Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
duuuh hii imetolewa recycle bin?
ZeMarcopolo sio wewe ambaye huwa unasema Mbowe hakusoma unaweza kutuambia huko UK alikwenda kusoma secondary?Hujui kuwa Mbowe ni member wa JF.
Alikuwa ctive sana wakati yuko shule UK.
Yes kuna watu wanafikiri wanayo-post humu yatapotea...duuuh hii imetolewa recycle bin?
Salaam Wana Jambo.
Kwanza kabisa naomba niwapongeze wale walioanzisha forum hii kama sehemu ya matumizi ya uhuru wao binafsi. Aidha, niwapongeze kwani forum hii ni sehemu ya harakati muhimu ya kujadili mustakabali wa nchi yetu.
Nimesoma maoni, pongezi, malalamiko, hofu, ushauri na mambo mengine kadhaa katika forum hii. Nimejadiliwa mara kadhaa katika hoja tofauti. Nawapongeza wote waliochangia mada zilizonihusu hata kama wamenipinga au kuzusha. Nitoe pongezi zaidi kwa wale walioonyesha kuipenda nchi yetu na kuitakia mema kwa mijadala mbalimbali.
Leo naandika kwenye forum hii kwa mara ya kwanza. Siyo kusudio langu kujibu hoja zinazonihusu moja kwa moja. Aidha, siyo nia yangu kuingia kwenye malumbano ya aina yeyote na wachangiaji. Naheshimu sana uhuru na mawazo ya wote hata kama kwa makusudi au bahati mbaya yanapotosha. Binadamu tunatofautiana katika fikra, uelewa na malengo.
Siasa na uongozi wa Taifa letu vina mahusiano ya moja kwa moja na maisha yetu ya kila siku.Tanzania ni nchi yetu sote. Hatuna sababu ya kufanya masihara na siasa wala viongozi wetu wote. Walio madarakani na wale wenye nia hiyo.
Mara nyingi, binadamu ni wepesi wa kulaumu na kuhukumu. Tunapenda kadhalika, kudai haki pengine bila kutafakari kwa kina tumetekeleza wajibu wetu kwa kiasi gani.
Tupende tusipende, Tanzania ina kilio. Wote tusipojiuliza na kutekeleza wajibu wetu, kila mtu na nafasi yake kukabiliana na msiba huu, kamwe kilio hakitaisha. Muda wetu wa kuishi maisha haya ni mfupi sana na kila mmoja wetu anastahili kujiuliza amechangia nini katika wajibu wa kumaliza msiba huu?
Naamini, tatizo kubwa la kwanza la kukabiliana nalo nchini mwetu ni WOGA na HOFU. Naamini Wana Jambo forum wengi ni watu wenye uelewa wa kutosha. Kwa nchi yetu iliyo hoi kielimu na hata kiuwezo, hawa ni watu wa "kutumainiwa" na familia zao na hivyo nchi yao kwani familia ni sehemu ya nchi. Napenda kuamini ni sehemu ya "cream" ya Taifa letu nanyi kwa kutoa mawazo yenu, mmekuwa sehemu ya harakati.
Nasikitika, wengi wa wana forum wanatumia majina yasiyo ya kweli. Sina hakika kama siyo ishara ya woga! Na kama wasomi, waelewa, wenye upeo wanakuwa hivyo, Watanzania wa kawaida wategemewe wawe vipi? "Authenticity" ya tunayoyaandika inafifishwa na hali hii?
CHANGAMOTO: KWA KUFICHA MAJINA YETU UJASIRI WETU WA KUHOJI, KULAUMU NA KUHUKUMU UNAPINGANA NA DHAMIRA YA HARAKATI? HARAKATI NA WOGA VINAENDANA? WOGA UNAWEZA KUOKOA TAIFA?
By concealing our identity, are we truly living to our motto which says "Where we dare talk openly?"
"The only thing we have to fear is fear itself" - President Franklin Delano Roosevelt, Washington DC, 4th March 1953
Nawashukuru na naomba kutoa hoja!!
Freeman Mbowe
KWANZA KARIBU MWENYEKITI,
PILI NAOMBA SOMA MAWAZO WANGU KUHUSIANA NA ISHU YA MWIGAMBA NA MIENENDO
YETU YA KUTUMIA MITANDAO YA KIJAMII.
Vijana wengi waCHADEMA tumekilaani na kukoseshwa raha na
kitendo cha Mwigamba, pamoja na hayo, hoja alizokuja nazo hadharani
Mwigamba si za kubezwa hata kidogo. Tulaani kwa upande mmoja na
tujikite kwenye maudhui ya hoja zake kwa upende wa pili.
