The Official Azam FC Thread

Leo hapo chamazini..

1. AISHI MANULA
2. SHOMARI KAPOMBE
3. GADIEL MICHAEL
4. AGGREY MORIS
5. PASCAL WAWA
6. MUDATHIR YAHYA
7. FRANK DOMAYO
8. SALUM ABUBAKAR
9. GAUDENCE MWAIKIMBA
10. DIDIER KAVUMBAGU
11. BRIAN MAJWEGA

AKIBA
1. MWADINI ALI
2. AMRI KIEMBA
3. BRAISON RAFAEL
4. FARIDI MUSSA
5. KIPRE TCHETCHE
6. ABDALLAH MASOUD
7. CHRISTOPHER MSHANGA
 
Huu msiba utakuwa mkubwa sana kwa wapiga debe hawa...
 
Full Time: Azam fc 4 - 0 Stand Utd Majegwa, Mwaikimba 2, Farid well done lads..
 
Azam FC yaanza kwa ushindi CECAFA Kagame Cup

By ppkahemele on July 19, 2015

Ikitumia mfumo wa 3-5-2 Azam FC leo imeichapa KCCA ya Uganda bao 1-0 goli lililofungwa na straika na nahodha John Bocco 'Adebayor'
Bocco aliiandikia bao hilo pekee lililowapa ushindi na pointi tatu dakika 11 kutokana na pasi ya Salum Aboubakary 'Sure Boy. Kabla ya kufunga Bocco alimfinya beki wa KCCA na kufunga kwa ufundi.
Azam iliyokuwa inacheza soka ya kuvutia kwa fomesheni hiyo ya 3-5-2 ambapo nyuma aliwatumia mabeki wa kati watatu Serge Wawa, Aggrey Morris na Said Morrad na kiungo kati akacheza Sure Boy, Himid Mao na Frank Domayo ikawafanya wang'are zaidi.

Ilifanya mabadiliko dakika ya 46 kwa kumtoa Mrundi Didier Kavumbagu na Muivory Coast Kipre Tchetche kuchukua nafasi, dakika 65 Frank Domayo alitoka akaingia Mnyarwanda Mugiraneza Jean Baptiste, dakika 82 alitoka Sure Boy akaingia Mudathir Yahya.
Kocha mkuu wa Azam Stewart Hall alisema, anashukuru kupata ushindi huo, vijana wake walicheza kwa kufuata ,maelekezo ndiyo maana walishinda. Pia fomesheni waliyobadili ni moja ya sababu ya ushindi huo.

Azam
Aishi Manula, Shomary Kapombe, Erasto Nyoni, Serge Wawa, Aggrey Morris, Said Morrad, Himid Mao, Salum Aboubakary 'Sure Boy, Frank Domayo, Didier Kavumbagu, John Bocco.

KCCA
Ochan Benjamin, Masiko Tom, Kavuma Habib, Mpuga Martin, Wasswa Hassan, Senkumba Hakim, Okot Denis, Nsibabambi Derrick, Mutyaba Muzamir, Ochaya Joseph Birung Michael.

Source: Azam FC yaanza kwa ushindi CECAFA Kagame Cup | The Official Website of Azam Football Club


Scorer of the only goal for Azam FC John Bocco (Right) pressuring KCCA player Joseph Ochaya during the CECAFA Kagame cup 2015 in Dar-es-Salaam, Tanzania. Final score Azam FC 1 - KCCA 0. Photo Courtesy of Bin Zubeiry Blog AZAM FC YAANZA VYEMA KAGAME, YAIKALISHA KCCA TAIFA | BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE
 
