The Official Azam FC Thread

The Official Azam FC Thread


Kipre Tchetche wa Azam Fc (juu) akiruka kwanja la beki wa timu ya
Barrack Young Controller, wakati wa mchezo wa timu hizo wa
marudiano Kombe la
Shirikisho, ulichezwa leo jioni kwenye Uwanja wa
Taifa
jijini Dar Es Salaam April 6, 2013. Katika mchezo huo timu hizo zimetoka sare
bila kufungana na
kuifanya Azam izidi kusonga


John Boko (kulia) akichuana na beki wa Barrack Young jijini Dar-es-Salaam, April 6, 2013

Picha zote kwa hisani ya Sufianimafoto wa SUFIANIMAFOTO
 
Hongera sana Azam fc,mmetutoa kimasomaso,kazeni butu muwatoe na hao FAR.Watanzania tupo nyuma yenu,yes you can!
 
AZAM WABANWA KUKUTANA NA WAMOROCO

Wawakilishi wa Tanzaniaa Azam fc leo wamelazimishwa sare na baqack yc ii mchezo wa kombe la shirikisho uliochezwa katika uwanja wa taifa sasa watawakabi AS FAR ya Moroco april 22 mwaka huu. Katika mchezo huo wa leo Barack YC II waliweza kuwadhibiti viungo wa azam fc katika kipindi cha kwanza kitendo kilichopelekea washambuliaji wa azam kukosa mipira ya uhakika katika kipindi cha kwanza huku mchezo ukitawala kwa kupokezana.

Katika kipindi cha kwanza kipa wa azam fc Mwadini Ally hakudaka mpira wowote wa maana huku kipa wa Barack YC akiwa na kazi ya ziada ya kuokoa hatari 3 kati ya nafasi 4 walizopoteza azam fc katika kipindi cha kwan9a kupitia kwa Mieno na Kipre Tchetche. Mshambuliaji toka Uganda Brian Umonyi leo alishindwa kuonyesha cheche zake na katika kipindi cha pili alipumzishwa na nafasi kuchukuliwa na Khamisi Mcha Viali. Katika kipindi hicho cha pili mchezo uliendelea kutawaliwa kwa zamu na safari hii Barack walifanikiwa kufika langoni mwa azam na kushindwa kutia mpira kimiani.

Kipre Bolou amanusura aipatia goli azam fc baada ya kuvunja mtego wa kuotea na kubaki na kipa ila mpira alioupiga ulipaa juu ya lang6. Azam fc walizidi kutengeneza nafasi za magoli lakini wakishindwa kuzitumia nafasi hizo, huku wakishindwa kupiga pasi nyingi kama walivyozoeleka, na mwisho wa mchezo azam fc 0-0 barack yc.

Azam wamewatoa Barack yc kwa jumla ya goli 2-1 waliyoyapata katika mchezo wa awali, huku AS FAR wanayokutana nayo katika hatua ya pili wakiwatoa Al nasri ya Libya kwa jumala ya goli 2-1.

Azam fc leo(Jana): MWADINI ALLY, HIMID MAO, WAZIRI SALUM, JACKSON ATUDO, DAVID MWANTIKA, MICHAEL BOLOU, KIPRE TCHETCHE, SALUM ABOUBAKARY, JOHN BOCCO, HUMPHREY MIENO/ABDALLAH SEIF NA BRIAN UMONYI/ KHAMISI MCHA.
 
Hongera sana Azam fc,mmetutoa kimasomaso,kazeni butu muwatoe na hao FAR.Watanzania tupo nyuma yenu,yes you can!

thanks sana mkuu pamoja we can make it nikupambana tu ndio mpira.. Forza azam fc
 
hongereni Azam, manaake hii mitimu mingine imekalia kulogana na kupinduana.!!
 
hongereni Azam, manaake hii mitimu mingine imekalia kulogana na kupinduana.!!

Mkuu,
Kweli Mkuu ngoja Azam FC ichanje mbuga na kuwatoa katika mashindano hawa AS FAR Morocco maana Taifa Stars ilishaonyesha kuwa pamoja na timu ya taifa ya Morocco kuwa na wachezaji wengi wa kulipwa ulaya walilimwa bao 3 kwa 1.

Hivyo dua za timu 'kongwe' kuwa Azam FC itakwaa kisiki cha timu ya waarabu wa Maghreb yaani AS RAF Morocco hazitatimia.
 
563981_317493605046359_1285431244_n.png



L'équipe nationale de Tanzanie qui a joué contre le Maroc comporte 7 joueurs du club Azam FC.

سبعة لاعبين من فريق آزام كانوا ضمن المنتخب التنزاني الذي لعب ضد المنتخب المغربي.ـ

hii imetoka kwa fans page ya mashabiki wa AS Far
 
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA

S. L.P. 42325,
Temeke,
Simu: 022 2850633,
Nukushi: (022) 2850635, Baruapepe:rbctemeke@pccb.go.tz,
Mtandao Home

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI - UCHUNGUZI WA WACHEZAJI WA TFF

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) inatoa taarifa kwa umma kwamba, uchunguzi uliofanywa na TAKUKURU Mkoa wa Temeke dhidi ya wachezaji wanne wa timu ya soka ya AZAM waliokuwa wakituhumiwa kupokea hongo/ rushwa ili kupanga matokeo, haukuweza kuthibitisha tuhuma hiyo. Kosa la kupokea rushwa ni kinyume na Kifungu cha 15(1) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya mwaka 2007.

