The Standard of the ''Reasonable Man'' Kiwango Cha Fikra ya Mtu wa Kawaida Uteuzi wa Mkurugenzi wa ZEC

The Standard of the ''Reasonable Man'' Kiwango Cha Fikra ya Mtu wa Kawaida Uteuzi wa Mkurugenzi wa ZEC

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
THE STANDARD OF THE REASONABLE MAN’’ (KIWANGO CHA FIKRA YA MTU WA KAWAIDA): MJADALA WA UTEUZI WA MKURUGENZI WA TUME YA UCHAGUZI ZANZIBAR

Lord Denning wanasheria wanamjua sana kwa hukumu zake.

Lord Denning kamueleza ‘’Reasonable Man yaani, ‘’Mtu wa Kawaida,’’ ni mtu gani.

Lord Denning kamweleza kwa kiwango ambacho hakimpi shida mtu yeyote kumtambua mtu huyu ni nani.

Kiwango hiki cha utambuzi kinamweleza mtu huyu na mimi hapa nitaleta maelezo katika mazingira ya hapa kwetu kuwa, ‘’Mtu wa Kawaida,’’ ni yule mwananchi katika barza ya kahawa mtaani mahali kama Manzese Uzuri au Magomeni Makuti na kweninge mfano wa huo ambae kwa kuongeza kusema si msomi, la hasha, ni mtu wa kawaida tu pengine ana ubao wake sokoni anauza nazi au ana genge mtaani anauza nyanya.

Huyu ndiye ‘’Mtu wa Kawaida.’’

Unapotoa uamuzi kwa jambo lolote kupima uamuzi uko sawa au tenge tumia kiwango cha mwananchi huyu wa kawada kuamua.

Tumia ubongo wa mwananchi huyu mkazi wa barza ya kahawa kupima yote usomayo na kusikia katika mjadala wa uteuzi wa Mkurugenzi wa ZEC.

PICHA: Kulia ni Lord Denning.

1668802575503.png

1668804066163.png

Lord Denning
 
Watu wa kawaida umetuacha. Pengine ukitumia lugha ya kawaida tunaweza kwenda sambamba. Unamaanisha nini mkongwe
 
Watu wa kawaida umetuacha. Pengine ukitumia lugha ya kawaida tunaweza kwenda sambamba. Unamaanisha nini mkongwe
Baba...
Rudia kusoma tena kwa taratibu utaelewa.

Mathalan kama mtu akichukua jiwe akalivurumisha katika kundi la watu kwa vyovyote litampiga mtu.

Ikiwa mtu huyu atakamatwa na kushitakiwa na katika kujitete akadai kuwa hakujua kuwa jiwe lile litamuumiza mtu nani atamuamini.

Hatoweza kuaminika kwani kwa kiwango cha kili ya mtu yeyote wa kawaida kitendo hicho atajua kuwa kina madhara.
 
Back
Top Bottom