July 21, 2015
Dar-es-Salaam, Tanzania

By ppkahemele

Azam FC yatinga robo fainali CECAFA, yaifunga Malakia 2-0

Ikicheza soka la kiwango cha juu na kuvutia Azam FC leo imeifunga Malakia ya Sudan Kusini 2-0 shukrani kwa magoli ya John Bocco dk 27 na Kipre Tchetche dk 52.
Bocco alifunga goli hilo kwa mpira wa adhabu ndogo alioupiga kwa ustadi mkubwa sana na goli la Kipre Tcheche lilitokana na kazi nzuri ya Shomari Kapombe aliyewazidi maarifa walizi wa tatu wa Malakia na kutoa pasi kwa mfungaji ambaye hakufanya ajizi kwa kuukwamisha mpira kwenye nyavu.
Azam FC ambayo inafundishwa na mwalimu mwenye uzoefu na weledi wa hali ya juu Stewart Hall, imebadili mfumo wa uchezaji toka 4-3-3 na sasa inatumia mfumo wa 3-5-2 leo imeutendea haki mfumo huo kwa kucheza kwa kuelewana na kwa ustadi mkubwa.
Ukilinganisha na muda uliotumika kuandaa timu, sifa za kipekee ziende kwa kocha Stewart Hall na benchi lake la ufundi pamoja na wachezaji wote ambao bila shaka wamefanya kazi kubwa sana.
Wachezaji wote leo wametimiza majukumu yao lakini sifa za kipekee ziende kwa mchezaji kinda na mgeni kwenye kikosi cha kwanza Abdallah Kheri SEBO ambaye amecheza kwa kiwango kikubwa sana.
Azam FC sasa imetimiza pointi sita na inaongoza kundi lake.


Azam FC players celebrating their win over Malakia FC in today's match of CECAFA Kagame Cup 2015 held in Dar-es-Salaam, Tanzania. Final results Azam FC 2 - Malakia 0. The results guarantees Azam FC a place to play in the quarter finals of the tournament.

Source: Azam FC yatinga robo fainali CECAFA, yaifunga Malakia 2-0 | The Official Website of Azam Football Club
 
July 25, 2015
Dar-es-Salaam, Tanzania

CECAFA Kagame Cup 2015: Tchetche kuanza. Bocco, Sure Boy wapumzishwa mechi ya Azam Vs Adama City

By ppkahemele

Straika Muivory Coast Kipre Tchetche aliyekuwa anaingia 'sabu', siku ya jumamosi ataanza kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha Azam FC kitakachoivaa Adama City ya Ethiopia katika mechi ya muendelezo wa mashindano ya Kombe la Kagame kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Tchetche atacheza straika kuchukua nafasi ya John Bocco 'Adebayor' ambaye atakuwa jukwaani kama shabiki na pacha atakayecheza naye kwa mfumo wa 3-5-2 atakuwa Ame Ally au Mrundi Didier Kavumbagu.

Kocha mkuu wa Azam FC, Muingereza Stewart Hall amesema, atampumzisha Bocco ili awe tayari kwa mechi ya robo fainali kwa sababu tayari wameshafuzu.

"Tchetche ataanza mechi ya jumamosi kwenye kikosi cha kwanza na nitamchezesha na Kavumbagu au Zungu, yoyote kati ya hao wawili atakayeamka vizuri.

"Nitampumzisha pia, kipa Aishi Salum na golini atasimama Mwadin Ally na kwenye kiungo, Salum Aboubakary 'Sure Boy' naye atapumzika, yeye ana maumivu ya enka,"alisema Stewart.

Stewart amesema maandalizi ya mchezo huo yanakwenda vizuri na kila kitu kinakwenda sawa na msimu huu, anataka kulibakisha kombe la Kagame Chamazi.

Tangu michuano hiyo ianze, Tchteche alikuwa mchezaji wa akiba na alikuwa akiingia kipindi cha pili, hivyo mechi hiyo itakuwa ya kwanza kuanza kwake.

Source: Tchetche kuanza. Bocco, Sure Boy wapumzishwa mechi dhidi ya Adama City | The Official Website of Azam Football Club
 
July 25, 2015
Dar-es-Salaam, Tanzania

CECAFA Kagame Cup 2015

Today's fixtures
KCC vs. Malakia 2pm
Adama City vs. Azam 4pm
 
July 25, 2015
Dar-es-Salaam, Tanzania

By By ppkahemele

Azam FC yaongoza kundi; yaitandika Adama City 5-0

Ikicheza soka safi la hali ya juu na kuelewana muda wote wa dakika 90, Azam FC leo imeigaragaza vibaya Adama City FC jumla ya mabao 5-0 na kujihakikishia uongozi wa kundi kwa “style” mbali na kutinga robo fainali huku huku nyavu zake zikiwa hazijaguswa.

