The Richest Man In Africa: Kila Utajiri una Ukafiri nyuma yake

 
Brother Habibu! I salute you! tafadhali naomba unitag!!Thank you!
 



The Richest Man in Africa: Kila utajiri una ukafiri nyuma yake







SEHEMU YA PILI





Katika sehemu ya kwanza ya mfululizo wa makala hii nilieleza juu ya kifo cha kamanda Anselme Masasu aiyehukumiwa na kupigwa risasi mbele ya rafiki yake na msaidizi wake Antoine Ngalamulume msituni karibu na mji wa Lubumbashi. Pia nilieleza juu ya kikao cha siri kilichofanyika katikati ya jiji la Kinshasa kati ya raia a Lebanoni na mfanyabiashara maarufu wa almasi Bwana Bilal Hritier aliyekutana na mwakilishi wa ‘kigogo’ kutoka Rwanda na George Mirindi ambaye alikuwa ni moja kati walinzi wakuu wa Rais Laurent Kabila. Kisha nikaeleza juu ya mabadiliko ya biashara ya madini ambayo Rais Kabila alikuwa anayafanya kutoka kuwa na ‘deal’ ya moja kwa moja na Heritier mpaka kuwapa kampuni ya kiisrael iitwayo IDI Congo ‘monopoly’ ya biashara ya almasi ndani ya nchi ya Congo. Lakini pia nilieleza juu ya mipango ya Rais Laurent Kabila kwa kushrikiana na Israel kutaka kutengeneza kitengo maalumu cha intelijensia ndani ya jeshi la Congo ili kubaini mapandikizi na wasaliti wote ndani ya jeshi.



Katika sehemu hii ya pili pia nitaeleza mfululizo wa tukio lingine muhimu ambalo lilitokea na tutalitumia kama rejea huko mbele kadiri hii makala inavyoendelea.



Tuendelee…





Kuna suala moja adhimu sana kuhusu saikolojia ya viumbe wote hasa wa asili ya wanyama akiwemo binadamu. Kwa mfano, licha ya ukali na ukatili wake wote, ukiweza kumchukkua simba angali bado mtoto na kumlea, pindi atakapokuwa mkubwa atakuwa tishio na uwezo wa kudhuru watu wote isipokuwa wewe ambaye umelea. Saikolojia ya wanyama wote ina ombwe la kiu ya mafungamano ya kudumu na kiu ya utii kwa wale ambao wamekuwa nasi tangu siku ya kwanza. Ombwe hili la kiu ya utii na mafungamano kama ambavyo ilivyo katika saikolojia ya wanyama wengine ndivyo vivyo hivyo pia ilivyo katika saikolojia ya binadamu. Kwa namna yeyote ile tunajitahidi mno kuwa na utii na kufungamano na wale ambao wametukuza na kuwa nasi tangu siku ya kwanza au tulipokuwa kwenye hali ya utete.

Nimeanza mjadala wangu kwa kusema hili ili kujenga msingi wa kile ambacho nataka kukieleza katika sehemu hii ya pili.





Wanasema kwamba madaraka yanalevya na yanaweza kukufanya usisfikiri sawa sawa na kuhisi kwamba unaweza kufanya lolote na yeyote yule asikuguse. Ulevi huu wa madaraka unaweza kukufanya hata ukajisahu na kuvuka mpaka wa kupuuza mafungamano na utii watu walionao kwa mtu ambaye unaunda naye uadui.

Kifo cha kamanda Masasu kilikuwa kama mwiba kwenye serikali ya Rais Kabila. Sijui kama Kabila mwenyewe hakulifikiria hili kabla au labda hakudhani kama litakuja kuzua kizungumkuti ambacho alikuwa anapambana nacho wakati huo.



Uvumi juu ya kuwawa kwa Kamanda Masasu kulizua taharuki kubwa na sintofahamu ndani ya jeshi la Congo. Masasu alikuwa ni kipenzi cha wanajeshi wengi na wengi walikuwa na utii na mafungamano naye wakumuona kama ‘mlezi’ wao.


