The Only One My Love moneytalk

Mwifwa

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2017
Posts
48,474
Reaction score
125,866

Hebu tazama uzuri wa sayari nzuri uionayo kichwani kwako, ifikirie taswira ya raha uipatayo huko na kisha rejesha mawazo yako katika muonekano halisi wa dunia uipendayo.

Ingekuwa chaguo la moyo wangu Basi ningetengeza dunia nyingine nzuri nikaishi na wewe tu. We ni chanzo cha Furaha ya maisha yangu kwani kuridhika kwa moyo wangu ni pale nikuonapo tu zaidi ya tabasamu lako hapo hunifanya nihamishe mawazo na niende katika sayari nyingine kimawazo.

Natafakari ukaribu wako hasa pale uwapo karibu na Mimi ni zaidi ya upendo Mara unifunikapo kwa joto lako tamu la uaminifu.

Hakika katika kila hangaiko lina raha yake. Kwani weee ni kile kisima nilichokitafuta miaka nikitembea jangwani na nyikani na hatimae Leo nimefika katika maji matamu ya kuburudisha hisia zangu.

Najiachia na naruhusu nafsi yangu itulie kwako kwani wewe ndio chaguo sahihi la moyo wangu.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…