre Balou, Kipre Tchetche, Salum Abubakar, John Bocco, Humprey Mieno/Gaudence Mwaikimba dk79 na Brian Umony/Khamis Mcha dk70.
AS FAR Rabat; Ali Grouni, Anouar Younes/Ennajar Tarik, Younes Hammal, Younes Belakhdar, Kaddoui Youssef, Abdelrahim Achchakir, Aqqal Salaheddine/Alloudi Soufiane, Mustafa Allaoui, El Kodry Yassine, El Bakkali Medamine na El Yousfi Mostafa.

sosi:
http://bongostaz.blogspot.com/2013/05/azam-fc-yafa-kiume-rabat-bocco-akosa.html
 
Azam FC imetwaa nafasi ya pili ya ligi kuu baada ya kuifunga JKT Mgambo Shooting Stars 3-0 katika mchezo uliochezwa Chamazi, Magoli ya Azam FC yamefungwa na John Bocco, Kipre Tchetche na Jockins Atudo

Thanks Azam FC for made my weekend..
 
[h=5]Maproo Azam FC waanza likizo, kuikosa JKT Oljoro

Baada ya kutwaa nafasi ya pili kwenye ligi kuu msimu wa 2012/2013 kocha wa Azam FC Stewart Hall amewapa likizo wachezaji wake wa kimataifa hivyo hawatacheza mechi ya mwisho ya kumaliza ligi dhidi ya JKT Oljoro itakayochezwa siku ya Jumamosi mkoani Arusha.

Wachezaji hao wamechangia kiasi kikubwa cha kuifikisha timu katika mafanikio hayo pamoja na kufanya vizuri kwenye mechi za kimataifa za Kombe la Shirikisho Afrika ambapo timu hiyo ilimaliza ikiwa imecheza mechi sita katika hatua tatu za mashindano hayo makubwa barani Afrika.

Akizungumza na www.azamfc.co.tz kocha Stewart aliwataja wachezaji hao kuwa ni Kipre Tchetche, Michael Bolou wa Ivory Coast, Humphrey Mieno na Jockins Atudo wa Kenya pamoja na mshambulia Brian Umony wa kutoka nchini Uganda.

Stewart amesema ameamua kuwapa mapumziko wachezaji hao ili wakae pamoja na familia zao kwa muda mrefu kutokana na mechi ya mwisho haitakuwa na umuhimu sana zaidi ya kumalizia ratiba kwa kuwa wameshapata nafasi ya pili na pia wametoa mfungaji bora.

"Kwangu kumpumzisha Kipre ni kutokana na mchezaji huyo kufunga magoli mengi ambayo hayatafikiwa na mchezaji yoyote, pia tumepata ushindi wa pili hivyo nimeona waende nyumbani kwa kuwa ni muda mrefu hawajakaa na familia zao" amesema Stewart.

Azam FC Jumamosi, Mei 18, itamaliza mechi zake za ligi kuu ikiwa ugenini dhidi ya JKT Oljoro kwenye mchezo utakaochezwa uwanja wa kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha, Azam FC inacheza mechi hiyo ikiwa na pointi 51, mshambuliaji Kipre amefikisha jumla ya magoli 17 ya kufunga.

Akizungumzia mchezo huo kocha Stewart amesema kikosi cha mechi hiyo ya mwisho kitaundwa na wachezaji wa ndani ambao watashirikiana pamoja na wachezaji vijana waliopo katika timu yake.

Michael Bolou na Tchetche Kipre wanatarajiwa kuondoka siku ya Alhamisi kuelekea kwao nchini Ivory na wachezaji wa Tanzania wataanza mapumziko yao mara baada ya kumaliza mchezo wa ligi kuu siku ya Jumamosi.

[/h]
 
[h=5]Azam are the most successful club in CAF competitions from East Africa. I't's official!
[/h]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…