The rise and fall of Colonel Muamar Gadaffi

Sasa hivi tutaletewa kila aina ya ushahidi na documents ambazo zina lengo la kuonesha utawala wa Gaddafi ni mbya, ulikumbatia West na US..
Basi documents zipatikane nyumbani kwa ofisa wa ubalozi wa UK, au ofisi za usalama,ujasusi wa Libya, kwenye dust bins, kwenye dumping sites....lengo hapa ni nini?
Demonisation na public opinion shaping....hili usilisahau.

Kitu ambacho hakitafanyiwa kazi wala kutakiwa ushahidi ni kuwa US-NATO wameingia Libya kufanya Regime change kinyume na Azimio la "no fly zone".
Kwa bahati tumetekwa na propaganda ya NATO-US na sisi kujisahau na kuwapa wao open check au kuona wanayoyafanya ni sawa.

US-NATO wamekiuka mipaka ya Azimio lao( azimio la no fly zone) na operation protect civilians badala yake wameleta nakama Libya, wameunda humanitarian crisis ambayo haikuwepo, wameharibu na wanaendela kuharibu miundo mbinu, uwezo wa Libya kujitosheleza, kujitegemea, kujenga chuki za ukabila, ...kiufupi walilomtuhumu Gaddafi ndilo wanalolifanya....and we give them a pass na badala yake tunamlaumu Gaddafi na serikali yake.

Nchi zetu zikiwa kwenye chaos, US-NATO ndio faida yao, pale ambapo hakuna chaos basi huzianzisha kama ambavyo imetokea kwa Libya.

Miafrika tuamke! US-NATO wanatuchezea akili and we easily fall for their lies.
 
...na badala yake tunamlaumu Gaddafi na serikali yake...
Licha ya mchezo mchafu unaochezwa na NATO kutokumlaumu Gaddafi ni makosa. Gaddafi na serikali yake ni lazima walaumiwe kwani wamechochea (kwa maoni yangu) kwa kiwango kikubwa timbwili la Libya.
 
When Muammar Gaddafi's soldiers fled this corner of a field outside Tripoli where they were camped, they left behind their army fatigues, a can of Brut deodorant -- and a Scud tactical missile.
Days later, the Soviet-made rocket, loaded on its launch truck and pointing towards the Libyan capital, is still sitting under the eucalyptus trees where they left it. The motley rebel forces who overthrew Gaddafi two weeks ago have set up no guard to prevent anyone taking it away or looting it for parts.

Western powers and Libya's neighbours fear that the power vacuum could allow huge quantities of unsecured weapons left over from the civil war to end up in the hands of Islamist militants, in particular the North African branch of al Qaeda.

Officials with Libya's interim government, the National Transitional Council, say they are trying to secure these weapons. But there was little evidence of that at the Scud site, in farmland about 25 km (15 miles) southeast of Tripoli.

RPT-EXCLUSIVE-Abandoned Libyan missile: a gift to militants? | News by Country | Reuters

Hii Vita ya NATO-US ilipoanzishwa hakuna chombo kilichoripoti kuwa ni civil war...sasa hivi kila chombo kinaripoti kuwa ni civil war. Je Ocampo hana kesi ya kuifungulia NATO kwa kuwabeba upande mmoja katika vita hii?

Nani atawachukulia hatua, viongozi wa France, UK, US kwa kuamuru mauaji ya raia wasio na hatia huko Libya?

Lakini hili la silaha kuangukia mikononi mwa islamists!!!??? Hivi US-NATO hawakujua kuwa wanawatumia islamists, terrorists katika vita hii?
Au ndio kutengeneza mazingira ya kuingiza jeshi lao kuikalia Libya kwa kisingizio cha kumaliza pockets of Gaddafi loyalists na kudhibiti silaha za Libya baada ya vita?
 
Licha ya mchezo mchafu unaochezwa na NATO kutokumlaumu Gaddafi ni makosa. Gaddafi na serikali yake ni lazima walaumiwe kwani wamechochea (kwa maoni yangu) kwa kiwango kikubwa timbwili la Libya.

Mkuu,
Lifafanue hilo kwenye nyekundu. Vipi Gaddafi na serikali yake wamelichochea?

Kumbuka Jeshi la Ghaddfi lilijibu mapigo baada ya vituo vya polisi kuchomwa moto,askari na wanajeshi wa serikali kuuawa, gereza kuvamiwa na kuachiwa huru wafungwa huko Benghazi. Gaddafi alikabiliana na armed gangs.

