Forgotten
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 3,518
- 10,839
Suala la Chris Brown mashabiki zake wote inabidi wajue, Chris wa sasa siyo yule wa zamani. Chris alipoteza mashabiki zake wengi kwa skendo zake za kupiga wanawake. Pia aina ya muziki anaofanya Chris Brown sasa hivi unamtenga na mashabiki wengi wasiopenda nyimbo zenye mashairi ya watu wazima (Explicit Content) tofauti na Justin Bieber ambaye nyimbo zake nyingi ni muziki unaoweza kusikilizwa na rika tofauti; Ngoma kama Intentions, Changes.umemaliza...Kuna jamaa nlkuwa namuelewesha anabisha kinoma
Chris Brown katoa nyimbo kama hizo zamani sana zikiwemo; Die Young, Beautiful People.
Sasa kama mashabiki tunapaswa kufuata muziki mzuri na siyo muziki unaotamba. Sasa hivi kuna wimbi kubwa la mumble rappers ambao nyimbo zao wanaimba kuhusu pesa, wanawake na matusi kibao ndiyo wana-hit ila hakuna cha maana wanaimba ila ukitaka muziki mzuri upo ila haupati nafasi kubwa kutokana na soko la muziki kubadilika.