Winga kinda mwenye kipaji cha hali ya juu Farid “Maliki” Mussa Shah kiibuka mchezaji bora wa mechi na kukomba zawadi toka wa wadhamini DSTV.

Azam FC waliandika bao la kwanza kupitia kwa Kipre Tchetche dakika ya saba akimalizia pasi kutoka kwa Amme Ally Zungu.

Kipre aliipatia tena bao la pili dakika 19, alikuwa kwenye engo kilipo kibendera nje kabisa ya 18, akamwangalia mlinda lango wa Adama City, Yacob Fiseha alivyokaa na kupiga mpira kiufundi uliokwenda moja moja golini.

Azam FC ilipachika tena bao la tatu dakika dakika ya 32 kupitia kwa Farid Mussa.

Azam ilianza kipindi cha pili kwa kasi na kupata bao la nne dakika ya 49 lililofungwa na Mudathir Yahya kwa kichwa kabla ya Aggrey Morris kufunga karamu ya mabao alipopachika la tano kwa njia ya penalti dakika ya 69.

Penalti hiyo ilipatikana baada ya Mogesi Tadese wa Adama City kuokoa kwa mkono, shuti la Mudathir na akatolewa kwa kadi nyekundu.

Pia beki mwingine wa Adama Eshetu Menna alitolewa nje kwa kadi nyekundu.
Source: Azam FC yaongoza kundi; yaitandika Adama City 5-0 | The Official Website of Azam Football Club
 
July 29, 2015
Dar-es-Salaam, Tanzania

Azam FC yatinga nusu fainali CECAFA Kagame Cup 2015

By ppkahemele

AZAM FC imefanikiwa kutinga Nusu Fainali ya CECAFA Kagame Cup baada ya ushindi wa penalty 5-3 baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90.

Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, shujaa wa Azam FC alikuwa ni kipa Aishi Salum Manula aliyepangua penalti ya beki mpya wa kushoto wa Yanga SC, Mwinyi Hajji Mngwali.

Wachezaji Kipre Herman Tchetche, Serge Wawa Pascal wote raia wa Ivory Coast, John Bocco, Himid Mao na Aggrey Morris walifunga penati zao, wakati za Yanga SC zilifungwa na Nadir Haroub ‘Cannavaro', Salum Telela na Godfrey Mwashiuya.
katika mtanange wa dakika tisini Azam FC iliutawala mchezo hasa kipindi cha kwanza na kukosa magoli mengi kupitia kwa John Bocco, Kipre Tchetche na Shomari Kapombe


Azam FC sasa itamenyana na KCCA ya Uganda katika Nusu ya pili Ijumaa, baada ya Khartoum N na Gor Mahia kupambana katika Nusu Fainali ya kwanza.

Utamu ni kwamba, Nusu Fainali zote zitakuwa marudio ya mechi za makundi, kwanza Azam FC iliifunga 1-0 KCCA katika mechi ya Kundi C na Khartoum N ilitoka sare ya 1-1 na Gor Mahia katika mchezo wa Kundi A.
Farid Mussa kwa mara nyingine alikuwa nyota wa mchezo wa leo

Kikosi cha Azam FC kilikuwa: Aishi Manula, Shomari Kapombe, Agrey Morris, Abdallah Kheri/Said Mourad dk46, Paschal Wawa, Jean Mugiraneza, Himid Mao, Frank Domayo/Ame Ally dk46, Farid Mussa, John Bocco na Kipre Tchetche.

Yanga SC: Ally Mustafa ‘Barthez', Nadir Haroub ‘Cannavaro', Juma Abdul/Joseph Zuttah dk69, Godfrey Mwashiuya, Donald Ngoma, Kevin Yondani, Mbuyu Twite, Deus Kaseke/Salum Telela dk61, Amisi Tambwe, Haruna Niyonzima/Malimi Busungu dk80 na Hajji Mwinyi.
Source: Azam FC yatinga nusu fainali Kagame Cup | The Official Website of Azam Football Club

 
July 30, 2015
Dar-es-Salaam, Tanzania

Nusu fainali CECAFA Kagame Cup 2015 Azam FC vs KCCA na Al Khartoum Vs Gor Mahia

Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM

NUSU Fainali za michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame inatarajiwa kuendelea kesho katika Uwanja wa Taifa, huku kiingilio cha chini katika michezo hiyo kikiwa ni Sh 3,000.