Kamanda Anselme Masasu


Wanajeshi wengi ambao walishiriki katika mapigano ya kumng’oa Mobuttu na kumuingiza madarakani Kabila walikuwa ni ‘vijana’ wa Masasu.



Kumbukumbu zinaonyesha kwamba Kamanda Masasu hakuwahi kupata mafunzo rasmi ya kijeshi katika maisha yake bali akiwa mtoto alichukuliwa na waasi nchini Rwanda na kufanywa mpiganaji wa msituni. Baadae akiwa kijana wa miaka ishirini na sita hivi alianzisha kikundi chake cha wapiganaji na wanajeshi wake wote walikuwa ni watoto. Baadae kikundi hiki kilikuwa kikubwa kwa idadi ya mamia na ndipo hapa ambapo alikipa jina la Revolutionary Movement for Liberation of Zaire. Mbele kidogo katika muendelezo wa makala hii nitaeleza juu ya uhusika wa ‘kigogo’ wa Rwanda katika kuunda kikundi hiki cha Kamanda Masasu kwa lengo la kwenda kuvuna rasilimali za nchi ya Congo. Katikati ya miaka ya tisini kikundi hiki cha Kamanda masasu kiliunganisha nguvu na kikundi cha waasi wa Kabila na kufanikiwa kumng’oa madarakani Dikteta Mobutu Sese seko. Kwa hiyo kwa maneno mengine Rais Kabila aliingia madarakani kwa mgongo na nguvu ya wanajeshi watoto wa Kamanada Masasu. Ndio maana siku ile msituni alipotakiwa kujitetea juu ya kupanga njama za kumpindua Rais Kabila, Masasu alikuwa na kiburi cha kutamba kwamba ‘Kabila yuko Madarakani kwa sababu yeye ameruhusu awe madarakani’. Jambo la kusikitisha zaidi hata walinzi wakuu wa kijeshi wa Rais na wanausalama walikuwa ni ‘vijana wa masasu’ ambao chimbuko lao ni kwenye kile kikundi cha wanajeshi watoto wa kamanda masasu waliotoka naye mpakani Rwanda.

Nitaeleza pia kwa undani chanzo hasa cha mgororo wa Kabila na Masasu, lakini kwa ufupi tu ni kwamba ilifikia muda Rais Kabila alianza kumuona Masasu kama tishio kwa utawala wake. Kukubalika na umaarufu wa Kamanda Masasu kwa jeshi ulikuwa ni mkubwa kufikia hatua kwamba alimzidi hata Rais kwa umaarufu na kukubalika ndani ya jeshi. Ndio maana Rais Kabila alihisi suluhisho la kuondoa tishio hili ni kumuondoa Masasu duniani.



Taarifa za kuuwawa kwa Kamanda Masasu zilianza kusambaa mwishoni mwa mwaka 2000 mwezi Desemba. Katika jeshi kulikuwa na taharuki kubwa watu kutaka kujua kama ilikuwa ni taarifa ya kweli ama la.

Serikali ya Kabila baada ya kugundua kuwa wamefanya kosa kubwa kumuua Masasu kutokana na utii wa wanajeshi wengi walionao kwa Masasu kutokana na mafungamano yao naye kwani ni kama aliwalea kutokea utoto wao alipowaingiza kwenye kikundi chake, ilibidi serikali kutumia nguvu kubwa kukanusha kuwa Masasu ameuwawa.

Kumbukumbu nzuri ni mkutano wa waandishi wa habari uliofanywa na Mandhimu mpya wa jeshi Generali Sylvestre Luetcha akiwa ameongozana na Generali Francois Olenga walikanusha vikali kabisa kwamba masasu hajauwawa bali anashikiliwa na serikali katkka jela ya siri kutokana na kosa la uhaini. Baada ya taarifa hii kueneo watu wengi walilipukwa kwa hasira wakitaka basi angalau Kamanda Masasu aonyeshwe kwa wanahabari, na ndipo hapa Genereali Francois Olenga alitoa jibu maarufu sana ambalo alinukuliwa akisema “Wahalifu wanaotishia usalama wa nchi hawapaswi kufanywa maonyesho”.



