Atakuwa anazunguka na ule wimbo wa "Tanzania ni donor country" kichwani mwake.
Acha kupotosha watu wewe dogo,mradi wa bomba la mafuta umechelewa sababu ya makubaliano kati ya Total na serikali ya uganda kuchukua muda mrefu. Kwani mafuta yameanza kuchimbwa huko Uganda?Nimecheka kwa nguvu hiki unachoandika hapa Paskali, unazungumzia faida ya SGR kwani hata imekamilika hiyo SGR? Nakumbuka ile siku ya uzinduzi wa bomba la mafuta Chongoleani Tanga, nilimsikia rais akipiga faida ya kodi ya mapipa ya mafuta tutakayoanza kupata kuanzia hii 2020 mradi ukishakamilika. Akawa anaoonyesha na sehemu pesa zitaiingia baada ya 2020, watu wakawa wanarukaruka kama wendawazimu. Kwakuwa nilikuwa namjua Museveni nitapeli nilikuwa nacheka kwa nguvu. Leo hii yako wapi kuhusu mradi wa bomba la mafuta, zaidi ya juzi Museveni kuja kumpigia kampeni Magufuli kwa kisingizio cha huo mradi? Unachoongea hapa Paskali ni zile porojo za ma Motivational speakers.
Mbona inajulikana upo Tanzania. Ndio maana moja kwa moja watalii wanatua kIA ili kupanda mlima kilimanjaro.
Ukweli ndio huo.Japo sio kweli kuwa asilimia kubwa ya mzigo unaopita bandari ya Dar ni wa Congo DRC, mzigo mkubwa wa Dar Port ni unaovuka Tunduma!. Ila kwenye long plan ya SGR yetu itafika Kigoma.
P
Ile 2017 kule Chongoleani Tanga mpaka wakapatanishwa Ruge RIP na Makonda, hao wazungu wa Total walikuwepo, mbele ya marais Museveni na Magufuli tukaambiwa 2020 mradi utakuwa umekamilika. Sasa ww haya maelezo yako ya mfukoni unatoa wapi? Kama mafuta yalikuwa hayajaanza kuchimbwa, na makubaliano na Total yalikuwa bado, lile igizo pale Chongoleani lilikuwa la nini?Acha kupotosha watu wewe dogo,mradi wa bomba la mafuta umechelewa sababu ya makubaliano kati ya Total na serikali ya uganda kuchukua muda mrefu. Kwani mafuta yameanza kuchimbwa huko Uganda?
Sisi tunanufaika bomba kupita hapa Tanzania ili mafuta yasafirishwe,sasa unaanza kuleta lawama hata mafuta hayajaanza kuchimbwa,unatakaka kusafirisha hewa?
Hizi habari wadanganye wanaufipa unaowaongoza kama kamanda mkuu.Wakenya hawana akili hiyo ya kusema mlima Kilimanjaro uko Kenya. Wao wanasema fika Kenya uone mlima Kilimanjaro, na kweli ukiwa Kenya unaona mlima Kilimanjaro. Na ukitaka kupanda unapewa bei yake na protocol zake za kupandia huo mlima. Simple hivyo yaani.
Mkuu tindo , kwanza nakiri mimi ni mywaji wa pombe, na huwa natembea sana na Joni Mtembezi alama nyeusi, uzuri wa Joni Mtembezi, hata ukilewa vipi, hauamki nazo, kwasababu, stimu yake haikai kwenye kimiminika kama bia hivyo kujaa tumboni, Joni Mtembezi ni vapour, stimu yake inaingia kwenye damu na ku evaporates kwa kupumua, hivyo unaamka fit na kusali misa ya kwanza.Paskali nahisi umemka umelewa, umeamka na mada za propaganda si propaganda bali vichekesho vitupu. SGR yetu kipande cha Dar-Moro tuliambiwa mwezi wa Nov 2019 kitakuwa kimekamilika, hadi sasa hakijakamilika na tunaambiwa kitakamilika Aprili 2021! Na kuna tetesi kuwa fedha zinasumbua kwenye huo mradi ndio maana simu ilipigwa kwa rais wa China. Unazungumzia mradi kufika Mwanza huku hata kipande cha 300km kimechekua zaidi ya 3yrs na bado hakijamilika!
Hao Uganda wana mradi wa bomba la mafuta, ilisainiwa toka 2017, na matarajio ingekamilika 2020. Lakini mpaka sasa haujaanza na hata kama ni kuanza ni kwa kusuasua. Sasa hapo unaoongelea mambo ya mradi wa SGR si vichekesho hivyo? Nikikumbuka ule utapeli wa sarafu ya pamoja ya E. Africa, kisha nikiona hizi mada zako kuhusu hawa matapeli, nacheka kwa nguvu.
