Ulijuaje au yamekukuta, uko mbali ningekupa 5, hiyo shortlist ya Things women do kama shirikishi vile kwa sababu kumpata mwanamke aliyekosa moja kati ya hayo tisa ni kazi kweli kweli. Yote uliyoyasema ni kweli na yanakatisha tamaa na kuwasononesha wanaume na wazazi wao. Lakini wanawake wanapaswa kujiuliza huyu baba niliyekumkuta ameshakuwa mtu mzima amefikia hali hii baada ya mchakato tena wa muda mrefu. Hebu Mwanamke jiweke kwenye viatu vya mama aliyebeba mimba miezi tisa na machungu yake, kisha akasota na mwanae kumtibu na kumlisha ili kuhakikisha anaendela kuwa hai akakosa usingizi mtoto akiugua,akajinyima yeye ili mtoto wake ashibe. Akapata presha mtoto akipata masaibu yeyote. Mtoto huyu akapelekwa shule, akaandaliwa kila siku asubuhi mavazi, chemsha kimya madaftari na kalamu, sare zilizofuliwa na kupigwa pasi, ada za shule na Tuition, kuanzia nursery hadi chuo kikuu miaka zaidi ya kumi na sita watu wanahangaika na katoto kao kisha unakuja Queen unambadilisha mtoto huyu na kumfanya wa kwako tene wa kwako peke yako na ndugu zako. Humuogopi mungu wewe, hivi unamtakia mumeo mema. Dhulma gani hii ukosefu gani shukrani. Unapaswa kuwashukuru na kuwaheshimu wazazi wa mumeo UKIONA VYAELEA VIMEUNDWA. Tafakari wewe mama unayemmiliki mmeo.