Umesahau kwamba kipindi chote cha Nyerere tulisimamisha shughuli zote za uchumi ukiwemo uvunaji wa madini ili kwanza kujenga umoja wa kitaifa?, japo uchumi ulisimama lakini huoni kwamba tulijenga misingi bora ya kufikia uchumi endelevu?, leo hii taifa halina matabaka yanayotishia jamii kugawanyika kwa misingi ya kabila, eneo, rushwa wala kipato, sasa hivi ni wakati muafaka kuanza kuchimba madini kwa ajili ya taifa zima
Nyerere angekuwa jambazi angeweza kuanza kugawa utajiri wote huu kwa kwa kabila lake na watu waliomzunguka, ndiyo chanzo cha ukabila na kubaguana kama Kenya, leo ukiondoa neno la LCD, hakuna lingine Kenya inaweza kuikosoa Tanzania, kuna kila dalili kwamba ndani ya miaka kadhaa Tanzania itakuwa middle income country, je ni lini Kenya itajenga umoja wa kitaifa na kuumaliza ukabila na rushwa iliyotamalaki?, Kenya haitaweza kujenga uchumi endelevu kama haitojenga unoja wa kitaifa, dalili zinaonekana, huenda uchaguzi huu ukawa ndio mwanzo wa Kenya kugawanyika kuwa nchi mbili, na huu ukipita salama, 2022 ndiyo mwisho wa umoja wa Kenya.
Badala ya kuzungumzia uchumi ni bora zaidi kwa Kenya kujifunza ni kwa jinsi gani Nyerere aliamua kuanza kujenga utaifa kwanza na kuacha kujenga uchumi, kwa sababu alijua kuna baadhi ya mambo usipoyarekebisha mwanzoni kabisa mara tu baada ya uhuru, sio rahisi tena kuyarekebisha baadae, mambo ya uchumi yanarekebishike wakati wowote ule, sasa wakenya mnadhani kujenga umoja wa kitaifa sio muhimu tena au imeshindikana Kenya kumaliza hizo tabaka mlizonazo kwa hiyo mumeamua kuziacha ziwatafune?