Bwahaaa bwahaaaa, nimecheka kwa nguvu, anayemiliki majengo ya urithi anampomcheka aliyepanga. Kwani mlipoanza mbwembwe na huo mradi wa SGR mlidhani ni kukaanga mayai?
Hii ya zito ndio unaileta hapa .post ya snitchUkweli ndio huo.View attachment 1660132
Fuatilia mambo kwa ukaribu,wazungu wa Total walikuwepo Chongoleani,ila zilitokea sintofahamu ambazo zilisababisha kuchelewa kuchimba mafuta. Hivyo sisi kama Tanzania huwezi kulaumu eti mradi umecheleweshwa na serikali yetu.Ile 2017 kule Chongoleani Tanga mpaka wakapatanishwa Ruge RIP na Makonda, hao wazungu wa Total walikuwepo, mbele ya marais Museveni na Magufuli tukaambiwa 2020 mradi utakuwa umekamilika. Sasa ww haya maelezo yako ya mfukoni unatoa wapi? Kama mafuta yalikuwa hayajaanza kuchimbwa, na makubaliano na Total yalikuwa bado, lile igizo pale Chongoleani lilikuwa la nini?
Mweshimiwa kabisa , naomba uone mfano huu:Ni jambo jema!
Lakini sidhani kama tuna mashindano na Kenya mkuu Pascal!
Mkuu, kwanza nimefurahi sana kwa kutoa hoja kwa data, hapa unazungumzia mzigo unaopita Central Corridor, the busiest transit border kwa mizigo nchini Tanzania, mzigo unaopita the Southern Corridor, ambao unapita border ya Tunduma. Japo Beggars Can Not Be Choosers, Tuache Siasa Kwenye Uchumi. We Have to Choose Or. ..Ukweli ndio huo.View attachment 1660132
Tanzania SGR yenyewe inasuasua sasa hivi hawana pesa tena! Mwanza kwenyewe itafika lini? Magufuli ataondoka madarakani na kuiacha hata TABORA haitafika! I can bet for that!Wanadodi,
Leo nimepata fursa ya kuendelea na zile makala zangu za kwa Maslahi ya Taifa, leo nikianzia kuibuka kwa fursa mpya kwenye reli ya SGR ya Tanzania, karibu.
Wakati Tanzania tukiendelea na ujenzi wa reli yetu ya SGR, shughuli nzito kwenye SGR sio ujenzi, bali ni kuiendesha kwa faida. Ili SGR iendeshwe kwa faida, ni lazima iwe na kitu kinachoitwa linkages, yaani muunganisho kati ya nchi moja na nyingine, ili hiyo SGR ipate mzigo wa kushiba na ku operate kwa faida.
Kwa nchi za Afrika Mashariki, Kenya ikitumia mtindo wa "ujanja kuwahi", ikawa ndio nchi ya kwanza kuchangamkia fursa hivyo ikajenga SGR ya Mombasa-Nairobi-Naivasha-Malaba, ili mzigo wa Uganda na Rwanda upitie bandari ya Mombasa, na Uganda ingejenga SGR kupokea mzigo wake na wa Rwanda na kuufikisha Kigali. Hivyo the linkaje ya mzigo wa Uganda na Rwanda, ndio roho ya SGR ya Kenya, Mchina kupitia benki yake ya EXIM akakubali kugharimia kila kitu.
Kumbe "ujanja nsi kuwahi, ni kupata", JPM baada tuu ya kuchaguliwa,ziara yake ya kwanza nje ya nchi, ni kutembelea Rwanda, wakakubaliana SGR ya Tanzania itaungana na ya Rwanda. Hivyo kitendo tuu cha kukubaliana SGR ya Tanzania itajiunga na Rwanda, ile linkages ya SGR ya Uganda kwenda Rwanda, ikakatika, hivyo SGR ya Kenya kuunga Uganda haitakuwa na faida, hali hiyo ikikapelekea mfadhili kujitoa kuendeleza SGR ya Kenya sasa itaishia Naivasha, na hakuna funding tena ku fund SGR ya Uganda!.
Baada ya mchina kugoma kugharimia SGR ya Uganda, MU7, nae kaamua kumfuatilisha JPM kwa kuamua kujenga SGR ya Uganda hata kama Kenya anasuasua. Uamuzi huu wa Uganda kujenga SGR yake bila kuitegemea Kenya ni fursa nyingine kubwa kwa SGR ya Tanzania na Bandari ya Dar es Salaam kubeba mzigo wote wa Uganda.
