The Tanzanian Shilling has been gaining against major currencies

The Tanzanian Shilling has been gaining against major currencies

Dua

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2006
Posts
3,236
Reaction score
669
Sarafu ya Tanzania imekuwa ikipata nguvu kila uchwao kutokana na juhudi za makusudi za kukuza uchumi wa Tanzania zinazofanywa na Serikali ya awamu ya 5.

''Tanzania’s shilling is expected to gain as inflows increase from tourism and agriculture. Commercial banks quoted the shilling at 2,292/2,302 on Thursday, up from 2,293 to 2,303 recorded last week, a trader in at Dar es Salaam told Reuters. "The shilling has been stable for the last two weeks and it keeps appreciating,” he said. “We expect more stability and further appreciation next week due to increase in inflows from the tourism sector as we are in the tourism season and from agriculture exports.”

Kama ada mwezi wa tisa mategemeo ya kuanza ku-reserve bullions ndio itakuwa ''another game changer'' Tanzania tunasonga mbele, wale wezi-koko watafute nchi za kukimbilia maana huwezi kukaa Tanzania kwa kutegemea wizi wa kisasa. Hongera zote ziende kwenye awamu ya 5.
 
Ndio mjue kilimo ni muhimu sana katika nchi hii ingawa kinapewa uzito mdogo.
 
hapana mkuu hela yetu ipo chini bado kwakweli tusilete maneno mengi kwenye mambo ya pesa aisee bado ipo chini mzee

msifie mzee baba kwa mambo mengine ila usimfie mpaka yeye mwenyewe akanuna mwishoni utaonekana mnafki
 
Kitu usichokijua wewe ni kwamba hizo sarafu kubwa zinakumbwa na mgogoro kwa hivi sasa..mfano GBP kuna ishu ya Brexit so imeporomoka sana tangu 2016, USD inasumbuliwa na mgogoro wa kibiashara wa China na US n.k
Tukirudi kwenye TSH hebu ilinganishe na sarafu za kikanda yan EAC halafu useme huo upuuzi wako wa kuimba mapambio ya Lumumba
 
Pamoja na mengi yatokeao Tanzania. Kupunguza tatizo la bihashara haramu za madawa ya kulevya, meno ya tembo na wizi mwingi ktk sector za nchi zimesaidia sana pesa kuimarika pia. Kingine walitakiwa wajitaidi ktk uzalishaji wa cement na usambazaji, cement imekuwa ishu wakati mwingine na kufanya uchumi kuwa na kugawana na wazalishaji wa njeee
 
Fursa hiyo ingia mt4 buy tsh/usd
 
Hivi jumatano hii mafuta yatapañda au yanashuka.
 
Kitu usichokijua wewe ni kwamba hizo sarafu kubwa zinakumbwa na mgogoro kwa hivi sasa..mfano GBP kuna ishu ya Brexit so imeporomoka sana tangu 2016, USD inasumbuliwa na mgogoro wa kibiashara wa China na US n.k
Tukirudi kwenye TSH hebu ilinganishe na sarafu za kikanda yan EAC halafu useme huo upuuzi wako wa kuimba mapambio ya Lumumba

Hujielewi, pesa inashuka au kupanda kutokana na uchumi wako mwenyewe na mara nyingi pesa zote zinapimwa kwa kutumia USD na Gold. Kama unafuatilia haya mambo kwanza lazima ufahamu zipi ni major currencies then angalia bei ya Gold. Kwa haraka haraka tu tofauti ya bei ya gold ya July to August ni karibu USD 200 na ushee kwa ounce. Ngoja baada ya mwezi Sept tukimaliza kuanza na sisi ku-reserve gold utaona shillingi yetu itaendelea kupata nguvu against all major currencies.
 
Back
Top Bottom