The Official Azam FC Thread

MWARABU ANADHARAU AMESEMA YEYE HATAKI CHA AGREGATE ANAZITAMBUA GOLI ZA LEO TU 3 GOLI MOJA LA HUKU KAFUTA.
Mweeer, ifike mahali tukipangiwa na jamaa tuwaachie tuu maana haya ni matumiz mabaya ya pesa, muda na rasilimali nyngne
 
Unajua tatizo tumeishaijenga hali hii kisaikolojia,yaani hata media zetu zimekomalia hilo.
Sasa unakuta kwamba wachezaji wakienda Nchi hizo tayari wanakuwa wameishafungwa kabla ya mpira kuanza,na hilo utalioan leo jinsi Azam walivyokuwa wanacheza,na Waarabu pia wanafuatilia vyombo vya habai na record na kugundua kwamba wanaogopwa.

Halafu unafiki wetu utaona eti magazeti yanaandika AZAM yatu Jijini Tunis yawa Gumzo,jiji zima latikisika kwa kuigopa AZAM,kocha anatetemeka kwa kuogopa AZAM,mbwembwe nyingiiiii,hovyo kabisa,haya wekeni heading zenu mbili na za kesho muone mlivyo wanafiki.
 
Jamaa wa suti washapigwa. Walifikiri wanacheza na mgambo. Kushabikia timu za Tanzania ni kukaribisha magonjwa ya moyo. TAKUKURU ingieni jikoni kwa TFF,tunahitaji mabingwa wa kweli ligi ya ndani. Haiwezekani tuache usingizi,tuchapwe kama watoto
 
Kesho sijui vyura watachezea ngapi,maana nao mhhh! Nitakuwa kwa waarabu,nipunguze maumivu.
 
Yanga ndio naihurumia zaidi,Ila wacha wafungwe maana hamna namna sasa,Si wanabebwa tu hapa!
 
Siyo mbaya ndo mpira ulivyo huwa sishangai saana, nafikir wachezaj wamelack confidence muhimu kujipanga upya na kujua umuhimu wa mechi za nyumbani.
 
TV Nationale 2 Tunisie tazama live Wataniya 2 live online | Tunisie 14

Dakika ya 22'' Yallah! Yallah! huyu Coulibaly wa Esperance hatari sana !
Dakika ta 23'' Krosi ya Esperance inangonga mtambaa wa juu wa goli la Azam!
Dakika 25'' Jamaa wanaweka pressure kubwa kwa Azam FC lakini wachezaji wa Azam FC wametulia hawababaiki
Dakika 29'' Manula anadaka shuti kali la shambulizi la Esperance
Dakika 31'' Hawa jamaa Esperance wanacheza kwa kukamia mpira upo half ya pitch ubabe wa Azam FC tu
Dakika 44'' Hongera kwa wachezaji wa Azam FC hasa safu ya ulinzi pamoja na kipa Aishi Manula ni jihadi kwenda mbele Esperance hawaamini wanayoona!
Dakika 45'' shuti! Aishi Manula anaokoa inakuwa kona
Dakika 45 + 1 Mpira ni mapumziko

DakiKa ya 49 '' Goal! Adhabu ndogo goli kwa Azam FC na ni Goal! Esperance wanafunga goli kupitia Bguir lakini naona kabla ya adhabu kupigwa watazamaji wanafanya faulo/ hujuma kwa kummulika machoni Kipa Manula na ''Laser beam/ light'' kupunguza umakini wake wa kuona na Esperance wanafunga goli.
Dakika ya 57'' Esperance wameamua kuwa na kumiliki mpira (total ball possession)kulinda goli lao moja na kuafanya mashambulizi ya kuvizia.
Dakika ya 60'' Espereance wanapata kona na Aishi Manual anaokoa.
Dakika ya 64'' Goal Jouini anaipatia Esperance goli la pili
Dakika ya 81'' Goal ! Youssef anaifungia Esperance Sportive De Tunis bao la tatu
Mpira umekwisha
Esperance 3 - Azam FC 0

Uchambuzi wa matatizo timu za Tanzania michuano ya kimataifa

Timu za Tanzania vinazoongoza ktk nafasi tano za juu ktk msimamo wa ligi VPL inabidi kuwa na uwezo wa kufunga mabao 4 mpaka 5 kila mara katika ligi ya nyumbani.

Timu bora nne za ligi VPL_Tanzani zikiweza kufunga mabao mengi basi wanajijengea uchu/uzoefu/umakini wa kufunga mabao kama hayo (4-5)wakija katika ngazi ya michuano ya kimataifa kwa sababu ukiangalia ligi yetu ya VPL timu nyingi ''bora'' zina uwezo wa kufunga wastani (average) wa mabao mawili tu.