Ili sisi Tanzania kuweza kuichangamkia fursa hii mpya, sasa hapa ndio "ujanja kuwahi", kwa kujenga SGR ya Mwanza fasta, ili mzigo wa Uganda ushuke Dar, ukimbizwe Mwanza, uvushwe ziwa Victoria hadi Uganda. Hili likifanyika, sio tuu, Bandari ya Dar itabeba cargo ya Uganda tuu, bali cargo kutoka South Sudan na North Eastern DR Congo itapitia bandari ya Dar es Salaam kupelekwa Mwanza. Changamoto pekee, in umbali wa route hii, kama italipa, na changamoto ya hatari zaidi, ni bada ya MU7 kuamua kujenga SGR, Kenya anaweza na yeye kuamua kukijenga kipande cha Naivasha-Malaba.
Background.
Taarifa za Uganda kujenga nmezisoma hapa Uganda plans to go it alone and build 2,700km-long standard gauge railway.
SGR ndio kipimo cha the economic super power of EAC, hivyo ni vita kubwa.
Reli ya SGR: Je, Tujifunze kwa wenzetu Kenya kuepusha SGR yetu kuwa ‘A White Elephant’? Wenzetu yameshawakuta...
Wanabodi Kuna msemo usemao "ukiona mwenzako ananyolewa, wewe tia maji tia maji" Tanzania tunajenga reli ya SGR, wenzetu Kenya wametangulia, ila reli yao imeanza kwa kuwa ni a white elephant. Jee kuna haja ya sisi Watanzania tujifunze kwa wenzetu, kuiepusha reli yetu kuwa tembo mweupe, au wao...www.jamiiforums.com
The SGR War: MagufuliKagame vs MuseveniKenyatta ni Vita Kubwa!. Who Will Win, Loose or Its Win Win Situation?.
Baada ya Rais Kagame na Rais Magufuli, kukubaliana kujenga reli ya SGR kutoka Isaka kwenda Kigali, ili mizigo yote ya Rwanda, ipitie bandari ya Dar es Salaam, Isaka hadi Kigali, Rwanda, kitu ambacho kingepunguza kuitegemea bandari ya Mombasa, huku rais Museveni na na rais Kenyatta, nao...www.jamiiforums.com
The SGR War: Magufugame vs Musevenyatta ni Vita Kubwa!. It is a Win Lose War!. When One Wins, the Other Lose, No Win Win Situation!.
Wanabodi, Rais Magufuli aliposema vita vya uchumi ni mbaya ni kuliko vita vya kawaida, alikuwa right. Hili ni bandiko kuhusu vita kubwa, ambayo mimi nimeipa jina la Magufugame vs Musevenyatta. Magufugame vs Musevenyata ni Vita Kubwa ya Kiuchumi!. Its a Win Lose War!. When One Wins, The Other...www.jamiiforums.com
The SGR War: Magufugame vs Musevenyatta ni Vita Kubwa!. It is a Win Lose War!. When One Wins, the Other Lose, No Win Win Situation!.
Wanabodi, Rais Magufuli aliposema vita vya uchumi ni mbaya ni kuliko vita vya kawaida, alikuwa right. Hili ni bandiko kuhusu vita kubwa, ambayo mimi nimeipa jina la Magufugame vs Musevenyatta. Magufugame vs Musevenyata ni Vita Kubwa ya Kiuchumi!. Its a Win Lose War!. When One Wins, The Other...www.jamiiforums.com
My Take
Kama tumeweza kuwapiga Tanchi kwenye SGR ya kuunganisha na Rwanda, kisha tukawapiga Tanchi kwenye bomba la mafuta la Uganga, Tanzania tukifanikiwa kuifikisha SGR yetu, Mwanza, hadi Kigoma, na pia tukajenga SGR to Tunduma, Tanzania ndio itakuwa the super power of EAC Region, na kama tukiifanya Dar Port kuwa a free port kwa baadhi ya bidhaa, with The AfCFTA in place!, Tanzania will fly!, no one will catch us!.
Nawatakia Jumapili Njema.
Paskali
Abiria pekee haiwezi kukupa faida kwenye SGR, na hata mizigo ikiwa michache bado ni tatizo kubwa, hasa wenzetu ambao pesa ya ujenzi yote ni mkopo. Unapo kopa unakuwa na tatizo zaidi: Unanyimwa uhuru kuweza kuendesha biashara nje ya makubaliano ya mkopo.Utajikomba sana mwaka huu lkn hupati uteuzi hata wa mjumbe wa nyumba kumi.
Kwa taarifa yako Kenya SGR tayari ishaanza kuingiza kipato,wananchi wa Kenya wamesha anza kuonja manufaa ya SGR .
Tangu mwezi wa November SGR ilikuwa imeshajaa hadi januari kwa wingi wa abiria.