Licha ya serikali ya Kabila kujitutumua mno kuaminisha umma na wanajeshi kwamba Kamanda Masasu yuko hai lakini uhalisia ni kwamba hofu na hasira ilizidi kuwa kubwa miongoni mwa wanajeshi ambao walimuona Masasu kama ‘Baba yao’.




Huyu mwanajeshi aliyezungushiwa mng'ao wa duara ambaye alikuwa ni moja ya walinzi wakuu wa Rais Kabila alikuwa ni moja ya vijana waliolelewa na Kamanda Masasu katika kikundi chake cha wanajeshi watoto wa msituni.


Katika tukio muhimu zaidi ambalo tutalitazama kwa undani zaidi kadiri ambavyo tunaendelea na makala hii basi ni tukio la siku ya tarehe 16 mwezi January mwaka 2001.

Ilikuwa ni siku tulivu, siku ya kazi ndani ya mji wa Kinashasa kama siku nyingine zote. Rais Laurent Desire Kabila alikuwa ofisini mwake katika katika makazi ya Rais ambayo mwenyewe alikuwa ameyapa jina la “Palais de Marbre” (Marble Palace). Yeye pamoja na msaidizi wake maalumu aliyeitwa Emile Mota walikuwa wanajiandaa kwa ajili ya mkutano wa nchi zinazozungumza lugha ya kifaransa ambao ulikuwa unafanyika siku chache kutoka siku hiyo. Katika chumba cha pili kulikuwa na Bw. Leonard Mashako Mamba ambaye alikuwa ni Waziri wa Afya wa Congo kipindi hicho naye akisaidia maandalizi ya mkutano huo.

Ofisi ya Mzee Kabila katikati ilikuwa na meza kubwa ndefu hivi ya duara kama ya mikutano alafu pembeni kabisa mwa ofisi hii ndio kulikuwa na meza na kiti cha ofisi cha Mzee kabila mwenyewe. Meza ile kubwa ya duara katikati ya chumba cha ofisi ilikuwa inazungukwa na viti vitatu vya sofa kila upande. Siku ya leo kiti kimoja kilikuwa kimekaliwa na Rais Kabila na kiti kingine kile cha pili kilikuwa kimekaliwa na msaidizi wake Emile Mota.



Ofisi hii ilikuwa na mlango mkubwa wa kawaida mbele yake lakini pia kwenye upande mmoja wa chumba cha ofisi kulikuwa na ‘private entrance’ ambayo ilikuwa inatumiwa na Mzee kabila mwenyewe na watu wachache maalumu. Mzee Kabila na msaidizi wake Emile mota wakiwawanaendelea kupitia hotuba yake alisikia mlango wake ule maalumu ukifunguliwa. Mlangoni pale alisimama moja ya walinzi wake wakuu aliyeitwa Rashidi. Alipiga saluti na kisha kusimama kwa ukakamavu akiashiria kusubiri ruhusa aingie ndani. Mzee kabila kwa tabasamu kabisa alimkaribisha Rashidi aingie ofisini.

Kwa mujibu wa ushahidi ambao umetolewa na Emile Mota, Rashidi alipoingia ndani ya ofisi ya Mzee Kabila hakusema neno lolote lile, alichomoa bastola kutoka kiunoni mwake na kumtandika Mzee Kabila risasi ya kwanza ambayo ilimpata kifuani. Risasi hiyo ilimfanya Mzee kabila kudondoka chini pamoja na kiti ambacho alikuwa amekalia. Akiwa anatapa tapa pale chini RAshidi alimuongeza Risasi nyingine mbili ambazo zilimpata tumboni.