Misinformation ilipikwa kuwa Gaddafi kaua "peaceful protesters" wapatao 6000.na kuwa Gaddafi ana nia ya kufanya mauaji ya halaiki Benghazi.

Ukiondoa hayo madai ambayo yamethibitishwa kuwa hayakuwa na ukweli, pata muda ,eleza vipi Gaddafi na serikali yake ni wa kulaumiwa katika hili.
Ili tumlaumu kama kuna hoja inayoshawishi kufanya hivyo.
 
Mkuu,
Lifafanue hilo kwenye nyekundu. Vipi Gaddafi na serikali yake wamelichochea?...
Kukaa madarakani kwa muda mrefu mpaka kujifikiria kuwa ni watawala wateule na ile "nji " ya Libya ni mali yao. Kasheshe lilipoanza Gaddafi angejaribu kutumia hekima na sio kujifanya yeye ni kisiki kisichong'oleweka. Mara hii imekula kwake!
 
Watoto wa Gaddafi wajitoa Bani Walid?

Libya conflict: Gaddafi sons 'left Bani Walid'
5 September 2011 Last updated at 11:27 GMT

Anti-Gaddafi forces have moved into positions around Bani Walid

Two sons of fugitive Libyan leader Col Muammar Gaddafi were holed up in the town of Bani Walid until Saturday but have now left, the head of the interim government has told the BBC.

Mustafa Abdul Jalil told the BBC that Saif al-Islam and Mutassim Gaddafi had been blocking the town's surrender.

Earlier, rebels said negotiations for Bani Walid's surrender had broken down and an assault was imminent.

But Mr Abdul Jalil said talks would continue until Saturday's deadline.

Meanwhile, a senior anti-Gaddafi commander is demanding an apology from the UK and the US for their role in his capture and torture in Libya in 2004.

-BBC
 
Kukaa madarakani kwa muda mrefu mpaka kujifikiria kuwa ni watawala wateule na ile "nji " ya Libya ni mali yao. Kasheshe lilipoanza Gaddafi angejaribu kutumia hekima na sio kujifanya yeye ni kisiki kisichong'oleweka. Mara hii imekula kwake!

Hivi matokeo ya hii vita yanalingana na gharama za kumuacha Gadafi awepo madarakani? Tusipende kuwa na Roho za ubaya namna hii. Sometime nafikiria watu waonyesha misimamo kutokana na stress zetu za hapa Tz za viongozi kufuja nchi huku tunadhani NATO ndio suluhisho kwa kuwa yaweza simamia mabadiliko. Si mapito ya Libya yalitupitia wakati wa Cold war "'Russia'' walifanikiwa kuchukua mali zetu they have nothing to do with us. We are working for them all profit is repatriated through global economy of which to Libya was minimal.
 
...Tusipende kuwa na Roho za ubaya namna hii...
Mi nafikiria Gaddafi na serikali yake ndie wenye roho za ubaya. Hivi Gaddafi yeye ni Mungu ambaye hawezi kukosolewa? Bila Gaddafi NATO wasingepata sababu za kirahisi za kufanya wayafanyayo huko Libya. Nawashangaa watu wanaojifanya hawataki kukubali kwamba Gaddafi alikuwa amewakumbatia na kufanya biashara na hao hao NATO kwa miaka nenda rudi!
 
.......

Askari kanzu nalazimika kukufananisha na Maralia Sugu...

Umekuwa unawatetea waasi kila kukicha, lakini leo naamua kukukumbusha kuwa uasi ulikuwapo tangu hapo mwanzo kwa mujibu wa Biblia.

Kuna walioasi huko mbinguni na kupelekea kutimuliwa.

Je ikiwa Mungu tu alishindwa kuwavumilia waasi, je Gadaffi hiyo busara unayomtakia angeitoa wapi?
 
Huyu jamaa mpumbaf kabisa sasa kama watoto wa Ghadaffi wameshaondoka bado anataka kushambulia ili iweje?...Kuna kipi kinachofichwa hapa?

Si walisema Ghadaffi amewazingira anataka kuwamaliza kule Benghazi wakaomba NATO ije kuwasaidia, sasa wao wanachokifanya Bani Walid na Sirte kinatofauti gani na Ghadaffi?
 