Tunaomba viongozi wetu wakuu wa CHADEMA waangalie namna
wanavyopokea mawazo mapya, namna wanavyowasikiliza wachache, namna ya
kutekeleza maamuzi ya wengi(wengi wape) na namna ya kutekeleza maamuzi
na maagizo ya vikao vikubwa vya kichama. Moja ya hoja ya Mwigamba kuwa
vikao na maamuzi yake haviheshimiwi na viongozi wakuu aliowataja,
sitaki kuamini kuwa hizo kasoro alishawahi kuzisema kwenye vikao sema
tu hao viongozi kama alivyosema hawasikilizi maamuzi ya vikao, kama
hawasikilizi maamuzi ya vikao wataweza kumsikiliza mtu mmoja anaye
wakosoa? kama ndivyo basi hii ndio sababu iliyopelekea kutoka hadharani.
Huenda namna ya hizo nilizozianisha hapo juu zikawa hazifanywi
katika namna ya kuridhisha na kupendeza, kama ndivyo, majukwaa ya
ndani ya chama yatakuwa yananyima fursa ya kupokea mawazo mapya na
kukosoa utendaji wa ofisi za viongozi wakuu. CHADEMA ijitathimini kwa
hili, isiishie kumchukulia hatua za kinidhamu tu Mwigamba bila
kuzifanyia kazi hoja alizokuja nazo hadharani.
Nimefurahi kusikia kuwa ametakiwa kudhithibitisha tuhuma
alizozitoa dhidi ya viongozi wakuu wa chama, natoa rai kama tuhuma
hizi zikithibiti basi Dr.Slaa, Mbowe, Zitto, Arfi na viongozi kama hao
wa upande wa Zanzibar wajiuzulu nyadhifa zao. Wabaki kama wanachama wa
kawaida na tuingize uongozi mwingine, uongozi utakaokuja kuendeleza
mazuri ya watu hao na kuacha mabaya ya watu hao.( kama hayo mabaya yapo
na yakithibiti). Endapo haya mambo yakithibiti na wasipojiuzulu basi
itakuwa ni ndoto kwa CCM kutoka ikulu na ni ndoto kwa CHADEMA kuingia
ikulu.
Kama Mwigamba akishindwa kuthibitisha hizi tuhuma alizozitoa
dhidi ya viongozi wakuu wa chama, asiishie kuvuliwa uongozi tu, lakini
pia afukuzwe uanachama na ikibidi ashitakiwe mahakamani kutokana
kitendo hichi kibaya na kichafu ili iwe fundisho kwa watu wote wenye
tabia kama hii ambao bado hawajajulikana, kwa kufanya hivi hao wengine
ambao bado hawajulikana wanaweza kuacha tabia hii kwa kuchelea
kukutwa na kitakachompata Mwigamba. Nafikiri hii ndio itakuwa njia ya
pekee ya kulinda nidhamu na heshima ya chama mbele ya wanachama na
watanzania kwa ujumla ambao kimsingi ndio wanunuaji wa sera zetu.
Tukilea ujinga huu watatokea wengi wa kutuvuruga kisa tu waliona
Mwigamba kapewa adhabu ndogo au onyo la kulaza ukope.
Hata hivyo sisi tulio nje ya ya vikao tunaweza kujiuliza
operesheni ya M4C imepotelea wapi? Au tumeicha mara baada ya kutokea
tukio la Iringa na vurugu za gesi Mtwara? Hivi ni kweli CCM
wanatuandalia matukio bila kujua? Je, wakiacha kuandaa hayo matukio kisa
tu Mwigamba kawashutua ndio CHADEMA bai bai? Pia tunaweza kujiuliza
uchaguzi wa chama utafanyika lini ikiwa ilisemekana hadi desemba mwaka
huu uchaguzi ungekuwa umekwisha malizika kwa ngazi zote, tunajiuliza
hili la uchaguzi nalo limepotelea wapi? Hizi ni baadhi ya hoja chache
alizokuja nazo Mwigamba hadharani. Je, sisi wanaCHADEMA tuishie kuona
usaliti wa Mwigamba bila kuzingatia hoja hizi? Kwanini viongozi
wasizijibu hoja za Mwigamba?
Kwa vyovyote vile watazijibu, wakati Mwigamba akithibitisha hizi
tuhuma, subira ndio kila kitu katika hili, kama katakiwa kuthibitisha
na kwa vyovyote vile nasi twakiwa kusubiri, kama ndivyo huu wimbo wa
usaliti usaliti unapata uhalali gani katika kipindi hichi cha kusubiri?