Ni ajabu sana, nasisitiza… ajabu sana, Rashidi hakumdhuru Emile Mota ambaye alikuwa amekaa pale pembeni ya Mzee Kabila. Badala yake Rashidi alitupa bastola chini na kisha kuanza kukimbia kutoka kwenye chumba cha ofisi. Rashidi akiwa anakimbia kutoka ofisini alipofika mlangoni alikutana na Leonard Mamba ambaye alikuwa kwenye chumba cha pili na alikuwa anakuja ofisini kwa Kabila aliposikia milio ya risasi. Emile Mota alikuwa anamkimbiza Rashidi kwa nyuma huku akipiga kelele kwa lugha ya Kiswahili, “..amepiga mzee masasi… amepiga mzee masasi (risasi).!”



Baada ya kusikia kelele hizi, moja ya walinzi wa Ikulu aliyeitwa Chiribangura baada ya kumuona Rashidi akikimbia kutoka kwenye ofisi ya Rais, alimfyamtulia risasi Rashidi ambaye ilimpta mguuni na kumfanya apoteze fahamu papo hapo.



Msaidiki mkuu wa kijeshi wa Mze Kabila ambaye pia alikuwa ni binamu yake, Kanali Eddy Kapend mbaye alikuwa eneo la Ikulu aliwasili mara moja kwenye eneo ambalo Rashidi alikuwa amepigwa risasi na Chiribangula. Kanali Kapend aliwasili akiwa ameshikilia bastola aina ya Kalashnikov mkononi. Chiribangula alipomtazama tu Kapend usoni alihisi kile ambacho alikuwa anataka kukifanya na alijitahidi kweli kweli kumsihi asifanye kile ambacho alikuwa anataka kukifanya… alimsihi asimuue Rashidi bali wasubiri azinduke na waanze kumuhoji kwa nini amempiga risasi mzee Kabila. Lakini Kapend hakutaka kumsikiliza Chiribangula, alimfyatulia Risasi kadhaa Rashidi na kumuua pale pale.



Jambo ambalo wakati ule hata serikali ya Congo wenyewe hawakulifahamu ni kwamba nje ya ukuta wa uzio wa Ikulu kulikuwa na gari ambayo ndani yake alikuwemo George Mirindi, moja ya wanausalama ambaye alikuwa ni mlinzi wa Rais. Mpango ulikuwa kwamba Rashidi akishampigarisasi Mzee kabila akimbie na kuruka ukuta na akifika nje George Mirindi ampakie kwenye gari na kutokomea pamoja.

Lakini baada ya Mirindi kuona Rashidi hatokei na milio ya risasi inaendelea kuunguruma ndani ya Ikulu alielewa kwamba mpango wao umeenda mrama. Kwa hiyo akang’oa gari na kutokomea katikati ya jiji la Kinshasa.

kama tujuavyo namna ambavyo habari mbaya inasambaa kwa kasi, kukaanza uvumi ndani ya jeshi kwamba Rais Kabila ameuwawa.
Kanali Eddy Kapend, yule binamu wa Mzee Kabila aliyempiga risasi na kumuua Rashidi, kinyume kabisa na protokali alichukua simu na kuanza kuwapigia simu wakuu wote wa vikosi vya jeshi maeneo yote ya Congo kuwaeleza kwamba Mzee Kabila amepata ‘ajali’ ndogo lakini ni mzima na hivyo wanatakiwa wadhibiti wanajeshi wao kusije kuzuka taharuki ndani ya jeshi ambayo inaweza kutishia usalama wa nchi. Japokuwa Kapend alikuwa na cheo kidogo kijeshi kulinganisha na wale wakuu wa vikosi ambao alikuwa anawapa amri, lakini wakuu wale wa vikosi vya jeshi walitii kwa sababu Mzee Kabila kwa muda mrefu alikuwa anapenda kumtumia Kapend kutoa maagizo kwa viongozi wa kijeshi. Kwa hiyo wakuu wale wa vikosi vya jeshi walitii maagizo ya Kapend kana kwamba yanatoka kwa Mzee Kabila, Amiri Jeshi wao mkuu.
Kapend hakuishia hapo tu, bali pia kinyume na protokali ya nchi alikwenda mpaka kwenye kituo cha televisheni cha Taifa na kutoa hotuba ya moja kwa moja kwa taifa kuwaeleza kwamba ni kweli Mzee Kabila amepatwa na ‘ajali’ ndogo hapo Ikulu lakini ni mzima hivyo wananchi wanapaswa kuwa watulivu na kusubiri taarifa zaidi zitawajia juu ya afya ya Mzee Kabila.


