The Official Azam FC Thread

Bidvest Wits of South Africa hammered by Tanzania's Azam FC

. Bidvest Wits fell to a 3-0 defeat to Azam Fc of Tanzania in their first leg Confederation Cup first round tie at the Bidvest Stadium on Saturday evening. The Tanzanian side grabbed three goals in ten minutes. Abubakar Sureboy scored the first in 51st minute while Shomari Kapombe scored in 57th minute and captain John Bocco killed the game at 60th minute.

Bidvest Wits 0-3 Azam FC (Confederation Cup First Leg) in Johannesburg, South Africa
Source: Azam Football Club youtube
 
Me najuaga azam ni ice cream. kumbe kuna timu pia inaitwa azam heeee....!!! makubwa haya
 

Tabogo Moerane (Right) of Bidvest Wits is challenged by Shomari Salum Kapombe of Azam FC during the CAF Confederation Cup match between Bidvest Wits and Azam on 12 March 2016 at Bidvest Stadium. Final Results Bidvest Wits 0 - Azam FC 3. Pic Sydney Mahlangu/ BackpagePix Azam thrash Wits in Confederation Cup clash
 
Machi 14, 2016

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KOCHA Msaidizi wa Azam FC, Mario Marinica raia wa Romania amesema beki wa kati Aggrey Morris sasa yuko fiti kwa asilimia 100 kuisaidia klabu hiyo katika kampeni za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Urejeo wa Aggrey Morris?
Aggrey Morris alirejea uwanjani Jumamosi Machi 12, 2016 kwa mara ya kwanza baada ya kuwa nje tangu Oktoba mwaka jana kutokana na maumivu ya goti na akaiongoza timu kuishinda Bidvest Wits 3-0 ugenini katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza Kombe la Shirikisho Afrika mjini Johannesburg, Afrika Kusini.
"Ametoka kwenye majeraha makubwa na ameonyesha kiwango kizuri leo (Jumamosi) ni ngumu kusema alikuwa mchezaji bora uwanjani, lakini ni mmoja wa wachezaji waliowadhibiti wachezaji wa Bidvest na sisi kutofungwa bao ugenini,” alisema Mario.

Aggrey Morris (kushoto) akifurahia na Himid Mao (katikati) na Erasto Nyoni (kulia) baada ya mechi na Bidvest

Kocha Mkuu, Stewart Hall akimpa 'tano' Aggrey Morris baada ya mechi Bidvest Wits Vs Azam FC

Source: Hisani kubwa ya Bin Zubeiry : KOCHA AZAM FC ASEMA MORRIS AMERUDI KAMILI KUONGEZA NGUVU VITA YA UBINGWA | BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE
 
Azam FC yaipiga Stand Utd, Kapombe azidi kufanya kweli
By ppkahemele on March 16, 2016

KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, imezidi kufanya kweli kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) baada ya jioni ya leo kuichapa Stand United bao 1-0 katika mchezo mkali uliofanyika Uwanja wa Azam Complex.

Alikuwa ni beki wa kulia Shomari Kapombe, aliyeihakikishia pointi tatu muhimu Azam FC baada ya kufunga bao zuri dakika ya 62 akiserereka chini na kupiga shuti lililigonga nyavu za juu akimalizia krosi safi ya nahodha John Bocco ‘Adebayor’ aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Allan Wanga.

Stand United walicheza mchezo huo kwa kulundikana eneo moja kila Azam FC ilipokuwa na mpira kuliwanyima mabingwa hao nafasi ya kuuchezea mpira hasa safu ya ushambuliaji iliyokuwa ikiundwa na Tchetche aliyekuwa akisaidiana na Wanga na hivyo kufanya kipindi cha kwanza kuisha kwa suluhu.

Hadi dakika 90 za mwamuzi Ngole Mwangole kutoka mkoani Mbeya zinamalizika, walikuwa ni Azam FC walioweza kuibuka kifua mbele na kuzoa pointi zote tatu.

