Kitabu The Prince, Mwana Mfalme, ni kitabu kilichoandikwa na mwanasias wa kale katika dola la Roma, Niccolo Machiavelli, mwaka 1513. Huyu aliangalia utawala ulivyokuwa, misingi yake, kuendelea au kufifia, na hatimaye akaandika kitabu hiki kama mwongozo kwa watawala wakitaka kudumu.
Moja katika misemo yake inayokumbukwa sana hata leo, na kutolewa ushahidi ni huu ' The end justifies the means', yaani ' Lengo huhalalisha njia yoyote ya kulifikia' Yaani tena, kama lengo lako ni kuhifadhi utawala wako, ni halali njia yoyote utakayoitumia!
Utaona si kitabu cha maadili, lakini hiyo ndiyo hasa hoja ya Machiavelli kwamba katika siasa, kwamba kuendelea kwa Utawala (power),anatoa hoja Machiavelli, kunategemea ukakamavu (strength), kuwa na uhalisia (realism), kujiongeza (adaptability) na utashi wa kuachana na maadili wakati utawala uko hatarini!
Kwa vile sina wakati, acha nifupishe falsafa ya Machiavelli, tuone jee, kuna anayeifuata?
AINA ZA UTAWALA
} Kuna utawala wa kurithi. Anasema, huu ni utawala rahisi sana kwa vile raia wamekwishazoea mfalme wao, au chama kinachowatawala.
} Nchi mpya. Hizi ni zile zilizoshindwa vita, au zilizopata uhuru karibuni. Hizi, anasema Machiavelli. ni ngumu mno kuzidhibiti na zinataka kiongozi ngangari!
MADARAKA HUPATIKANA VIPI?
} Aidha kwa uwezo wa mtu au kwa bahati. Watawala wanaotegemea ustadi wao wa kuongoza wanadumu madarakani muda mrefu kuliko wanaotegemea bahati au vitu vingine.
KUOGOPWA NA KUPENDWA:
Ni vyema zaidi watu wakuogope kuliko wakupende, kama huwezi kuvipata vyote viwili. Lakini kuogopwa kusigeuke kuwa kuchukiwa. Kama itabidi kutumia nguvu, mtawala alifanye hilo mara moja na kwa muda mfupi, na lielekezwe tu kule hatari itokako.
MAADILI NA SIASA
}Mtawala atakayefanikiwa ni yule atakayekuwa tayari kuachana na maadili, ikibidi!
} Kuonekana kuwa mtu mwema ni muhimu zaidi kuliko kuwa mtu mwema.
}Siasa hufuata mkondo tofauti na maadili ya mtu binafsi!
KUZATITI MADARAKA
} Waondoe wapinzani wako. Ametumia neno 'eliminate' wafyeke, watokomeze, wamalize!
} Jaribu kupata sapoti ya raia. Jiepushe na kuchukua mali zao au kuwatweza na kuwavunjia heshima familia zao.
}Endana na wakati na mabadiliko
RISALA YA MWISHO
Italia inahitajia kiongozi shupavu, ngangari kuunganisha nchi na kuihami
Mtawala inabidi abadili staili yake kila wakati unavyosonga mbele
Mtawala adhimu anajitengezea mfumo wake imara kupitia werevu, maarifa na kuchapa kazi, si kusitasita na kupoteza wakati!