Sat 09/04/16 African Sports 1 - 0 Kagera Sugar More info
Ndanda 2 - 1 Mwadui More info
Sun 10/04/16 JKT Mgambo 0 - 1 Mbeya City More info
Mon 11/04/16 Toto Africans 1 - 2 Maji Maji More info
Wed 13/04/16 Mtibwa Sugar 0 - 1 Azam More info
Young Africans 2 - 1 Mwadui More info
Sat 16/04/16 Coastal Union 1 - 0 Ruvu Stars More info
Ndanda 2 - 0 Kagera Sugar More info
Young Africans 1 - 0 Mtibwa Sugar More info
Sun 17/04/16 Simba 0 - 1 Toto Africans
 
April 20, 2016

By ppkahemele on April 20, 2016

Changamoto za AZAM FC mashindano ya nyumbani FA Cup, VPL

Kocha Stewart Hall amesema kabla ya mazoezi ya Azam FC ufukweni Hoteli waliyofikia ya El Mouradi Gammarth, Tunisia , wachezaji wake wasahau yaliyopita ya kutolewa katika mashindano ya kimataifa ya CAF Confederation Cup na sasa wafikirie mechi zao nane zilizobakia katika Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) na Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) ili kufanya vizuri.


Azam FC inayodhaminiwa na Benki ya NMB, Jumapili ijayo Aprili 24 itakuwa na mchezo mgumu wa nusu fainali ya FA Cup watakaocheza ugenini dhidi ya Mwadui ya mkoani Shinyanga kabla ya siku tatu baadaye (Aprili 27) kukipiga na Majimaji katika mechi ya ligi itakayofanyika Uwanja wa Azam Complex.

“Nimewaambia lazima tujipange vema kwa michuano miwili hiyo tuliyobakiwa nayo, kwa sababu tunataka kujaribu kushinda makombe yote hayo tuliyobakiwa nayo jambo ambalo tunaweza, tmebakiwa na mechi nane hivyo tunatakiwa kuhakikisha tunashinda mechi zote, jambo zuri zaidi Kipre, Wawa, Migi wanarejea kikosini, bado tutaendelea kuwa bila Kapombe, hivyo kama una wachezaji watatu wanarejea na wachezaji wengine wako fiti kikosi kinarejea kuwa na nguvu yake,” alisema. Source: Hall: Tumetolewa na timu bora Afrika | The Official Website of Azam Football Club
 
April 24, 2016
Mwadui

By ppkahemele

Match Pre-view FA Cup : Mwadui FC vs Azam FC

LEO ndio leo ndani ya Uwanja wa Mwadui, mjini Shinyanga, ambapo utashuhudiwa mchezo wa nusu fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) kwa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC kuvaana na wenyeji wao Mwadui FC saa 10.00 jioni.

Tunataka kuingia fainali

Akizungumzia mchezo huo, Kocha Mkuu wa Azam FC, Stewart Hall, alisema kuwa mchezo huo ni muhimu sana kwao kwani ikizingatiwa wanataka kuingia fainali ya michuano hiyo.

“Kiukweli mchezo huo ni muhimu sana kwetu, tunataka kuingia fainali, jambo la kwanza tunataka kurudisha ari za wachezaji vizuri mara baada ya matokeo mabaya tuliyopata Tunisia, tunatakiwa kuondoa hilo akilini mwa wachezaji na kuwafikirisha zaidi umuhimu wa mchezo huo, huwezi kubadilisha jambo lililotokea bali unatakiwa kuangalia mbele ili kufanya vizuri.

“Kwa sasa tuna wachezaji sita wanaoumwa kidogo kutokana na uchovu, tutajua hali zao zinaendeleaje kikao cha mwisho kesho (leo) kabla mchezo huo, hatuna majeruhi wapya, tunashukuru Migi na Himid wanarejea kikosini ambao wako vizuri kiafya, Vialli (Khamis Mcha) naye yupo vizuri,” alisema.

Hata hivyo kwenye mazoezi ya mwisho ya Azam FC yaliyofanyika Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza jana jioni, wachezaji wa timu hiyo walionekana kucheza kwa bidii hasa baada ya kutambua ya kuwa mchezo huo una umuhimu mkubwa sana kwao kama wataibuka na ushindi.

Hall alisema kuwa mchezo huo utakuwa mgumu sana kutokana na aina ya timu wanayoenda kukutana akikumbushia namna walivyoonyeshwa upinzani mkali katika mechi mbili zilizopita walizokutana nao kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL).