Viingilio vingine vya michezo hiyo ya kesho ni VIP A ni shilingi elfu kuni na tano (15,000) na VIP B & C, Shilingi elfu kumi (10,000) na sehemu nyingine ya uwanja iliyobakia ni shilingi elfu tatu (3,000) kwa viti vya rangi ya bluu, kijani na rangi ya chungwa.

Timu nne kutoka katika nchi nne wanachama wa michuano hiyo, Azam FC (Tanzania), Gor Mahia (Kenya), KCCA (Uganda) na Al Khartoum (Sudan) zimefuzu kwa hatua ya nusu fainali itayochezwa uwanja wa Taifa siku ya ijumaa.

Mchezo wa kwanza utakaonza saa 7:30 mchana utazikutanisha timu za Gor Mahia ya Kenya itakayocheza dhidi ya Khartoum ya Sudan, mchezo unaotarajiwa kuwa wa vuta nikuvute kufutia timu hizo kutoka sare katika mchezo wake wa awali hatua ya makundi.

Katika mchezo wa kwanza uliozikutanisha timu hizo, kocha wa Khartoum Kwesi Appiah na Frank Nuttal wa Gor Mahia walitoka sare ya bao 1- 1 ndani ya dakika 90, hali ambayo inapelekea kufaya mchezow wa kesho kuwa mgumu kwa kila timu kuhitaji nafasi ya kusonga mbele hatua ya fainali.
Gor Mahia mabingwa mara tano wa michuano hiyo, wataingia uwanjani kusaka ushindi ili kusonga hatua ya fainali ili waweza kutwaa ubingwa huo kwa mara ya sita, sawa na klabu ya Simba inayoongoza kwa kutwaa ubingwa huo.

Kocha Frank Nuttal atakua akiwategemea wachezaji wake nyota, Khalid Alucho, Kagere Meddie, Michael Olunga, Sibomana Abouba, Karim Nzigiyimana, Godfrey Walusimbi, Nahodha Musa Mohamed, na mlinda mlango Boniface Oluoch katika kusaka ushindi dhidi ya Khartoum.
Kwesi Appiah atashuka dimbani akiwategemea wachezaji wake nyota, Antony Akumu, Dominic Abdui, Samawal Meshani, Wagdi Wawd, Ouismaila Baba na nahodha Amin Ibrahim.

Vita kali itakua kwa washambulaji Michael Olunga wa Gor Mahia na Salaheldin Osman wote wenye mabao manne, wakiwania kuongeza bao katika mchezo huo wa kesho ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kutwaa kiatu cha dhahabu.

Nusu fainali ya pili itawakutanisha waoka mikate wa Azam FC dhidi ya Mamlaka ya jiji la Kampala (KCCA), mchezo utaokanza majira ya 9:45 kwa saa za Afrika na Kati katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Mchezo huo pia unatarajiwa kuwa na upinzani mkali kufutia timu hizo katika mchezo wa hatua ya makundi, Azam FC kuibuka na ushindi wa bao 1- 0, bao liliofungwa na nahodha wake John Bocco.

KCCA chini ya kocha wake Mike Mutebi watashuka dimbani kusaka ushindi katika mchezo huo, ikiwa ni kulipiza kisasi kwa mchezo wa kwanza na kupata ushindi utakaowavusha mpaka katika hatua ya fainali.

Kocha Mutebi atakuwa akiwategmea wachezaji wake nyota, Nahodha Tom Matiko, Opio Emmanuel, Joseph Ochaya, Hassan Waswa, Isaac Sserenkuma, Habib Kavuma na Muzamil Mutyaba.

Azam FC itashuka dimbani kutaka kuendeleza ubabe wake dhidi ya KCCA ya Uganda, na kuweza kukata tiketi ya kucheza fainali siku ya jumapili katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Kocha wa Stewart Hall wa Azam atakua akijivunia safu yake ya ulinzi ambayo haijaruhusu bao tangu kuanza kwa michuano hiyo, huku safu yake ya ushambuliaji ikiwa imefunga mabao 8 katika michezo mine iliyocheza.

