Movic Evara
Senior Member
- Jan 31, 2018
- 197
- 431
Wakati mnaanzisha combination zenu zisizoeleweka, tuliwauliza mmejiandaa? Mlipounda tahsusi kama vile Arabic, Music & Sports (ArMS) tuliwauliza serikali imeandaa walimu wa Arabic, walimu wa Music na walimu wa michezo wa kutosha? Tuliuliza kwa sababu tunajua vyuo vyetu haviandai walimu wa masomo haya. Pale UDSM vijana wa FPA wanasoma Music lakini hawaandaliwi kuwa walimu. Hata TASuBa vijana wanasoma Music lakini hawaandaliwi kuwa walimu.
Sasa huyu mtoto wa kidato cha 5 atafundishwa music na nani? Na hata tukichukua vijana wote wanaosoma muziki vyuo mbalimbali tuwafanye walimu wa "crush program" bado hawatoshelezi mahitaji ya nchi nzima. Lakini badala ya kutusikiliza mkatuita wachochezi na kusema tunazua taharuki. Haya sasa kiko wapi? Mbona mmefyata mkia dakika za mwanzoni tu?
Kwanza mmesumbua shule binafsi kwa sababu mlizilazimisha ziajiri walimu wa tahsusi mpya na wakatii. Leo mnasema mtaala mpya umesitishwa, wale waalimu waende wapi? Hiyo hasara analipa nani?
Pili, Mmetesa watoto wetu bila sababu. Kati ya watoto yatima ninaowasomesha kuna mmoja alipangiwa French, Arabic & Chinese (FArCh) lakini tangu aripoti shuleni hakuna alichofundishwa. Hakuna Mwalimu wa Kifaransa, Kiarabu wala Kichina. Saivi wanaambiwa wabadili tahsusi waende HKL, HGK au HGL. Serikali ilikurupuka nini kuwapangia watoto shule kama ilikua haijajiandaa vya kutosha?
Kwanini elimu ya nchi hii inachezewa na kila kiongozi anayejisikia kufanya hivyo? Tangu enzi za Mungai tunarushwarushwa tu kama gari bovu. Mara huyu afute michezo, mwingine aunganishe Physics & Chemistry, mwingine afute Kilimo, mwingine aanzishe tahsusi zisizoeleweka. Yani elimu yetu imekua sandakalawe, kila kiongozi analeta anachojisikia.
Marehemu Mkapa aliwahi kusema tunahitaji mjadala wa kitaifa kuhusu elimu yetu. Kama kweli tunataka elimu yenye tija na ushindani kimataifa tuweke public forums watu watoe maoni yao, wataalamu wayachukue na kuyachuja na kuamua kwa mustakabali wa taifa. Tukiendelea kuruhusu hawa viongozi waamue kwa matashi yao, tutapotea.!