Bingwa wa FA Cup

Baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kurudisha michuano hiyo tena msimu huu, sasa bingwa wa michuano hiyo ataiwakilisha Tanzania Bara katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika mwakani (CC) badala ya mshindi wa pili wa ligi iliyokuwa ikitumika kwa takribani miaka 14 iliyopita mashindano hayo yalipokufa.

Hivyo kama Azam FC ikitwaa ubingwa huo itakuwa imejihakikishia nafasi ya kushiriki michuano hiyo ya pili kwa ngazi ya vilabu barani Afrika.

Kama ikitokea Azam FC ikitwaa ubingwa huo FA pamoja na taji la ligi VPL basi hiyo itamaanisha ya kuwa itashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani na aiyeshika nafasi ya pili kwenye FA Cup atashiriki Kombe la Shirikisho.
Source: MATCH PREVIEW: Mwadui vs Azam FC | The Official Website of Azam Football Club
 
Apri 24, 2016
Mwadui
FA Cup : matokeo Mwadui FC 5 - Azam FC 7

Dakika 90 " Zakamilika Mwadui FC 1 - Azam FC 1
Dakika 120" zikikamilika: Mwadui 2 - Azam FC 2

Penalti mikwaju mitano zinafuatia : Mwadui FC 3 - Azam FC 5

Jumla ya matokeo : Mwadui FC 5 - Azam FC 7.

wafungaji Azam FC ndani ya dakika 120 ni Mcha Khamis 'Vialli' dakika za 2" na dakika 97".
Wafungaji wa penalti tano za Azam FC : John Bocco, Himid Mao, Allan Wanga, Waziri Salum na Aggrey Morris.

Kwa matokeo hayo ya mchezo huo wa nusu fainali ya FA Cup Mwadui FC 5 - Azam FC 7 , timu ya Azam imetinga fainali ya FA Cup.
 
April 27, 2016
Dar-es-Salaam

Azam yapaa mpaka nafasi ya pili ligi ya VPL : Azam FC 2 - Maji Maji 0

Baada ya ushindi mnono wa mechi ya kiporo baina ya Azam FC vs Maji Maji , Azam imepanda mpaka nafasi ya pili ya msimamo wa ligi ya VPL Tanzania nyuma ya Young Africans (Yanga).

Mabao ya Azam FC yalifungwa na Mudathir Yahya katika dakika za 51" na 63" na Azam kujikusanyia jumla ya pointi 58. Wakati Yanga wana pointi 62 huku Simba SC wakiwa na pointi 57. Timu zote za Azam , Yanga na Simba sasa zimecheza michezo 25 ya ligi hiyo ya VPL Tanzania.
 

Safi sana Azam tuko pamoja
 
May 4, 2016

Matokeo Ligi Vodacom VPL : Azam FC 2 - JKT RUVU 2

Mabao ya Azam FC yalifungwa na pacha kutoka Ivory Coast, kiungo Kipre Michael Balou dakika ya 31 na mshambuliaji Kipre Herman Tchetche dakika ya 37.

Wakati mabao ya JKT RUVU inayofundishwa na Kocha Abdallah Kibadeni 'King' yalifungwa na Saad Kipanga kwa mkwaju wa penalti dakika ya 56 kabla ya Najim Magulu kufunga la pili dakika ya 72.

Kwa matokeo hayo Azam FC imejiongezea pointi moja na kufikisha 60 baada ya kucheza mechi 27 na inaweza kumaliza na pointi 69 ikishinda mechi tatu za mwisho.

Matokeo hayo ya Azam FC yameipa Young Africans (Yanga) nafasi ya kutetea taji lao Mei 10 kama Yanga wataishinda timu ya Mbeya City Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, kwani Yanga watafikisha pointi 71 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine ya Ligi Kuu .
 
July 5, 2016
Dar-es-Salaam, Tanzania

By Abducado Emmanuel

Kipa Mhispania atua kujaribiwa Azam FC

KIPA raia wa Hispania, Juan Jesus Gonzalez, ametua nchini jana mchana, tayari kabisa kufanya majaribio ya kujiunga na Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC.

Ujio wa kipa huyo unatokana na benchi jipya la ufundi la Azam FC chini ya Zeben Hernandez, ambalo linataka kuongeza nguvu kwenye eneo la langoni ili kutengeneza safu bora ya ulinzi na ushindani wa namba katika nafasi hiyo.

Gonzalez mwenye umbo la urefu aliyepokelewa na Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffar Idd, ataanza rasmi majaribio yake mara baada ya kikosi cha Azam FC kuanza mazoezi ya maandalizi ya msimu mpya (2016-17) kati ya kesho Jumatano au Alhamisi.


