Kadhia hiyo inahitaji uthibitisho ili isiwe watu wanavumisha kwa ajili ya maslahi ama chuki binafsi. Jana niliona taarifa ya habari ITV ikionyesha mapokezi ya watoto 20 waliopelekwa india kufanyiwa upasuaji wa moyo wakirudi salama baada ya operesheni zao kuwa za mafanikio. aidha wazazi na wasindikizaji pomoja na baadhi ya watoto walisikika wakishukuru wahisani waliowafadhili upasuaji huo.. wakiwemo Lions club (host).
Huku mmoja wa waratibu wa mpango huo wa lions club akisisitiza kuwa gharama za kufanikisha upasuaji huo hukusanywa kutoka kwa wafadhili mbalimbali, na kukubali kwa hospitali inayotoa tiba hiyo kutoza malipo nafuu. Kwa maelezo hayo nadhani kuna upungufu mkubwa wa ukweli wa madai hayo. tutafakari