Lakini ukweli ni kwamba Mzee Kabila alifariki pale pale alipopigwa risasi.

Japokuwa hali ya dharura haikutangazwa moja kwa moja, lakini jeshi liliwekwa kwenye utayari wa hali ya juu huku anga la nchi hiyo likifungwa na hata wanajeshi na watu wa usalama wakiranda randa kwenye mitaa ya Kinshasa.

Kwa hiyo ili kuhalalisha kile ambacho walikuwa wanawaambia wanachi, kwamba Mzee Kabila ni mzima japo amepata ‘ajali’ ndogo… ilibidi mwili wa Kabila usafirishwe mara moja kwa ndege kutoka Congo kwenda Zimbabwe kwa ajili ya “matibabu”.

Wakati ‘maigizo’ hayo yakiendelea, viongozi wakuu wa jeshi na ‘wazee’ walituma taarifa kwenda Lubumbashi ambako mtoto wa Mzee Kabila, Joseph Kabila alikuwepo kwa ajili ya kazi maalumu ya kijeshi. Joseph Kabila alitakiwa kufika Kinshasa mara moja kwa ajili ya suala maalumu ambalo ‘wazee’ hao na viongozi wa kijeshi walidai kwamba Mzee Kabila alikisema kabla ya ‘ajali’ aliyoipata.



