Theists wa kibongo hawana pointi halafu ni wepesi mno kupanic

Theists wa kibongo hawana pointi halafu ni wepesi mno kupanic

Rule L

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2020
Posts
1,846
Reaction score
2,754
Majuzi kati nikiwa kijiweni ulitokea ubishani mkali sana juu ya uwepo wa Mungu, mimi nikiwa nahitaji kuthibitishwa uwepo wake.

Tuliongea mengi sana ila itoshe tu kusema hawa watu hawana facts kabisa, imagine mtu anakuambia kama sio Mungu ningekua sioni.

Nikauliza vipofu wao hawaamini uwepo wake au?? Wanaanza kusema kila mtu kupangiwa njia yake😌😌😌

Kulikua kuna bubu pale akasema mimi sina akili kwa kusema Mungu hayupo huyu nilimjibu kwamba apewe uwezo wakuongea na roho mtakatifu.

Ila nilijifunza kwamba kuna aina gani ya watu tulionao nchini, kwanza wao wanaamini kua anayesema Mungu hayupo ni mwendawazimu. Chakushangaza hio hoja yao hawawezi kuitetea.

Pia umaskini uliokithiri umewafanya baadhi yao kua majuha, na tumaini pekee ambalo wanalo ni kua ufalme wa mbinguni ni wao.

Baada ya kuishiwa kabisa hoja wakawa wakali eti wanipige ninamkataa Mungu, kuna jamaa pale alikua mstaarabu akawaelekeza tu kua msihangaike atapigwa na Mungu mwenyewe.


Hapa ndio nilielewa maana ya kondoo wa bwana ni nini.
 
Back
Top Bottom