Theresia Dismas : Mama jasiri aliyeiletea Tanzania medali ya kwanza 1965

Theresia Dismas : Mama jasiri aliyeiletea Tanzania medali ya kwanza 1965

Melubo Letema

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2020
Posts
416
Reaction score
414
Katika medani ya kimichezo Tanzania, historia ya kuletwa medali ya kwanza katika mshindano ya kimataifa ilitekelezwa na mwanamama Theresia Dismas
IMG_4215.jpeg

Watanzania hatukumjua na hata tukatabiri kwamba mama yetu Theresia Dismas hayupo duniani kama nilivyowahi kuandika katika blog hii.
Ukweli ni kwamba mtanzania wa kwanza kufungua pazia la medali yupo hai na kwamba watanzania tuanze juhudi za kumtambulisha kwa viongozi wakuu wa serikali.
Nilipoandika story kuwa mwanamke ndiye aliyeleta medali wa kwanza wengi walistuka maana historia hii inayowainua wanawake ilifichwa kwa muda mrefu bila shaka kutaka kupotosha ukweli.
Jana nimepigiwa simu toka Uingereza na mtoto wa Theresia Dismas akaniambia habari yote katika blog yangu ni kweli “Isipokuwa” mama yao yupo hai na salama na anaishi Kenya!
'Mimi nilistuka na kushindwa jinsi ya kumjibu ila nilifurahi kwamba blog yangu imevumbua dhahabu iliyofichwa' na kwamba nitafanya juhudi kwa kushirikiana na wazalendo wenzangu tuweze kuandaa mwaliko (Reunion) wa mama huyo aje kutoa neno la busara, pia watanzania tumjue kwani yeye ni kioo cha jamii.
Sina shaka kabisa naamini jambo hilo ni kwa masilahi ya taifa na wengi watalifurahia, na nitafanya bidii hilo litimie maana nimefarijika sana; Iweje jina la mama yetu huyo isiwepo katika kumbukumbu za Chama Cha Riadha? "Maneno yake ya jinsi alivyofanikiwa 1965 yataleta morale kwa wasichana wa leo"
Napenda pia kuomba radhi kwa familia ya mama Theresia Dismas kwa kuandika neno 'Marehemu' hiyo haikuwa dhamira yangu bali dhamira yangu ilikuwa kuweka historia sawa.

Chanzo : gidabuday Blog
 
Kweli bayi miyeyusho, lakini hili la huyu mama yetu kuishi kenya kisa amkimbie bayi naamini si kweli.
Inawezekana sio kweli, ila Kanali Juma Ikangaa ndiye mmeba maono ya huyo mama hadi kuanzisha mashindano ya "ladies first" nadhani utanielewa taratibu
 
Tanzania haipendi kabisa kutambua michango ya watu kama hao katika kuipa nchi heshima lakini angekuwa ni kada wa ccm na amsifie "mama" hakika barabara nyingi zingeisha itwa kwa jina lake.
 
Back
Top Bottom