Na wale wanawalaumu Mbowe na viongozi wenziwe waliotajwa katika bandiko
la Mwigamba pia wanapata uhalali gani wa kufanya hivyo ikiwa bado
Mwigamba hajathibitisha katika vikao halali na uthibitisho huo
kukubalika? Tuvute subira kwani siku zote ndio huvuta heri, kinyume
chake labda tunataka maamuzi ya chama juu ya hili yazingatie mbwembwe
zetu badala ya uthibitisho wenyewe.
Pamoja na hayo, Mwigamba kama aliona mawazo yake hayasikilizwi
na kutekelezwa, na kama aliamini mawazo yake ni sahihi na yako
kwaajili ya kujenga chama, basi ni vema MOSI angejiuzulu; hakuna
umuhimu wa kufanya kazi na watu usiowaamini na kuwakubali au
wasiokusikiliza au wanaokubeza. Pili, angetoka hadharani, tena si
kwakutumia jina bandia, bali angetumia
Hakuna kitu kinachonipita akili yangu kama kutojibu hoja kwa kujifanya kujibu hoja! Maneno ya kebehi na dharahau yanaweza kuvutia hisia lakini hayashindi hoja. Je upinzani wa Tanzania jinsi ulivyosasa unaweza kukabidhiwa nchi nzima kuiongoza? Jibu langu ni HAPANA HAPANA HAPANA!! Je CCM jinsi ilivyosasa inaweza kuongoza nchi yetu jibu ni NDIYO NDIYO NDIYO! Je CCM na matatizo yake yote na mapungufu yake yanayoweza kujaza vitabu inastahili kupewa uongozi wa nchi jibu ni HAPANA HAPANA HAPANA, Je upinzania namapungufu yake yanayoweza kujaza juzuu wanastahili kupewa uongozi wa nchi jibu ni HAPANA HAPANA HAPANA!! Nitafafanua.
Chama cha Mapinduzi ni chama ambacho kimelewa madaraka na viongozi wake wengi wamebweteka na vyeo vyao na kutokana na chama hicho kukita katika kila kona ya maisha ya Watanzania basi viongozi hao hawaoni haja ya kulitumikia Taifa letu jinsi ile inapaswa! Pamoja na hayo yote, CCM imeweza kufanya mambo ambayo Watanzania wanayathamini licha ya kujua udhaifu mkubwa wa Chama hicho. Unafikiri viongozi wote wasomi walioko CCM hawajui udhaifu wa chama chao au ni sisi wewe kwenye Jambo Forum ambao ndio tuna akili zaidi kuliko Mtanzania yeyote?
Wengi wa wanachama wa CCM ambao wamepima upinzani na chama tawala wamechagua chama tawala. CCM inafanyiwa mabadiliko toka ndani, toka viongozi waliopo ndani, na toka wanachama waliondani. Hawasubiri wakosoaji walio nje kujiunga nacho ndio waanze kufanye mabadiliko!! CHADEMA, CUF, TLP na wenzao hawawezi kusubiri watu wajiunge nacho ndio waanze mabadiliko!!
Kuna watu wanajifanya wanajua historia hapa, bila ya shaka wanaijua historia ile inayowafaa wao na matakwa yao! Martin Luther King Jr hakuwa mwanasiasa, na kilichomsukuma sio haja ya kuwa na cheo cha kisiasa. Alisukumwa na imani yake!! Soma maandiko yake ya "Barua toka Jela ya Birmingham"!
Wanamtolea mfano Abraham Lincoln, nani aliwaambia Lincoln alikuwa mpinzani wakati alipotia sahihi "tangazo la kuwekwa huru" kwa watumwa kusini mwa Marekani? Je unajua hata tangazo lake halikuwafungua watumwa wote? Lincoln, alifanya mabadiliko hayo akiwa Rais wa Marekani! Kwa kifupi, kama kuna mtu anayeweza kuleta mabadiliko makubwa katika Tanzania si Mbowe, si Lipumba, si Mrema, ni Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!
Mmemtaja Mandela, Mandela alileta mabadiliko makubwa zaidi alipokuwa kifungoni au alipotolewa nje? Nitawaacha mfikiri nina maana gani hapo!
