The Official Azam FC Thread

The Official Azam FC Thread

Mabeki wa Azam wanafanya uzembe, hilo goli la pili ni uzembe wao.
 
Tumia herufi kubwa, AS FAR 2-1 Azam, maana ukiandika as far inakuwa kama maneno ya kizungu tu na sio jina la timu.

aaah huyu beki kazingua kweli.. ngoja tuone kipindi cha pili..
 
kipindi cha pili kimeanza sasa..

as far 2 - 1 azam
 
Mkuu leo inabidi tukae kitanzania zaidi, Azam akishinda hataathiri chochote kwenye ubingwa wenu.

Mkuu natumia Mchina handset, ningekupa 'LIKE', umenena vizuri sana. Ninachukia kuona vijembe kwa timu yangu wakati hatuna utani na Azam. Acheni vijembe tuwasapoti vinginevyo RIP Azam FC.
 
Inabidi Azam watumie cross zaidi kama wanataka kupata goli, lakini kama wataendelea kupita katikati na kupiga mpira mirefu itawachosha tu na wanaweza wasipate goli.
 
Tupo mkuu tunafuatilia...Taifa kwanza

Mkuu hebu waite hawa mashabiki wa Ndala pamoja na wale Mnyama waje huku tuishangilie Lambalamba FC, waambie hii sio ligi kuu hatuna cha kupoteza tukiwashangilia Azam sana sana tunaonyesha uzalendo.
 
Back
Top Bottom