Akizungumza na mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz juu ya ujio wake, Zeben alisema kwa ufupi kuwa eneo la langoni ni sehemu muhimu sana ambalo amepanga kuliongezea nguvu zaidi.

“Nimefurahi sana kufanikiwa kwake kutua hapa, namjua Gonzalez ni kipa mzuri na hili ni jambo muhimu sana kwa Azam FC katika kuboresha eneo hilo, atakuwa hapa kwa majaribio akifanya vizuri tutamchukua,” alisema.

Hii ni mara ya pili kwa Azam FC kumleta kipa toka nchi ya ulaya ndani ya kikosi chake, mwaka 2011 iliwahi kumnasa kipa kutoka nchini Serbia, Obren Cirkovic, ambaye alianza kuwika akiwa na timu ya Yanga.

Pia kuna wachezaji kadhaa waliokuja kwenye majaribio kama Juan Jesus Gonzalez toka nchi za kiafrika wakiwemo makipa Daniel Yeboah (Ivory Coast) na Nurdin Yusuf (Medeama, Ghana).
Source: Kipa Mhispania atua kujaribiwa Azam FC | The Official Website of Azam Football Club
 
July 5, 2016
Dar-es-Salaam, Tanzania

By Abducado Emmanuel

Makocha wapya watua kuanza kazi Azam FC

MAKOCHA wapya wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC kutoka nchini Hispania, wametua rasmi jijini Dar es Salaam leo saa 9 Alasiri tayari kabisa kuanza maandalizi ya msimu ujao (2016-17).

Wakufunzi hao waliotua leo na kupokelewa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba, pamoja na Ofisa Habari Jaffar Idd, ni Kocha Mkuu Zeben Hernandez na Msaidizi wake Yeray Romero, Kocha Mkuu wa Viungo Jonas Garcia na Msaidizi wake, Pablo Borges na Kocha wa Makipa Jose Garcia.



Jopo hilo la makocha litaongezewa nguvu na makocha wengine wazawa waliokuwa na Azam FC msimu uliopita, Kocha Msaidizi Dennis Kitambi na wa Makipa, Idd Abubakar.

Akizungumza na mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz mara baada ya kutua kwa mara ya pili nchini Kocha Mkuu Zeben, alisema wamekuja kuanza rasmi kazi kuanzia Jumatatu Ijayo (Julai 4, 2016) kwenye Makao Makuu ya Azam Complex, Chamazi katika viunga vya Jiji la Dar-es-Salaam.

Kocha huyo wa zamani wa CD Santa Ursula ya Hispania, alisema kuwa kabla ya kuanza kazi rasmi Jumatatu, kesho Jumapili wanatarajia kukutana na uongozi wa Azam FC pamoja na kutembelea makao makuu ya Azam Complex.

Daktari kutua Julai 12

Katika hatua nyingine alisema kuwa Daktari wa timu hiyo, Sergio Perez, anatarajia kutua nchini Julai 12 mwaka huu, na hawakuweza kutua naye leo kutokana na kumalizia baadhi ya mambo na timu yake anayofanya kazi kwa sasa.

Tayari Zeben ameshaweka wazi kuwa jambo kubwa analokuja kulifanya Azam FC ni kuifanya timu hiyo ipate matokeo mazuri na kutisha barani Afrika ikiwa inacheza soka safi la kisasa lenye muoanekano wa Kihispania.

C.E.O afafanua ujio wao

Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba, alisema kuwa makocha hao wanatarajia kuanza programu yao wiki ijayo huku kesho (Jumapili) wakitarajia kufanya nao kikao kwa ajili ya kujipanga na msimu ujao.

“Tunamshukuru Mwenyezi Mungu baada ya makocha wetu kufika salama, kama tulivyopanga kesho watakuwa na kikao na uongozi, baada ya hapo wataanza rasmi programu yao Jumatatu na hapo ndipo tutakuwa tunaanza maandalizi ya msimu ujao,” alisema.
Source: Makocha wapya watua kuanza kazi Azam FC | The Official Website of Azam Football Club
 
July 6, 2016
Dar-es-Salaam, Tanzania

By Abducado Emmanuel

KIPA timu ya Taifa ya Ivory Coast, Daniel T. Yeboah, kujaribiwa Azam FC.

KIPA wa zamani wa timu ya Taifa ya Ivory Coast, Daniel Techi Yeboah, ametua nchini jana jioni tayari kabisa kuanza majaribio kesho ya kujiunga na mabingwa wa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA Kagame Cup), Azam FC.