Ushindi huo unaifanya Azam FC kuifikia Yanga kwa pointi, wote wakiwa nazo 50 huku akiwa ameachwa kwa pointi nne na kinara Simba iliyojikusanyia jumla ya pointi 54 lakini iko mbele kwa michezo miwili dhidi ya wapinzani wake hao katika mbio za ubingwa.

Kikosi cha Azam FC kiliundwa;

Aishi Manula, Shomari Kapombe, Farid Mussa/Wazir Salum (dk 65), Aggrey Morris, Pascal Wawa, Erasto Nyoni, Jean Mugiraneza, Frank Domayo, Mudarhir Yahya/Michael Bolou (dk 79), Kipre Tchetche, Allan Wanga/John Bocco (C) dk 45.

Source: Azam FC yaipiga Stand Utd, Kapombe azidi kufanya kweli | The Official Website of Azam Football Club
 
Machi 18, 2016

Esperance ya Tunisia Yabisha hodi Azam FC

MECHI kati ya Azam FC na Esperance ya Tunisia ipo njiani. Hiyo inafuatia timu zote kushinda mechi zao za kwanza ugenini za Raundi ya Kwanza Kombe la Shirikisho Afrika mwishoni mwa wiki.

Wakati Azam FC iliaadhibu Bidvest Wits mabao 3-0 mjini Johannesburg, Afrika Kusini Jumamosi, Esperance iliichapa mabao 2-0 Renaissance nchini Chad siku hiyo hiyo.

Na hii itakuwa mara ya kwanza kabisa kwa Azam FC kwa ujumla kwenda kucheza Tunisia, ingawa si mara ya kwanza kucheza nchi za Kaskazini mwa Afrika, wakati Esperance si wageni Tanzania, kwani wamekwishakuja mara kadhaa.

Mara ya mwisho Esperance iliitoa Yanga SC katika Raundi ya Pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2007 kwa jumla ya mabao 3-0, iliyoshinda mjini Tunis kabla ya kutoa sare ya 0-0 mjini Mwanza.

Mwaka 2013 Azam FC ilitolewa na FAR Rabat ya Morocco baada ya sare ya 0-0 Dar es Salaam kabla ya kwenda kufungwa 2-1 mjini Rabat.

Source: Habari kwa hisani kubwa ya Bin Zubeiry ESPERANCE YABISHA HODI AZAM FC | BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE
 
Mar 19, 2016

Bidvest Wits unapologetic about how they set to approach CAF competition game against Azam FC 20/03/2016.

Bidvest Wits head coach Gavin Hunt is unapologetic about how they set to approach the CAF competitions and gave an impression that this is a club’s policy. Hunt says that in the second leg match against Azam Fc they will be fielding the second string team because he cannot ‘risk’ his core team. The Clever boys will play-up against Azam Fc tomorrow the 20th of March 2016, 14:00 PM at Chamazi Stadium, Dar es Salaam, Tanzania.

Source: Soccer SABC Sports Wits top the league
 
Posted: 20 March 2016 Time: 14:08



Bidvest Wits trails Azam 2-1 at half-time of their second leg CAF Confederations Cup first round tie in Tanzania, and trail 5-1 on aggregate.

Azam netted twice in the first half, while The Clever Boys managed to pull one back right on the stroke of half-time to narrow the lead to just one goal at the break.

However, Gavin Hunt's side now trail 5-1 on aggregate with just 45 minutes left in the tie. CAF Confed Cup First Round Second Leg: Azam FC vs Bidvest Wits
 
Matokeo baada ya kuisha dakika tisini Chamazi Complex, Dar-es-Salaam, Tanzania. Azam FC 4 - Bidvest Wits 3. John Bocco afunga bao 1 na Tchetche amefuga 3 hat-trick leo ktk mchezo huo wa pili.

Jumla ya matokeo baada ya timu hizo kukutana mara mbili ugenini na nyumbani ni Azam FC 7 - Bidvest Wits 3. Azam sasa watakutana na Esperance ya Tunisia katika hatua ifuatayo ya mashindano haya ya Afrika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…