Mwifwa
JF-Expert Member
- Apr 3, 2017
- 48,474
- 125,866
Hebu tazama uzuri wa sayari nzuri uionayo kichwani kwako, ifikirie taswira ya raha uipatayo huko na kisha rejesha mawazo yako katika muonekano halisi wa dunia uipendayo.
Ingekuwa chaguo la moyo wangu Basi ningetengeza dunia nyingine nzuri nikaishi na wewe tu. We ni chanzo cha Furaha ya maisha yangu kwani kuridhika kwa moyo wangu ni pale nikuonapo tu zaidi ya tabasamu lako hapo hunifanya nihamishe mawazo na niende katika sayari nyingine kimawazo.
Natafakari ukaribu wako hasa pale uwapo karibu na Mimi ni zaidi ya upendo Mara unifunikapo kwa joto lako tamu la uaminifu.
Hakika katika kila hangaiko lina raha yake. Kwani weee ni kile kisima nilichokitafuta miaka nikitembea jangwani na nyikani na hatimae Leo nimefika katika maji matamu ya kuburudisha hisia zangu.
Najiachia na naruhusu nafsi yangu itulie kwako kwani wewe ndio chaguo sahihi la moyo wangu.
Oohoo my love nashindwa hata niseme nini jaman,nimejikuta nalia kwa furaha,kila siku unanifanya nijione mpya nakama vile naitawala duniani nzima kwa mapenzi yako kwangu,mwifwa wangu wewe nimwanaume wapekee sana ktk maisha yangu na naamini ulizaliwa kwa ajili yangu,siku zote sitachoka kumshukuru mwenyezi mungu kwakunipa wewe,nakupenda sana mpenzi wangu,daima tuzidi kumuomba mungu atuongoze katika safari yetu Tanisha! nakupenda mume wangu