Rashidi Muzele



Kanali Eddy Kapend




Itaendelea…

The Bold - 0718 096 811
To Infinity and Beyond
 

Attachments

  • IMG-20180614-WA0024.jpg
    18.6 KB · Views: 288
SEHEMU YA PILI


Nifah Divine... glory to yhwh BansenBurner Alisen Papushikashi Magazine Fire miss chagga SANCTUS ANACLETUS mngony Excel Mussolin5 Jimena Inferiority Complex gwijimimi wambura marwa Hoshea shareef conscious wambeke The Boss Deejay nasmile gkileo Juma chief Mangi flani hivi Ngongo makaveli10 KENZY kadada wa pili Root aretasludovick jonnie_vincy Clkey KAFA.cOm mbewe makedonia Afande Nyati peterchoka Leonard Robert Nchi Kavu STUNTER Chrizo jully Van persie Khalidoun Tetramelyz punje haradari Mazigazi @Alybaba babu na mjukuu platozoom jimmyfoxxgongo Nicodemas Tambo Mwikozi Ls man Heaven Sent sifongo Infantry Soldier haa mym 20acres MTS MarkHilary compos Tembo2 Erick the future nancy1983 Bulah binsaad Fazzaly the wolf everhurt Melvine Mgibeon kijana wa leo samsun Coolant Jagood pacesetter apologize payton George Betram kisengeli Kiranga Jiwe Linaloishi Madame B jay john Guasa Amboni Dinazarde Analyse Diva Beyonce snowhite Mmanu Expected Value onechromosome Missy rose Innocenthezron Immortal_MH Ficus sunola Robot la Matope mamaafacebook II JEKI likikima Compact scorpio me G'taxi YNWA adna yuzo ntamaholo Otorong'ong'o naan ngik-kundie kandukamo1 AFRICA101 mwalidebe Kobe Blaki Womani kalendi savius The Great Emanuel r2ga Ntaluke.N. Transcend Msemachochote Mchumiajuone mwampepec MTOTO WA KUKU Fukara proto cute kawombe zinginary MLALUKO JR Vupu barafu BlackPanther Ntuzu Matola impongo ntamaholo Mkoroshokigoli Deadbody KING easy mahoza Msolo kkenzki deborah1 KIDUDU buffalo44 winlicious riziki Allys MUHUNZI Moses2015 nacktary Liuumi dochivele Renzo @barbers hmjamii mbere TATIANA famicho LUCKDUBE mwanadome Straton memphis ghazar Graph Theory Honey Faith Shunie Slave ddcmanesto zinginary pacesetter Nkanaga KOMUGISHA mikatabafeki johnsonmgaya lee empire wigo MJINI CHAI Asprin mtzmweusi Erasto kalinga Chrizo kichakaa man LULU bike FORTALEZA poleni shibumi ZE DONE umande Edger Sr sir joshua sammoo Roram Password Bavaria hambiliki mwanangu Asili100 Evarist Massawe nice1 Jumong S Rogie 1babake nasreen uberito baest dustless Kilemachocho Tumosa mtembea kwa miguu Debbs Joe scorpnose musacha shibumi seeker of knowledge Simuchi Veni Vidi Vici TUJITEGEMEE abuu garcia Hon Nkundwe Festo Festo marion09 mike2k The dream bro kay vandelintz kirikou1 POINT LOAD lusaka city Dirham Rodcones bato MANCNOO multiphill90 GEORGE Dalali mwanamalundi90 MwaFreeca Roram Ta-kibombo troublemaker mambo KOMUGISHA calabocatz Papaa Azonto Msemachochote Mdomo bakuli tizo1 option dikembe iL Buono fakalava ABDUL KAREEM @Gobe Justine Marack Goodluck Mchika MR UNINFORMED darcity nkasoukumu nG'aMBu thatonegAl kabanga MPARE KIBOGOYO Edward Sambai Rassa mnonje srinavas last king of uscoch proto cute Kennedy krava Rais2020 kbosho Mzee wa BsN sam2000 fuma 999 Bableee dawa yenu The Certified DON SINYORI mij addenbwii ONTARIO Kobe The Vein Mondray jaxonjaxon successor mzee wa liver sawariya Sitaki ukuda Domhome Mpatanishi MKANDAHARI mtugani wa wapi huyo wealthier cluecell Toyota escudo mgumu2 troublemaker Linamo shedede kamtu33 SteveMollel ngushi Donald stewart Mshuza2 Glycel mnonje Ochuanilove SingleFather Santi DEOD 360 ngushi anatory antony ukhuty chris van chicha auxillius Goma Son Hubeb pes KING DUBU VILLAIN mwayena donbeny Aleppo JipuKubwa shoo61 BOMBAY John mungo Nyakageni bato Dogo 1 sufra chamlungu painscott wegman Bravo Engliash MOSELBAY wa stendi FaizaFoxy bigmind cadabraa Internal Kelvin mwalukas mnonje Kelvin X Somoche Wgr30 Miiku Poise Jabman kalamuyamwalimu BOMBAY the say juxhb witnessj Gide MK Mmanyema mgogoone Mnongane Mandingo koncho77 afsa ngaboru Paradoxer Heavy Metal KIMBURU 06 Raaj kichekoh ngumba njeche kikale DullahTza Goodluck Mshana julius Darcy Denis Kasekenya mashonga kitalembwa Khaleed Shaban middle east SirChief jiwe jeusi Mkambarani mansakankanmusa gambada ynwa ney kush mossad 03 white wizard xtaper Mzigua90 Ollachuga Oc Gidbang Mateja M.G Yango jipu abaa4all DIBAJI Agenda1 Grahnman The MaskmaN Slim5 Xubzero agprogrammer JoJiPoJi Architectus blance86 Mamtolo monde arabe Ngao Ya Imani stardust JK naiman64 Dharra seledunga ABB SHAMMA Richard Waziri wa Kaskazini Mwinjuma1 Kanungila Karim baracuda Mwamba028 besaro Pyepyepye Bilionea Asigwa ibn Kiti Chema Tugas Royal Warrior mederii mmangO manzi james LIKUD adrenaline Royal Son Mhadzabe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…