Kukaa madarakani kwa muda mrefu mpaka kujifikiria kuwa ni watawala wateule na ile "nji " ya Libya ni mali yao. Kasheshe lilipoanza Gaddafi angejaribu kutumia hekima na sio kujifanya yeye ni kisiki kisichong'oleweka. Mara hii imekula kwake!

MIAFRIKA ndivyo tulivyo...tuna laana sio bure unakuta mtu mzima anasema ooh Ghadaff mbaya ukimuuliza wewe ambae chama kimoja kinakutawala miaka 50, una maji? umeme? vipi matibabu anaanza kulalama tuuuu hana la kusema!! Libya is by far better than some parts of Europe in terms of life standards lakini unakuta watu wana chuki tuuu ya wivu na husda...watu wa Libya wenyewe wanajua Ghadaff amewatoa mbali sana na wanampenda haya mambwa NATO...YANAUA WAAFRIKA WENZETU MIJITU MINGNE INASHANGILIA!!!
 
Wewe ni mwendawazimu au...?
 
Head of Gaddafi's security brigade in Niger -officials
Mon Sep 5, 2011 2:19pm GMT

AGADEZ, Niger, Sept 5 (Reuters) - The head of Muammar Gaddafi's security brigades, Mansour Dhao, has crossed into Niger from Libya and is due to travel on to the Nigerien capital, Niamey, two Nigerien officials said on Monday.

The officials, who asked not to be named, said Dhao and about a dozen other Libyans crossed into Niger on Sunday after several days of talks while they waited at the border.
(Reporting by Abdoulaye Massalatchi in Agadez and Nathalie Prevost in Niamey; writing by David Lewis)

Reuters
 
Kukaa madarakani kwa muda mrefu mpaka kujifikiria kuwa ni watawala wateule na ile "nji " ya Libya ni mali yao. Kasheshe lilipoanza Gaddafi angejaribu kutumia hekima na sio kujifanya yeye ni kisiki kisichong'oleweka. Mara hii imekula kwake!
Mkuu.
Kigezo chako hapa ni domokrasia ya US na West? Muhula mmoja, miwili,mitatu?

Kubadilisha rais, waziri mkuu ndio kipimo pekee cha domokrasia?

Au kuwa na vyama viwili (vingi)? Nani haelewi kuwa US, UK, France mbali na kuwa na siasa za maigizo, serikali zinaendeshwa puta na corparationists na uchumi na mahela yote yanamilikiwa na 1% 3% ya top layer na kuwaacha raia wa kawaida na madeni yanayowatia stress na kuwafanya wafanye mambo ya ajabu ajabu tu.

Hapa kwetu, tokea TANU na CCM, tena tukalazimishwa multiparty systerm na IMF na World bank ili wakwapue mashirika ya umma na utajiri wa TZ (utandawizi na ubinafsishaji), Ameoka Ali Mwinyi na timu yake, Kaingia Mkapa na timu yake, na sasa yupo baba Ridhwani kila timu na kiongozi ikitoka inaondoka na "chukua chako mapema". Imetusaidia vipi sisi wananchi wa kawaida hili DOMOKRASIA zaidi ya kumalizia hasira kwenye key board?

Kinyume chake, Gaddafi ana record mkuu ya kuitoa Libya katika mashimo na kuipandisha juu ya mlima..kama sisi tulipopandisha bendera ya uhuru wa karatasi juu ya mlima wa Kilimanjaro.

Kulingana na system ya kimadaraka aliyotumia Gaddafi wananchi wanashiri moja kwa moja kupitia commities na congresses na kila mwananchi ananuafaika na rasilimali za nchi. Personally, nisingekuwa na kigugumizi kukubali Gaddafi awe rais wa maisha, au mfalme kwa nchi yetu. Mbali na mapungufu yake, The man has performed and delivered...in fact no one else among politicians in recent history has achieved/ accomplished what Gaddafi has done.

Wakati sipingi US na West kufuata mifumo ya siasa wanayoipenda na kujiamulia, sifurahi hata kidogo kuona wababe hawa wanahubiria nchi na mataifa mengine kuwa zifuate mifumo yao na domokrasia yao. Na undumikuwili wao ndio hasa unaorudisha nyuma juhudi za wananchi katika nchi mbali abali kufikia kujenga jamii wanazozitaka.