Mkuu tindo , kwanza nakiri mimi ni mywaji wa pombe, na huwa natembea sana na Joni Mtembezi alama nyeusi, uzuri wa Joni Mtembezi, hata ukilewa vipi, hauamki nazo, kwasababu, stimu yake haikai kwenye kimiminika kama bia hivyo kujaa tumboni, Joni Mtembezi ni vapour, stimu yake inaingia kwenye damu na ku evaporates kwa kupumua, hivyo unaamka fit na kusali misa ya kwanza.
Ni kweli SGR yetu kipande cha Dar-Moro kimechelewa kukamilika due to janga la Corona ambalo limeathiri kila kitu hadi upatikanaji wa fedha. Ile simu ya China, sio ilipigwa, tulipigiwa sisi!, na ombi la fedha za ku fund SGR sio ombi jipya, ni kukumbushia tuu kwasababu the original plan ilikuwa ni China kuifund SGR yote 100% kwa masharti ya kui oparates hadi deni lilipwe lote ndipo wakabidhi, na catchment area yake ilikuwa ni bandari ya Bagamoyo. Kwa vile kiukweli kabisa, sisi kama sisi, hatuna uwezo wa kuitandaza SGR Tanzania nzima, hivyo ile kanunu ya ili ule ni lazia uliwe, msije kushangaa mradi wa bandari ya Bagamoyo ukaendelea na Mchina akagharimia SGR yote iliyobakia nchi nzima.
P
Unafahamu pesa tuliyokwisha lipa au ubwabwaja tuTanzania SGR yenyewe inasuasua sasa hivi hawana pesa tena! Mwanza kwenyewe itafika lini? Magufuli ataondoka madarakani na kuiacha hata TABORA haitafika! I can bet for that!
We hujamuelewa Pascal umejipu kwa pupa anazungumzia mzigo.Hata huku Meter gauge ya TRC kwenda Arusha na Moshi imejaa mpaka Jan huko sembese SGR ya huko.Utajikomba sana mwaka huu lkn hupati uteuzi hata wa mjumbe wa nyumba kumi.
Kwa taarifa yako Kenya SGR tayari ishaanza kuingiza kipato,wananchi wa Kenya wamesha anza kuonja manufaa ya SGR .
Tangu mwezi wa November SGR ilikuwa imeshajaa hadi januari kwa wingi wa abiria.
Fuatilia mambo kwa ukaribu,wazungu wa Total walikuwepo Chongoleani,ila zilitokea sintofahamu ambazo zilisababisha kuchelewa kuchimba mafuta. Hivyo sisi kama Tanzania huwezi kulaumu eti mradi umecheleweshwa na serikali yetu.
Hapa tunaongelea usafiri kwa ujumlaWe hujamuelewa Pascal umejipu kwa pupa anazungumzia mzigo.Hata huku Meter gauge ya TRC kwenda Arusha na Moshi imejaa mpaka Jan huko sembese SGR ya huko.
Mkuu tindo , kwanza hoja iliyo mezani ni SGR, bomba la mafuta ni something else, ila kwa vile mimi na Total ni dam dam, nitakuelimisha kidogo kuhusu kuchelewa kwa mradi huu, has nothing with us, mradi huu kwanza umechelewa na Uganda kwa kampuni ya Tullow kushindwa kuelewana na Total kuhusu mgawanyo wa mapato, hili limemalizika, Total imeinunua kampuni ya Tullow 100%, sasa mambo yanaendelea. Ila kitakachochelewesha mradi kuanza, ni kitu kinachoitwa "price elasticity of demand", wakati ule barrel la crude oil ilikuwa $ 60 sasa ni $ 16 per barrel, hivyo sasa wasoma trends wana soma kwa makini economic projections kama price itakuja ku stabilize in a near future, ndipo ujenzi uanze, vinginevyo kwa bei hiyo ya $ 16 per barrel, haiwezi kulipa gharama za extraction, treatment and transport, itakuwa ni hasara, hivyo the final ivestment decision bado haijasainiwa!.Nimecheka kwa nguvu hiki unachoandika hapa Paskali, unazungumzia faida ya SGR kwani hata imekamilika hiyo SGR? Nakumbuka ile siku ya uzinduzi wa bomba la mafuta Chongoleani Tanga, nilimsikia rais akipiga faida ya kodi ya mapipa ya mafuta tutakayoanza kupata kuanzia hii 2020 mradi ukishakamilika. Akawa anaoonyesha na sehemu pesa zitaiingia baada ya 2020, watu wakawa wanarukaruka kama wendawazimu. Kwakuwa nilikuwa namjua Museveni nitapeli nilikuwa nacheka kwa nguvu. Leo hii yako wapi kuhusu mradi wa bomba la mafuta, zaidi ya juzi Museveni kuja kumpigia kampeni Magufuli kwa kisingizio cha huo mradi? Unachoongea hapa Paskali ni zile porojo za ma Motivational speakers.