Yeboah mwenye umbo kubwa la kimpira na urefu wa wastani anaungana na kipa kutoka Hispania, Juan Jesus Gonzalez, ambao wote wataanza kujaribiwa katika mazoezi ya Azam FC ya kujiandaa na msimu ujao yatakayoanza rasmi kesho Alhamisi saa 2.30 asubuhi.

Kipa huyo aliyekuwa akikipiga katika timu ya KSV Oostkamp ya Ubelgiji, amewahi pia kukipiga nchini Ufaransa ndani ya vikosi vya Bastia na Dijon huku akianzia soka lake kwa miamba ya Ivory Coast, Asec Mimosa’s.

Wakati akiwa Mimosas, aliwahi kuwa nahodha wa beki kisiki wa kati wa Azam FC, Pascal Wawa kabla ya beki huyo kutimkia kwa miamba ya Sudan, El Merreikh, pia amewahi kufanya kazi na kipa wa Simba, Vincent Angban, ambaye alifanikiwa kumweka benchi na kisha kutimkia Ufaransa.

Yeboah pia amewahi kuchezea kikosi cha timu ya Taifa ya Ivory Coast kilichoshiriki Kombe la Dunia Afrika Kusini mwaka 2010 na fainali za Mataifa ya Afrika 2013 nchini humo, kilichoundwa na mastaa wengine kama vile Didier Drogba, Didier Zokora, Kolo Toure, Yaya Toure, Solomon Kalou, Aruna Dindane, Emmanuel Eboue.

Akizunguma kwa ufupi na mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz wakati akiwasili nchini jana na kupokelewa na Meneja wa Azam FC, Luckson Kakolaki, Yeboah alisema kuwa amekuja akiwa na fiti na kazi yake ni moja tu kuhakikisha anashinda changamoto zote na kusajiliwa na timu hiyo.

“Kwanza siku zote mimi huwa napenda sana upinzani na nimekuja hapa nikiwa kamili kukaniliana na hilo, mashabiki watafurahi wenyewe nikifanikiwa kubaki hapa,” alisema.

Baadhi ya dondoo za kiwango chake, ni uwezo wake mkubwa wa kuzuia michomo, kuusoma mchezo pamoja na mawasiliano mazuri na walinzi wake akiwa langoni, ambapo kutokana na kipaji chake cha hali ya juu aliwahi kufananishwa na gwiji wa zamani wa Ivory Coast, Alain Gouamene.

Source: Kipa Ivory Coast aja kujaribiwa Azam FC | The Official Website of Azam Football Club
 
July 11, 2016
Dar-es-Salaam, Tanzania

By Abducado Emmanuel
Sita watemwa rasmi Azam FC, wawili wafeli majaribio
UONGOZI wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, umetangaza rasmi kuwatema wachezaji nyota sita kwa awamu ya kwanza huku wengine wawili wakifeli majaribio.

Nyota sita walioachwa ni makipa Ivo Mapunda, Khalid Mahadhi aliyekuwa ametolewa kwa mkopo Mafunzo ya Zanzibar, mabeki Said Morad, Racine Diouf kutoka Senegal pamoja na washambuliaji Didier Kavumbagu (Burundi) na Allan Wanga (Kenya).

Cuts za wachezaji waliofeli majaribio Azam FC
Source: Azam Football Club

Akizungumza na mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffar Idd, alisema wachezaji hao wameachwa wakiwa wamepata stahiki zao kwa wale ambao waliokuwa wamebakiwa na mikataba.

Alisema mbali na wachezaji hao, pia wachezaji wawili kati ya wanne waliokuwa kwenye majaribio nao wameachwa rasmi ambao ni beki wa kushoto kutoka Ghana, Nurudeen Yusif aliyetokea Medeama ya huko na kiungo mshambuliaji David Wirikom (Cameroon).

Wawili hao wamepewa majibu ya kufeli majaribio yao leo asubuhi kufuatia Kocha Mkuu Zeben Hernandez, kutoridhishwa na uwezo wao kwa siku nne walizofanya mazoezi na kikosi cha Azam FC.

Wachezaji wanaoendelea kwenye majaribio ni makipa Daniel Yeboah (Ivory Coast) na Juan Jesus Gonzalez (Hispania), ambao wanawania nafasi moja ya usajili katika eneo la golikipa.

Jaffar alimalizia kwa kusema kuwa wanatarajia kuwapokea wachezaji wengine wa kimataifa ndani ya siku mbili au tatu zijazo kwa ajili ya majaribio yote ni katika kuendelea.
Source: Sita watemwa rasmi Azam FC, wawili wafeli majaribio | The Official Website of Azam Football Club
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…