Kwa mujibu wa kifungu hicho ni kosa kwa mtu yoyote kuomba, kupokea, kushawishi au kulazamisha kupewa rushwa au kuahidi kutoa rushwa. Wachezaji waliokuwa wakilalamikiwa ni (1) DEOGRATIUS BONIVENTURE MUSHI (DIDA), (2) ERASTO NYONI,
(3) SAID HUSSEIN MORAD na
(4) AGGREY MORRIS.

Wachezaji hawa kwa pamoja walituhumiwa kupokea rushwa kwa lengo la kupanga matokeo ya mechi kati ya AZAM FC na SIMBA SPORTS CLUB iliyochezwa tarehe 27/10/2012 katika Uwanja wa Taifa – jijini Dar es salaam. Katika mechi hiyo AZAM FC ilifungwa magoli 3 - 1. Tuhuma hizo ziliwasilishwa TAKUKURU Mkoa wa Temeke tarehe 9/11/2012 kutoka AZAM FC ikiwatuhumu wachezaji hao kupokea kiasi cha shilingi milioni saba (7,000,000/=) kutoka kwa uongozi wa Simba Sports Club ili wagawane na kupanga matokeo ya mechi. Fedha hizo zilidaiwa kupokelewa siku moja kabla ya mechi kati ya AZAM FC na SIMBA SC (tarehe 26/10/2012).

AZAM FC, imeweza kutimiza wajibu wake wa kushiriki katika kuzuia na kupambana na rushwa kwa kutoa taarifa za tuhuma za rushwa kwa TAKUKURU – chombo ambacho ndicho chenye dhamana na mamlaka ya kisheria kuchunguza makosa ya rushwa. Tunatoa wito kwa taasisi nyingine na wananchi kwa ujumla, kuendelea kutoa taarifa za tuhuma za rushwa kwa TAKUKURU ili kwa pamoja tuweze kudhibiti vitendo vya raushwa katika nchi yetu

Imetolewa na Doreen J. Kapwani - Afisa Uhusiano wa TAKUKURU,
Jumatatu tarehe 08/04/2013

Home
 
Timu kongwe nao waige mfano wa Azam FC kutoa taarifa TAKUKURU kama kuna ka-harufu ka-rushwa na siyo kupanga mapinduzi haramu au maandamano dhini ya viongozi wa klabu na kusababisha soka la Tanzania kuyumba.
 
April 8, 2013
Dar-es-Salaam, Tanzania

Mechi Sita Kuonekana SuperSport ‘Live' Super Week Monday, 08 April 2013 14:22 admin



Kituo cha televisheni cha SuperSport cha Afrika Kusini kitaonesha moja kwa moja mechi sita za Ligi Kuu ya Vodacom katika Super Week kati ya Aprili 11 na Mei 18 mwaka huu.

Mechi hizo ni kati Azam na African Lyon itakayochezwa Aprili 11 mwaka huu badala ya Aprili 10 mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam. Yanga na Oljoro JKT ambayo sasa itachezwa Aprili 13 mwaka huu badala ya Aprili 10 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Azam na Simba itakayochezwa Aprili 14 mwaka huu badala ya Aprili 13 mwaka huu Uwanja wa Taifa, na mechi kati ya Coastal Union na JKT Ruvu itakayochezwa Aprili 16 mwaka huu badala ya Aprili 10 mwaka huu.

Mechi nyingine ya Super Week itakayochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga ni kati ya Mgambo Shooting na Yanga itakayofanyika Aprili 17 mwaka huu badala ya Aprili 13 mwaka huu.

Pia mechi nyingine itakayooneshwa live na SuperSport ni kati ya Yanga na Simba itakayofanyika Mei 18 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kutokana na mechi za Super Week, mechi kati ya Mtibwa Sugar na Oljoro JKT iliyokuwa ichezwe Aprili 13 mwaka huu sasa itachezwa Aprili 17 mwaka huu Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.

Source: News
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

UCHUNGUZI WA TAKUKURU DHIDI YA TUHUMA ZA RUSHWA KWA WACHEZAJI WANNE (4) WA AZAM FC

AZAM FC inatoa taarifa rasmi kuwa TAKUKURU haijawakuta na hatia ya rushwa wachezaji; DEOGRATIUS BONIVENTURE MUNISHI,
ERASTO NYONI,
SAID HUSSEIN MORAD NA
AGREY MORRIS.

Hivyo wachezaji hao wanakaribishwa rasmi kurudi kikosini AZAM FC kwa ajili ya kujiunga na mazoezi na wachezaji wenzao. Tunatanguliza shukrani

Imetolewa.na NASSOR IDRISSA- KATIBU MKUU wa AZAM FC. Jumanne 9/4/2013
 
Kikosi cha leo dhidi ya African Lyon.
1. Aishi Salum
2. Himidi Mao
3. Waziri Salum
4. Jockins Atudo
5. Luckson Kakolaki
6. Jabir Aziz
7. Kipre tchetche
8. Ibrahim Mwaipopo
9. Abdi Kassim
10. Salum Abubakar (C)
11. Mcha Khamisi

Akiba
Mwadini Ali
Humphrey Mieno
Seif Karihe
Malika Ndeule
Gaudence Mwaikimba
Omari Mtaki
Brian Umony
 
Kipindi cha pili kimeanza

Azam fc 2 - 1 A lyon
 
Back
Top Bottom