The Official Azam FC Thread

The Official Azam FC Thread

Azam, KACC, URA watinga nusu fainali Mabingwa watetezi wa kombe la mapinduzi, Azam FC pamoja na timu mbili za Uganda; KCC na URA wamefanikiwa kutinga nusu fainali ya mashindano ya kombe la Mapinduzi yanayoendelea Zanzibar baada ya kuwabwaga wapinzani wao kwenye michezo ya robo fainali iliyopigwa leo Unguja na Pemba. Katika mchezo ulipigwa saa nane mchana, Azam ilikuwa ya kwanza kutinga nne bora baada ya kuwabwaga Cloves Stars ya Pemba kwa magoli 2-0 yote yakifungwa kipindi cha pili na walinzi Aggrey Morris na Waziri Salaum. Mchezo wa pili kwenye uwanja wa Gombani Pemba, watoza ushuru wa Uganda, URA wamewafyatua maafande/mabaharia KMKM kwa goli 1-0 la Owen Kasule dakika ya 42, sikisalia dakikatatu kabla ya mapumziko kwa mkwaju wa chinichini baada ya walinzi kuzembea kuondoa mpira langoni. Kwenye mchezo wa Unguja KCC wamefanikiwa kucheza nusu fainali wakiwatoa mashindanoni makamu bingwa wa mwaka jana Tusker ya Kenya katika changamoto ya mikwaju ya penati baada ya dakika 90 kumalizika huku timu hizo zikiwa 0-0. KCC walifaniukiwa kuweka kimiani penati zao zote 4 wakati Tusker wakifunga tatu tu na moja ya Ismail Dunga ikiokolewa na mlinda lango Salim Magoola na ya Luke Ochieng ikigonga mlingoti wa goli Katika mchezo huo Tusker walilazimika kucheza dakika nne za mwisho wakiwa 10 baada ya kiungo Osborne Monday kutolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kuoneshwa kadi ya pili ya njano. Masuala mengine mawili muhimu ya mchezo huo ni la walinda milango wawili Ochieng na Magoola kupiga mikwaju yao ya penati kwa kufuatana na kufunga, na pia timu ya Tusker kumaliza dakika 90 bila kupiga hata mkwaju mmoja uliolenga lango huku KCC wakipiga mikwaju 5 langoni ambayo ama iliokolewa na kipa au kugonga mwamba. Steven Bengo wa KCC ameteuliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo na hivyo anazawadiwa kisimbuzi cha AzamTV. Huu ni utaratibu utakaokuwa ukifanyika katika michezo yote iliyobakia hadi fainali Kwa matokeo hayo Azam itacheza na KCC katika nusu fainali ya kwanza huku URA wakicheza na mshindi kati ya Simba na Chuoni ya Zanzibar watakaokutana kwenye mchezo wa baadaye leo usiku kuanzia saa 2. Nusu fainali zote mbili zitachezwa Ijumaa hii na fainali ni Jumatatu Januari 13.

credit azam tv
 
Kwani kuna Mwana Azam wa humu ndani aliyekuwa anategemea Azam watatwaa ubingwa?
 
Changing Room
1524817_690443350996024_1112678292_n.jpg
 
VIP room za uwanja wa Azam Fc kama zinavyoonekana
1512674_689922681048091_1674994552_n.jpg
 
Uwanja wa Azam Complex Chamazi kama unavyoonekana. Uwanja huu upo katika maboresho ya kawaida ya kila mwaka. Azam FC imedhamiria kucheza mechi zake za CAF Chamazi
1601032_689414894432203_1108372288_n.jpg
 
Azam FC, Kikosi kinachoanza leo ni Mwadini
Erasto
Malika
Moradi
Aggrey
Bolou
Himid
Sureboy
Brian
Kipre
Kimwaga
Substitute
Aishi
David
Popo
Jabir
Mcha
Kone
Karihe
 
Azam tusipochukua ndoo msimu huu sijui tutajitetea vipi..Maana naiona timu ikiwa iko njema sana.

"Nlikuwepo":bolt:
 
Azam FC
Mwadini, Malika, Erasto, Aggrey, Moradi, Bolou, Himid, Sure Boy, Kone, Kipre & Kimwaga
 
Back
Top Bottom