The return of champions, kuiokoa Yanga jumapili?

Kijogoodi

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2021
Posts
1,362
Reaction score
2,373
Msemaji mkuu wa Yanga bwana Haji Manara ameongea na waandishi wa habari na kuwahakikishia mashabiki kuwa Yanga itaibuka na ushindi mnono siku ya jumapili dhidi ya timu ya Rivers united kutoka nchini Nigeria kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa Afrika.

Manara amesema wanaenda uwanjani wakiwa na slogan ya The return of champions(Mabingwa wamerudi) na kuwataka mashabiki kuanza kuimba slogan hiyo kama mbinu ya kuongeza hamasa kuelekea mchezo huo.

Manara pia amewataka mashabiki kupuuza habari za uzushi za kwamba Djuma, Aucho hawatacheza kwa sababu hawajalipiwa kwani zinalenga kuwatoa kwenye mchezo.
 
The return of champions - Mabingwa wamerejea

Safi sana.
 
Caf nayo inawahuju si ndio? Tatizo timu inaendeshwa kama kikundi cha panya road,,
Sipati picha ingekuwa ndo tff imewasimamisha wachezaji wao kuhusu huo ucheleweshaji wa itc zao, hayo malalamiko sijui ingekuwaje
 
Kwani wamesimamishwa kweli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…