The Official Azam FC Thread

The Official Azam FC Thread

Wachezaji wote wanne waliosimamishwa kupisha uchunguzi wa tuhuma za rushwa dhidi yao wameripoti kambini tayari kuikabili Simba SC siku ya jumapili

Aggrey Morris na Erasto Nyoni wakifuatilia mchezo kati ya Azam FC na African Lyon, Picha kwa hisani ya Blogu ya Binzubeiry Kurejea kwa wachezaji hao kunamaliza mgogoro uliokuwepo na kudumu kwa takribani miezi mitano kufuatia shutuma za rushwa ambazo zilipelekwa takukuru kuchunguzwa ili kujua ukweli na uongozi wa Azam FC unaishukuru takukuru kwa kazi nzuri ambapo imegundulika kuwa wachezaji hao hawakuhusika na hivyo kusafishwa na chombo hicho chenye mamlaka ya kuchunguza tuhuma za rushwa.

Wachezaji hao wote wanatarajiwa kuwemo kwenye mchezo wa Jumapili dhidi ya Simba SC ikiwa mwalimu ataona inafaa na wapo katika hali nzuri kuweza kucheza. Mchezo huo wa jumapili ni muhimu sana kwa Azam FC kwani ikishinda itaizidi Simba SC pointi 14 huku simba ikisaliwa na michezo minne na hivyo kumaanisha kuwa Kagera Sugar atabaki kuwa mpinzani pekee wa Azam FC katika kuwania nafasi ya pili.

ni vyema wasicheze kuondoa lawama endapo Azam watafungwa
 
Leo ligi kuu

azam 2 - 2 simba

flop of the match Luckson Kakolaki
 
554563_439508536135412_1739336122_n.jpg
 
Ndetichia,
Asante kwa kutuwekea kumbukumbu maana safari hii timu kongwe mpaka wanaunga 'chama moja' kushangilia dhini ya Azam FC lazima wanaona 'ukiritimba' wao ktk soka la Tanzania unaanza kuyoyoma kwa kasi.
 
Kocha wa Azam FC na sisi wapenzi wa Azam Fc tunasema kama ni mapato mlangoni Azam FC ikicheza dhini ya timu kongwe, mapato ni makubwa tu sasa hofu ya marefa na wadau wengine kuwa hamasa ya kuhudhuria uwanjani watazamaji itapungua siyo kweli bali imeongezeka.

Hivyo wakubali wasikubali Azam FC imechochea kiwango cha ushindani ndani ya uwanja kuwa juu hivyo wasifanye hujuma timu ambazo siyo kongwe kujipenyeza na kuwa kuwa katika msimamo wa ligi ya soka Tanzania.
 
kweli kabisa mkuu tena huwa wanazikandamiza kimakusudi..
 
Kesho gemu yetu na As Far rabbat itaoneshwa star tv stay tuned ni kuanzia saa 10 jioni kesho jumamosi 20/04/13
 
Back
Top Bottom