The Official Azam FC Thread

The Official Azam FC Thread

JB19 akirejea katika hali ya kuziona nyavu, wakati walinzi wa timu pinzani wakimtupia jicho KP10, huku kukiwa na super sub KF7. Unazani CHAMA LANGU LA CHAMANZI LITA DROP POINT,
 
Final score: Azam FC 2 - Simba Sc 1

Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
AZAM FC imezidi kupiga kasi katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya jioni hii kukiagusha kigogo, SImba SC kwa mabao 2-1 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Tayari timu hizo zilikuwa zimekwishafungana bao 1-1 hadi mapumziko, Azam FC wakitangulia kupata bao lao kupitia kwa Khamis Mcha Vialli dakika ya 16 na Simba SC wakisawazisha kupitia kwa Joseph Owino dakika ya 45 na ushei.

Mcha alifunga bao kwa urahisi baada ya kutengewa mpira kwa kifua na Kipre Tchetche aliyepokea krosi Gardiel Michael- ambaye naye alipata pasi ya John Bocco aliyefanya kazi kubwa ya kupanda na mpira kutokea nyuma.

Mchezaji wa Simba, Owino alifunga kwa kichwa akiunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na winga machachari, Ramadhani Singano ‘Messi’.

Mshambuliaji wa Azam FC, John Raphael Bocco ‘Adebayor’ alifunga bao la ushindi dakika ya 56 kwa kichwa kufuatia pasi ya tika tak ya Kipre Herman Tchetche.


Picha: Shujaa; Mfungaji wa bao la ushindi la Azam FC kulia akipiga shuti pembeni ya kiungo wa Simba SC, Jonas Mkude.

Habari na picha kwa hisani kubwa ya Source: Bin Zubeiry wa JOHN BOCCO AISOGEZA AZAM FC JIRANI KABISA NA UBINGWA - BIN ZUBEIRY
 
Cdhani kama azam anaweza kua bingwa msimu huu yanga bado nafac ipo
 
team ya azam fc imewasili salama jijini mbeya leo jioni kwa ajili ya mtanange wa kesho dhidi ya mbeya city...

come on lambalamba #AzamFor2014
 
13 April 2014
Mbeya, Tanzania

Final score: Mbeya City 1 - Azam Fc 2

AZAM FC ndiye bingwa mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2013/2014, baada ya kuifunga Mbeya City mabao 2-1 Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

Mchezo ulikuwa mkali na ulianza kwa kasi timu zote zikishambuliana kwa zamu, na sifa ziwaendee makipa wa timu zote mbili, David Burhan wa Mbeya City na Aishi Manula wa Azam FC kwa kazi nzuri ya kuokoa hatari langoni mwao.

Azam walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 43, mfungaji Gaudence Mwakimba aliyemalizia pasi nzuri ya beki wa kulia Erasto Nyoni.

Baada ya bao hilo, Mbeya City walicharuka na kufanya mashambulizi mawili hatari langoni mwa Azam, lakini hawakuweza kupata bao hadi kipyenga cha kuhitimisha kipindi cha kwanza kinapulizwa.

Kipindi cha pili, Azam waliingia na mfumo wa kucheza kwa kujihami ili kulinda bao lao, mbele wakimuacha Mwaikimbe pekee na John Bocco akashuka katikati huku Salum Abubakar ‘Sure Boy' akimsaidia Kipre Balou kukaba kiungo cha chini.

Mfumo huo ulikabirisha mashambulizi mengi langoni mwa Azam na haikuwa ajabu Mbeya City walipokomboa bao dakika ya 70 kupitia kwa Mwagane Yeya baada ya kuuwahi mpira uliopanguliwa na kipa Aishi Manula kufuatia shuti la Deus Kaseke.

Bao hilo kidogo liliwachanganya Azam FC na Mbeya City wakauteka mchezo kwa dakika kadhaa, kabla ya shambulizi la kushitukiza kuipa ushindi timu ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa dakika ya 86, baadaa ya John Bocco kukutana na mpira uliorudishwa.

Wachezaji wa Mbeya City walimzonga refa Nathan Lazaro wa Kilimanjaro baada ya bao hilo na kusababisha mchezo kusimama kwa zaidi ya dakika tatu.

Refa huyo alitoa kadi nyekundu kwa Mwagane Yeya baada ya vurugu hizo. Askari wa jeshi la Polisi walilazimika kufanya kazi ya ziada baada ya mechi kwa kuwadhibiti mashabiki wa Mbeya City waliotaka kufanya vurugu na pia kuusindikiza msafara wa Azam FC.

Pamoja na kuwa timu ya kwanza kuifunga Mbeya City kwenye Uwanja wake leo, Azam FC pia inakuwa timu ya kwanza nje ya Simba na Yanga kutwaa ubingwa wa Bara tangu mwaka 2000 Mtibwa Sugar ilipofanya hivyo.

Azam inakuwa timu ya sita nje ya Simba SC kutwaa taji la Ligi Kuu, baada ya Cosmo mwaka 1967, Mseto mwaka 1975, Tukuyu Stars mwaka 1986, Coastal Union 1988 na Mtibwa Sugar mara mbili mfululizo 1999 na 2000.

Kikosi cha Mbeya City leo kilikuwa; David Burhan, Aziz Sibo/Hamad Kibopile dk50, Hassan Mwasapili, Yussuf Abdallah, Yohana Morris, Anthony Matogolo, Mwagane Yeya, Steven Mazanda, Paul Nonga, Saad Kipanga/Alex Sethi dk68 na Deus Kaseke.

Timu ya Azam FC; Aishi Manula, Erasto Nyoni, Gardiel Michael, Said Mourad, Aggrey Morris, Kipre Balou, Himid Mao, Salum Abubakar, Gaudence Mwaikimba, John Bocco na Kipre Tchetche/Kevin Friday dk51.


Gaudence Mwaikimba akishangilia baada ya kuifungia Azam bao la kwanza, Kulia ni Kipre Tchetche.

Source: Picha na habari kwa hisani kubwa ya Bin Zubeiry BlogSpot AZAM BINGWA LIGI KUU, YAICHAPA MBEYA CITY 2-1 SOKOINE - BIN ZUBEIRY
 
Back
Top Bottom