Quarz anadai ati siwezi kuwa mkosoaji tu na sitoi masuluhisho ya aina yoyote. Inaonekana hujafuatilia maandishi yangu. Mimi ni mkosoaji mkubwa wa serikali ya Kikwete, nilipigia kelele suala la Mahita kabla ya watu wengi kulipigia kelele, niliungana na wengine kupigia kelele suala la Richmond bila haya (na nikaitisha kuondolewa kwa Msabaha), nilipigia kelele mambo mengi ambayo wasikilizaji wangu wanayajua! Leo nikisimama na kusema kuwa licha ya kelele zangu CCM bado ni chama pekee kinachoweza kuongoza Tanzania watu wanadhani nimejigeuka! Hata kidogo. Mimi sina maslahi katika Upinzani, sina maslahi na CCM (sio mwanachama). Maslahi pekee niliyonayo ni yale yanayohusu Tanzania nzima na siyo chama au kikundi fulani cha watu! Ni kwa sababu hiyo siwezi kutetea kuikabidhi hatima ya Tanzania kwa watu wasio na nia wala uwezo wa kuongoza Taifa alimradi ati ni wapinzani na wao pia wanaichukia serikali ya CCM. Nina madhaifu mengi, lakini ujinga wa kisiasa sio mojawapo!
Nimetoa mapendekezo ni nini upinzani ufanye ili ujiweke mahali pazuri pa kushinda watu wanadhani ninawaletea husuda! Kama wao wanasubiri watu wajiunge nao ndio waanze kujiimarisha, basi waendelee kusubiri!! Anzeni kujiimarisha wenyewe msisubiri hisani ya CCM! CCM haina mpango wa kuwaimarisha wala haina nia ya kuona mmeungana!! Papa mkaange kwa mafuta yake!
Kuhusu hilo la kunitakia nifie huku huku niliko, wala halinitishi kwani nikifa au nikiwa hai mimi ni mali ya bwana, na nitakufa kama Mtanzania, kama nitafia kwenye ardhi ya wazazi wangu au ugenini!! Anyway, nakutakia wewe na wenzio muishi maisha marefu na ya afya, na muweze kuitumikia nchi yetu kwa kujituma zaidi kuliko wale ambao wamefanya hivyo hadi sasa.
Wabillah Tawfiq!
Ni zuri, usingelinukuu kwakuwa unawachosha wanaotumia simuandiko refu lakini lenye mchanganuo wenye afya kuhusu mustakabali wa chadema!
Wakuu,
Hii post iliwekwa mwaka 2006 tuliichangia kipindi hicho.Sasa wengine wasidhani ni mpya
Mheshimiwa Mbowe umenikuna. Umetuthibitishia kama alivyosema Mzee ES kuwa forum hii inapitiwa na watu wazito! Ahsante sana kwa kuingia hapa. It has boosted the profile of the forum, but of course, of our party as well! Najua hakuna kiongozi wa CCM anayeweza kuthubutu kutumbukia humu. Kwanza wale jamaa wana allergy na kusoma. They just dont even read! Chinga waamushe hao wenzako waanze kutafuta maarifa katika maandishi!
Sasa tuwaonye akina Nungwi kuwa hapa hakuna nafasi ya longolongo, hoja zenye akili tu zinatakiwa. Sio blabla na propaganda ya kutetea mambo ambaye hayateteeki.
Nyongezea katika majibu ya kutumia pen names: Binadamu tunahlika wakati mwingine wa kuangalia 'nani amesema badala ya amesema nini'. Kwa hiyo tuliona ili to-focus kwenye hoja tukakubaliana tangu enzi za BCS kwamba tutumie pen names. Ila nakuhakikishia sio kwa sababu ya woga hata kidogo. Hatukuogopi maana mambo mengi humu ndani hatuzushi hata kidogo.
JJ: ni vizuri kwamba kuna kesi Dar kuhusu ubunge wa EAC. Lakini unajua kinachokosekana katika siasa za upinzani TZ na hasa katika CHADEMA ni militarism. We need millitant politics. Hii ya Zitto peke yake anapiga kelele wakati wengine wanaendelea na business as usual inaturudisha nyuma. Bado hatujawatia jambajamba CCM. Na ukiona CCM wanatusifia kuwa ni chama cha wastaraabu, ujue hatujafanya kazi yetu vizuri. Kuna mambo mengi ya ku-capitalise on. Inasikitisha kwamba wabunge wetu hawakulibebea bango suala la Richmond katika bunge lilipita. Hatuku-capitalise pia katika tatizo la wamachinga na wewe kama Mkurugenzi wa Vijana nafikiri hili linakuhusu moja kwa moja. In short, we must miliitarise our political party. Hawa jamaa ni mafia hasa, watatusogeza hadi uchaguzi watakuwa hawajafanya kitu lakini na sisi pia tutakuwa hatuna cha kuonesha kwamba wa are an alternative. Safari njema Dar.
Guys,For God's sake.Tumetoa tahadhari hii ID ilipost karibia miaka 8 iliyopita na tulijadiliana sana hapa wengine muda huu wamebadili ID miongoni mwao my seniors nawajua ,hatusemi hapa.Someni Tarehe ambayo mtu alipost basi.Ah !