Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
''THE THREE MUSKETEERS''
Hiyo picha hapo chini nzuri sana muonekano wake.
Inawaonyesha viongozi wakiwa katika ukakamavu na fikra nzito.
Walikuwa wanafikiri nini?
Lakini linaloweza kumfikirisha mtu katika hii picha anaependa kuhangaisha kichwa chake ni historia za viongozi hawa.
Wanasema chini ya kila paa la nyumba kuna historia.
Hakika.
Kila picha ukiiangalia hutokosa cha kujifunza.
Picha hii inanikumbusha kitabu cha Alexandre Dumas, "The Three Musketeers."
Huyu Alexandre Dumas alikuwa Mfaransa mwandishi bingwa wa vitabu.
Kitabu chake kingine mashuhuri ni "The Count of Monte Cristo."
Ndani ya vitabu hivi kuna mengi yanayofanana na harakati za siasa kama zinavyochezwa Afrika.
Kuanguka na kunyanyuka.
Picha hii imenifikirisha kidogo asubuhi hii.
Lakini sifa zote zimwendee mpigaji wa picha hii.
Hii ni moja ya zile picha zinazokataa kufa.
Itatazamwa baada ya miaka 100 na mtazamaji atajiuliza, "Hawa walikuwa nani na nini historia yao?"
Itapendeza kama viongozi hawa wataandika tawasifu zao.
In Shaa Allah na ikiwa wataandika kila mmoja wao katika kitabu chake asikose kuweka picha hii.
Picha huzungumza maneno 1000.