The Official Azam FC Thread

Azam mmezoea lambalamba

wenzenu mozambique wanakula magimbi
mtawaweza wapi na usoft wenu uo
 
Azam mmezoea lambalamba

wenzenu mozambique wanakula magimbi
mtawaweza wapi na usoft wenu uo

ushindi finyu nyumbani usitegemee kushinda ugenini na hili wanalijua sema wanajifanya hawajui bora tumskilizie yanga atafika wapi..
 
ushindi finyu nyumbani usitegemee kushinda ugenini na hili wanalijua sema wanajifanya hawajui bora tumskilizie yanga atafika wapi..

Sisi Yanga, historia haitupi nafasi hata ya 1% kusonga mbele; kama Goliathi aliuawa na kijana Daudi vivyo hivyo tunasubiri miujiza kuwatoa hao Waarabu. Mungu ibariki Yanga Afrika isonge mbele.
 
ushindi finyu nyumbani usitegemee kushinda ugenini na hili wanalijua sema wanajifanya hawajui bora tumskilizie yanga atafika wapi..

Inategemea na timu Mnyama mkali wa porini alishabitisha kwamba unaweza kufanya vibaya nyumbani na ukafanya vizuri ugenini au kinyume chake, rejea mambo ya Mfulira wanderers na Stella Abidjan, nadhani utakuwa umenielewa. Mozambique ni wazuri sio sawa na Wacomoro. Poleni sana washabiki wa Azam.
 
Sisi Yanga, historia haitupi nafasi hata ya 1% kusonga mbele; kama Goliathi aliuawa na kijana Daudi vivyo hivyo tunasubiri miujiza kuwatoa hao Waarabu. Mungu ibariki Yanga Afrika isonge mbele.

Hapo umenena maana bahati nayo kwenye mpira hutokea sana, inawezekana siku hiyo bahati ya ushindi ikawa upande wenu kama ilivyoangukia kwa Simba kipindi kile wanawatoa Zamalek, Inabidi wachezaji wenu wajipange na wakifika golini waache uzembe la sivyo mtajuta kuwafahamu hao wamisri.
 
Nakubaliana nawe 100%. Unakumbuka SSC ilivyotolewa na Textile de Pungu ya Msumbiji?
 
Ushauri umepokelewa, utafanyiwa kazi.
 
Nakubaliana nawe 100%. Unakumbuka SSC ilivyotolewa na Textile de Pungu ya Msumbiji?

Mkuu kwa ujumla Msumbiji ni kipimo kizuri kwa timu zetu, kuanzia vilabu hadi timu ya Taifa with exception to female football team maana walitolewa kwa jumla ya magoli 15 labda na Azam walienda na reference ya matokeo ya timu ya wanawake.
 
tushapoa sana mkuu..
 
Nilimsikia Maganga Jaffar akijitapa kuwa Azam itaifunga Ferroviario kwao; nakumbuka ile 1993 SSC ilipofika fainali CAF, Simba 1-0 FeV Tz na FeV 1-0 Moz, SSC ilishinda kwa matuta. Over-confidence huwa si nzuri, wajipange mwakani.
 
Sisi Yanga, historia haitupi nafasi hata ya 1% kusonga mbel; kama Goliathi aliuawa na kijana Daudi vivyo hivyo tunasubiri miujiza kuwatoa hao Waarabu. Mungu ibariki Yanga Afrika isonge mbele.

Mkuu Mbona Kikos Chako Hukiamin Kiasi Hicho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…