Kwa utendaji ambao Gaddafi ameuonesha sio kwa Libya tu bali hata kwa Afrika, kwa kukaa miaka 42 bado mimi sioni cha kumlaumu. Hata AU kukataa kumpa muhula mwengine wa uongozi walifanya makosa ambayo sasa watajutia kwani sasa kutokana na sakata la Libya AU imeshahasiwa. Gaddafi alipasa kuongoza AU kwa miaka at least 10. lol, cheers,mkuu.
 
Mkuu.
Kigezo chako hapa ni domokrasia ya US na West? Muhula mmoja, miwili,mitatu?

Kubadilisha rais, waziri mkuu ndio kipimo pekee cha domokrasia?...
Sijazungumzia domokrezia ya US wala West. Mfano (na huu ni mfano tu), je unakubali kutawaliwa na wazazi wako kwa miaka 42 (wakuamlie kutokuvuta sigara, kukuchapa viboko etc.)? Hayo ndio maisha? Huyu Gaddafi ni nani aliyempa haki ya kutawala kwa miaka 42?
 

Yes, sir. ninakubali. Mimi nitabaki mtoto kwao hata kama nitakuwa na miaka 67.

Lakini Gaddafi alishaanza reforms hasa kupitia Saif , au taasisi ya Saif...sasa walibya walikuwa wamuunge mkono huyu dogo ili awe na ushawishi zaidi wa kupunguza ukaidi wa baba yake..mabadiliko hayaji kwa siku moja na katika hali inayoendelea Libya ni kuwa atatoka mzalendo, ataingia kibaraka.

Kuna ule msemo wa kuruka kutoka katika karai unaangukia katika moto.

Nilipata kusikia masimulizi kuwa Gaddafi ni mteule wa Mungu.

Yeye ni king of kings na mlezi wa waafrika wote.
 
Yes, sir. ninakubali. Mimi nitabaki mtoto kwao hata kama nitakuwa na miaka 67...
Swala sio kubaki kuwa mtoto kwao (wazazi). Wote tutabaki hivyo. Swala ni kuwa na uhuru (kujiamlia kuondoka nyumbani na kuanza maisha yako, i.e kuoa, na kutengeneza familia etc) Sidhani kama utakubali ufikie miaka 67 na bado tu uhuru wako wa kujiamlia maisha bado unatawaliwa na wazazi. Huo utakua ni uoga uliokubuhu au nidhamu isiyo ya dhati!
 

Kama mzazi wangu atajibebesha jukumu hilo ,mimi nitakubali aniamulie maisha. Najua itafika siku yeye atakuwa hajiwezi, hapo itakuwa zamu yangu kumuamulia maisha. Au huku mitaani uswahili haiko hivyo...mzazi anapokuwa hajiwezi anamfuata mtoto na mtoto ndio anakuwa king?

Ulaya ndio wana hayo mambo ya mimi sikubali, akifika 16, 18 dogo anakitoa na wazazi wanaishia nyumba za kulelea vizee.

Walibya wangemstahamilia mzee wa watu kwa miaka 3, 5 basi hiyo Libya waliyokuwa na ndoto yao wangeipata bila ya kudondoshewa mabomu. Sasa wanapoteza mali yao, uhuru wao na utu wao lakini baya zaidi ni kuwa wanakubali mzee wao adhalilishwe. Hasara iliyoje!!!

Wazazi wa aina ya Gaddafi ambao wanajibebesha jukumu la kuwalinda raia wao na matai waharibifu ni tunu katika dunia hii. Unaweza kuwahesabu kwa vidole.
 
Duhu!!
 
Libyan Islamist says interim council should quit

A Libyan Islamist military commander who helped defend Benghazi against Muammar Gaddafi's forces has called on the interim cabinet to resign because they are "remnants of the old regime".
In an early sign of divisions among the victors in Libya's six-month civil war, Ismail al-Salabi also took a swipe at secular groups he said were trying to give Islamists a bad name and create political strife that would only benefit Gaddafi.

Salabi leads the February 17 brigade which many Libyans credit with the successful last-ditch defence of Benghazi, where the uprising began on that date. Only later did NATO air power tip the balance in favour of the largely untrained rebel forces.

"The role of the executive committee is no longer required because they are remnants of the old regime. They should all resign, starting from the head of the pyramid all the way down," Salabi told Reuters in the eastern city.

CORRECTED-INTERVIEW-Libyan Islamist says interim council should quit | News by Country | Reuters
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…