23 December 2020
Dar es Salaam, Tanzania
Mshambuliaji "Platini" Mpiana Mozinzi atua Azam Fc kupitia usajili wa dirisha dogo.
Timu ya Chamazi jijini Dar es Salaam imefanikiwa 22 December 2020 kumsajili mchezaji hatari Mpiana Mozinzi kutoka timu iliyopo Lubumbashi Congo DR ya FC Lupopo, imethibitishwa na uongozi wa timu ya Azam FC ya Tanzania.
Video Source : FC Saint Eloi Lupopo Officiel
Video hiyo juu inaonesha makali ya mchezaji huyo akiwa uwanjani na inategemewa ataendeleza makali ya ktk Ligi Kuu ya Tanzania na kuisaidia Azam FC kunyakua tena kombe la Ligi Kuu ya Tanzania.
Mchezaji huyo wa FC Lupopo , Mpiana Mozinzi amekuwa ktk radar za maskauti wa kusaka wachezaji bora Afrika ili aweze kushawishiwa kujiunga na timu mpya. Timu hizo kubwa zilizokuwa zinammezea mate ni pamoja na Orlando Pirates ya South Africa, Zamalek ya Egypt, Young Africans na Simba SC za Tanzania kabla ya Azam FC kufanikiwa kumdaka.