The return of the king

The return of the king

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2014
Posts
24,501
Reaction score
28,711
THE RETURN OF THE KING

Mourinho anarudi katika EPL kuifundisha Spurs baada ya Spurs kuwa wameachana na kocha wao Pochetino kutokana na kile walichosema ni kutokana na mwendelezo mbovu wa matokeo.

Mourinho alifukuzwa Manchester United mwaka jana ivyo sasa ametumia mwaka mmoja nje ya ukocha nadhani amejifunza mengi na ameona mengi kwenye mpira kipindi yupo nje ya ukocha.

Awali zilitoka taarifa kuwa Mourinho alitakiwa na Lyon lakini alikataa kutokana na kuwa hakuwa tayari kufanya kazi Ufaransa kulingana na maelezo ya rais wa Lyon Aulerius .

Ni siku chache tu Bayern wafukuze kocha wao na ilisemekana Mourinho ndo anaenda kuchukua pahala pa Kovac pale Munchen ila mambo yamekuwa tofauti baada ya usiku wa jana Mourinho kuibukia London mitaa ya White Hat-lane eneo la barafu yalipo masikani ya Tottenham Hot Spurs na kutangazwa kuwa atakuwa kocha mpya wa Spurs atakayehudumu pale hadi 2023.

Mourinho anakuja kuifundisha timu ya aina gani pale?

Spurs ni moja ya timu ambayo ina wachezaji wengi ambao ndo wachezaji vipenz wa mourinho hasa wale wenye nguvu za kukaba na miili mikubwa, wale wenye kukimbia sana na ufundi wa kawaida.

Spurs imejaza hawa watu kitu ambacho kinaonekana wazi kuwa haitomchukua kocha muda kupata First Eleven yake maana silaha zote zipo, yanaweza kuwepo mabadiliko kidogo ila wengi ni walewale labda tusubir maongezo ya January.

Wachezaji wengi wa Spurs wanaweza kucheza physical battle, man to man, in and out track runways nk, na mara nyingi hawa ndo vipenzi wa Mourinho.

Mourinho anakuja Spurs akiwa na benchi jipya la ufundi ambalo limeundwa na Wareno wenzie kutoka pale lile na hawa ni Joao Sacramento na Nuno Santos.

Hawa watu wawili wao ni minded attacking coaches yaani wanapenda sana mpira wa wazi na wakushambulia ambao tunaita modern football Ila tunapokuja kwa kocha mkuu ambaye ni Mourinho yeye ni defensive coach yaan kocha anayependa kukaba sana na kucheza kwa kujifunga sana, hapo unaweza ukaona kitu.

Nataka niseme kuwa hii combination sasa inaweza ikamfanya mou awe bora pande zote yaan katika kukaba na katika kushambulia na ukiingalia spurs INA hao watu wote wanaoweza kushambulia na wakabaji pia.

Vipi, Mourinho ni kocha sahihi kuja spurs?

Swali hili ningependa kujibu kwamba kwa muda huu Spurs ilihitaji kocha wa aina ya Mourinho kwa sababu imejengwa muda mrefu na haina mafanikio makubwa upande wa vikombe, Spurs wamekuwa wakifanikiwa ktk kuvuna pesa ila linapokuja suala la ubingwa wamekuwa hawana mtu wa kuwapa kombe.

Mtu wa kuwapa kombe sio mchezaji tu Bali hata kocha na mbinu zake na mtu sahii wa kukupa makombe ni Mourinho.

Moja ya makocha bora kuwahi kuwashuhudia wakitafuta vikombe duniani huwezi kumtoa Mourinho katika wale wanne; atafundisha ovyo lkn ataipa timu kombe, na kiu ya wanaSpurs wote ni kombe.

Kwenye mpira siku zote maboss wa team yaan ile bodi ya wakurugenzi huwa inalenga kwanza kupata pesa ili kunufaika kutokana na mwenendo wa kampuni (timu), ila mashabiki wao mara zote huwa wanataka (makombe). Na hili kuwepo na usawa lazima uwe na kocha ambaye n mkubwa na anaweza kufanya vyote kwa wakati mmoja kama mourinho (anakupa makombe na atakupa pesa).

Vipi mourinho atafanikiwa pale spurs?

Naweza kusema kuwa kwa msimu huu katika EPL kufanikiwa kwa mourinho n kugumu ila anaweza kuirudisha timu katika nafasi zile sita za juu, ila kuhusu UEFA naiona Spurs hii inaweza ishangaza dunia tena kama walivyofanya misimu mitatu mfululizo iliyopita na linapokuja suala la game za knock out Mourinho anajua kucheza sana hizi mechi na ni mbobevu wa mashindano haya ya ulaya kwa miaka mingi.

Aidha Mourinho anaweza kufanya vizuri pale Spurs kutokana na kwamba ameenda timu ambayo haina pressure kubwa za mashabiki kama alikotoka yaani naweza nkasema kuwa Spurs hii n sawa na Porto ya 2003-2005 na Inter ya 2010. Hapa Mourinho alifundisha mpira bila pressure na alipata mafanikio makubwa.

Pia Mourinho anaenda timu ambayo anaizid sasa katika mafanikio kimakombe, amechukua makombe 25 na Spurs wana makombe 24 jumla ivyo anaweza kupewa muda afanye kaz kwa uhuru zaid kuliko sehemu nyingine na hili linaweza kumfanya afanikiwe.

Aidha, Mourinho anaenda kufanya kazi na boss ambaye hana fujo na makocha wake na sio muongeaji sana (Dany Levy). Mara nyingi tumemuona Levy akisema vitu huwa anatekeleza, sasa nadhani hili pia linaweza kumsaidia Mourinho afanikiwe.

Kutoka kwa Rafiki yangu Ramsey

IMG-20191120-WA0013.jpeg
 
Wachezaji wa huyu Mreno, Mourinho ni wa msimu moja. Anawachosha mno wachezaji, mwisho wa msimu majeruhi kibao. Anawakimbiza mbaya, nguvu nyingi. Hataki kutengeneza wachezaji, hana muda, anataka matokeo kwa namna yoyote.
 
Ngonja tuone j moss atafanya nn
Huwez kumpima kwa mech 1

Ndio maana levy amempa muda had 2023

Sasa hivi napata taarifa hapa

Mou amemuomba Levy alimlete LUIS CAMPOS

Director aliyewaibua kina

Bernardo Silva

Mbappe

Pepe

N.k

[@SkySports] | Highly respected sporting director Luis Campos is open to the idea of joining Spurs and working with new head coach Jose Mourinho at Tottenham Hotspur with a view to becoming the club’s new sporting director.

#THFC #COYS Ricky Sacks 🎙 on Twitter
 
Wachezaji wa huyu mreno,Morinyo,ni wa msimu moja. Anawachosha mno wachezaji,mwisho wa msimu majeruhi kibao. Anawakimbiza mbaya,nguvu nyingi. Hataki kutengeneza wachezaji,hana muda,anataka matokeo kwa namna yoyote
Mou amekuta Spurs imekamilika hapo nikuongeza tu wahuni wawili watatu.
 
Anataka kumleta Pepe na Ramos waendeleze ukatili.
 
..probability ya mou kufanya vizuri ipo na hii timu ilivyojikamilisha kwa sasa, labda aongez wachache
Tuanze kusikia harufu ya vikombe spurs
 
Back
Top Bottom