Hall atashuka dimbani akiwategema nyota wake Nahodha John Bocco, Pascal Wawa, Aggrey Morris, Himid Mao, Kipre Tchetche, Jean Baptist Mugiranenza, Frank Domayo na mlinda mlango Aishi Manula.

Wakati huo huo: Rais wa TFF, Jamal Malinzi ametuma salam za pongezi kwa klabu ya Azam FC kwa kufanikiwa kuingia katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Kagame inayotimua vumbi jijini Dar es salam.

Katika salamu zake kwa uongozi wa klabu ya Azam, Malinzi amewataka kutobweteka na kuongeza bidii katika hatua hiyo ya nusu fainali ili waweze kufuzu kwa hatua ya fainali na kutwaa Ubingwa huo na kuwaomba watanzania wote kuwasapoti wawakilishi pekee wa nchi kwenye michuano hiyo.
TFF kwa niaba ya familia ya mpira na watanzania wote, inatwakia kila la kheri Azam FC katika mchezo wake wa kesho wa nusu fainali dhidi ya KCCA.
Source: KIINGILIO AZAM NA KCCA, KHARTOUM NA GOR MAHIA NUSU FAINALI KAGAME BUKU TATU TU | BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE

 
July 31, 2015

Dar-es-Salaam, Tanzania

CECAFA Kagame Cup 2015

Hureeeeee.... Azam FC yatinga fainali CECAFA Kagame Cup


Photo: Azam FC players celebrating their victory over KCCA Club during the CECAFA Kagame Cup 2015 semi final tie in Dar-es-Salaam, Tanzania. Final score Azam FC 1 - KCCA 0.

By ppkahemele

Azam FC imetinga hatua ya fainali za CECAFA Kagame Cup kwa mara ya pili baada ya kuichapa KCCA ya Uganda bao 1 - 0 na sasa itacheza fainali jumapili usiku katika dimba la uwanja wa taifa na Gor Mahia ya Keny.

Sifa zimwendee winga Farid Mussa aliyepachika bao hilo dakika ya 76 baada ya kupokea krosi nzuri ya Ame Ally. Katika mchezo huo ambao kwa mara nyingine beki , Muivory Coast Serge Wawa kachaguliwa kuwa mchezaji bora 'Man of the Match.

Azam FC ilikuwa ishangilie ushindi huo mapema kupitia kwa straika Muivory Coast Kipre Tchetche katika dakika ya 33 na 39 lakini ya mashuti yake kutoka nje.

Hata hivyo, mlinda lango, Aishi Manula alifanya kazi ya ziada dakika ya 36 alipookoa shuti la Sserunkuma Isaac ikawa kona tasa.

Azam FC ililiandama lango la KCCA baada ya kocha Stewart Hall kufanya mabadiliko kipindi cha pili kwa kuwatoa Mudathir Yahya na naasi yake kuchukuliwa na Ame Ally, Erasto Nyoni akaingia Shomari Kapombe na Kipre Tchetche akaingia Didier Kavumbagu.

Kikosi cha Azam FC leo kilikuwa; Aishi Manula, Erasto Nyoni/ Shomari Kapombe, Said Morrad, Aggrey Morris, Wawa, Mugiraneza, Mudathir Yahya/ Ame Ally, Domayo, Tchetche/ Kavumbagu, arid Mussa, John Bocco,

Source: Hureeeeee.... Azam FC yatinga fainali CECAFA Kagame Cup | The Official Website of Azam Football Club
 
Aug 2, 2015
Dar-es-Salaam, Tanzania

CECAFA Kagame Cup 2015 Final : Azam FC vs Gor Mahia : Kick off time 15:45 Hrs (EAT) Venue National stadium Dar-es-Salaam, Tanzania.


TEAM PHOTO: AZAM FC of Dar-es-Salaam, Tanzania
 
Mimi Yanga ila UZALENDO kwanza. Azam shindeni mchukue kombe libaki nyumbani.
 
Azam watulie walianzanza vizuri naona Kama wamechanganyikiwa hivi sasa.wataumia sasa hivi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…