The Official Azam FC Thread

The Official Azam FC Thread

1. MWADINI ALI
2. SHOMARI KAPOMBE
3. GADIEL MICHAEL
4. DAVID MWANTIKA
5. AGGREY MORIS
6. BOLOU MICHAEL
7. HIMIDI MAO
8. SALUM ABUBAKAR
9. JOHN BOCCO
10 KIPRE TCHETCHE
11. KHAMISI MCHA

AKIBA
AISHI MANULA
MUDATHIR YAHYA
SAID MORAD
ABDALLAH KHERI
FARID MUSSA
DIDIER KAVUMBAGU

come on azam fc...
 
Kagame on the move 6 pm today cone on lambalamba..
 
Azam fc wanahitaji kufanya marekebisho:upigaji pasi za uhakika,kasi ya mchezo na upigaji wa mashuti golini,wachezaji waongeze stamina bila hayo itakuwa ngumu kwenye mashindano wanayoshiriki !
 
Azam FC yaichapa 4-1 Adama City Kombe la Kagame


Submitted by ppkahemele on Sat, 2014-08-16 18:17
IMG_9677.JPG



AZAM FC imemaliza kwa ushindi mnono mechi za makundi, Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame baada ya kuifumua mabao 4-1 Adama City ya Ethiopia.

Kwa matokeo hayo Azam FC ya Tanzania Bara, imepanda kileleni mwa Kundi A kwa kufikisha pointi nane baada ya mechi nne, ikishinda mbili na sare mbili- hivyo kutinga Robo Fainali kibabe.

Rayon Sport ambayo hivi sasa inacheza na Atlabara ya Sudan Kusini, inaweza kupanda kileleni mwa kundi hilo iwapo itashinda.
Dakika 45 za kwanza zilimalizika timu hizo zikiwa zimefungana bao 1-1, Azam wakitangulia kupitia kwa Nahodha John Bocco ‘Adebayor' akiunganisha krosi ya Khamis Mcha ‘Vialli' kabla ya Desaleny Debesh kuisawazishia Adama dakika ya 39.

Refa Mohamed Hassan kutoka Somalia alikataa bao la Kipre Herman Tchetche dakika ya 42, akidai kipa alibughudhiwa na kipindi cha pili Azam iliingia na moto mkali na kufanikiwa kuongeza mabao matatu.

Alianza Didier Kavumbangu dakika ya 55, akimalizia krosi ya Erasto Nyoni akafuatia Khamis Mcha ‘Vialli' dakika ya 60 baada ya kuuwahi mpira uliotemwa na kipa na Kipre Tchetche akamalizia dakika ya 74, krosi ya Nyoni.

Kocha Mcameroon Joseph Marous Omog alifurahia matokeo hayo na akasema sasa anajipanga kwa Robo Fainali. "Ushindi huu ni mzuri, nafurahi tunaingia Robo Fainali kwa kujiamini, sasa tunaelekeza nguvu zetu huko,"alisema.

Source: http://www.supersport.com/football/cecafa-cup/news/140816/Azam_thrash_Adama_City http://www.azamfc.co.tz/content/azam-fc-kucheza-na-el-merreikh-robo-fainali-kagame
 
Lionel na Kapombe wote tayari kuivaa Merreikh kesho Kagame


Submitted by ppkahemele on Tue, 2014-08-19 11:43
AZAM%20WEB.JPG



BEKI Shomary Kapombe na mshambuliaji Lionel Saint- Preux kutoka Haiti wote wamefanya mazoezi kikamilifu jana na leo kuelekea mchezo wa kesho wa Robo Fainali Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame Azam FC ikimenyana na El Marreikh ya Sudan, Uwanja wa Nyamirambo, Kigali, Rwanda.



Wawili hao waliokuwa wanasumbuliwa na maumivu ya nyama za paja, walikoa mchezo wa mwisho wa Kundi A dhidi ya Adama City ya Ethiopia, Azam FC ikishinda 4-1.



Na katika mazoezi ya leo asubuhi Uwanja wa Kiyovu, Nyamirambo mjini hapa, kocha Mcameroon Joseph Marious Omog ameonekana kuwahusisha nyota hao katika kikosi kitakachoanza kesho.



Majeruhi mwingine, beki Waziri Salum pia amefanya mazoezi wakati kiungo Himid Mao anatarajiwa kurudi pia baada ya kukosa mchezo dhidi ya Adama kwa sababu ya kadi za njano.



Omog amekuwa akiandaa Azam FC kitaalamu mno kuelekea mchezo huo, akiwaelekeza mifumo na aina tofauti ya uchezaji, ikiwa ni pamoja na kutumia mipira mirefu na mifupi.



Amekuwa akiwandaa pia kwa kupiga penalti, kwa kuwa iwapo mchezo huo utamalizika kwa sare, matuta yataamua timu ya kusonga Nusu Fainali.



Kwa ujumla Azam ambayo imewekwa hoteli moja na wapinzani wao hao, Merreikh, Kigali View eneo la Nyamirambo, ipo vizuri kuelekea mchezo huo, ambao unasubiriwa kwa hamu na Watanzania wengi.


Robo Fainali za Kagame zinaanza leo, mchezo wa kwanza ukiwa kati ya Polisi ya hapa dhidi ya Atleitco ya Burundi, kabla ya Rayon Sport kumenyana na APR, zote za hapa leo, wakati mbali na Azam na Merreikh, mchezo mwingine wa kesho utakuwa kati ya KCC ya Uganda na Atlabara ya Sudan Kusini.
Source: http://www.supersport.com/football/cecafa-cup/news/140816/Azam_thrash_Adama_City Leonel na Kapombe wote tayari kuivaa Merreikh kesho Kagame | The Official Website of Azam Football Club
 
Back
Top Bottom