These pics of Nairobi Terminus will make you think a bullet train is on the way but...

Niwe mfuasi wa Jubilee au upinzani, ninacho omba ni mhoji kitaalam, muache mihemko na ukurupukaji. Tumia muda wako kutafiti na kusoma, ongeza akili zako kwa zile za kuambiwa. Watu tubishane kwa hoja zenye mantiki. Hadi leo sijaona hata mmoja wenu anayethubutu kuzifanyisha akili zake kazi kwa kufuata data, nyote mnahoji muonekano wa hivyo vichwa.

Hela hata kama ni zako, lazima ufuatilie kitaalam, uhoji nini mantiki ya kununua vichwa vyenye muonekano wa hivyo, nini sifa za hivyo vichwa, vina ubora gani, vimejengwa vipi na vina uwezo upi. Ukinishinda kwenye hoja kama hizi, nitakuona mzalendo na mwenye uchungu na nchi na mwenye nia njema, lakini kwa kukurupupa na kuniita Jubilee, nakuona huna tofauti na umati wa watu ambao hufuata wanasiasa nyuma na kuitikia kila wanachoambiwa, bila ya wao kutumia ubongo wao.

huwezi ukaweka masharti na mipaka ya maswali ya wenye nchi kwa sababu amekutwika mamlaka ya uongozi. sisi sio wataalamu wa shughuli za reli. lakini hamna asiyejua kuhoji kuhusu utumiaji wa hela za kwake. maswali ya uajibikaji hayahitaji utaalamu. wewe ndio mihemko ya kutetea kujubilee umefumbika macho. na mie sipo hapa kwa mashindano kama ulivyo omba, ni mjadala kuhusu uajibikaji kwa hela zetu! even when the king is clearly naked unamwambia yupo sawa tu!!
 
Congratulations to the united Republic of Chinese people
 
huwezi ukaweka masharti na mipaka ya maswali ya wenye nchi kwa sababu amekutwika mamlaka ya uongozi. sisi sio wataalamu wa shughuli za reli. lakini hamna asiyejua kuhoji kuhusu utumiaji wa hela za kwake. maswali ya uajibikaji hayahitaji utaalamu. wewe ndio mihemko ya kutetea kujubilee umefumbika macho. na mie sipo hapa kwa mashindano kama ulivyo omba, ni mjadala kuhusu uajibikaji kwa hela zetu! even when the king is clearly naked unamwambia yupo sawa tu!!

Sio lazima uwe mtalaam wa masuala ya reli ili uweze na kuwa na uwezo wa kuhoji vitu vya msingi. Hata uanponunua gari hususa la kubebea mizigo, kuna maswali ya msingi na yenye mantiki ya kuuliza na kuhoji. Huwezi ukaishia tu kwenye muonekano wa nje, utafuata zaidi ya kutaka kujua engine power na mengineyo.

Kama gari unanunua la kuonyesha onyesha marafiki, labda hapo utaishia tu kwenye image. Lakini kama la mizigo na biashara, nina uhakika asilimia 100% utahitaji kujua mengine. Pia nakuhakikishia hata kama ingelikua Raila au Kalonzo, lazima kuna baadhi yetu tungehoji kwa kutumia ubongo na sio vitu vya kukaririshwa kwenye vijiwe vya kuangalia muonekano.
 
Mbona mambo rahisi unajaza page 2. Uajibikaji, hauitaja kupata kugugumizi kutoa jibu isipokuwa kama unasuka story kama kawaida ya serikali hii. Unakokwenda zipo. Nitakutuma kwa wizara ya ujenzi Na miundo mbinu kachunguze mambo ya vichwa n.k
 
Labda utaona kama nipo kwenye ushindani na wewe, lakini ukija kunielewa utashangaa mwenyewe. Mimi ni mwananchi mzalendo wa nchi yangu na mwenye uchungu na nchi, na huwa napenda sana kujadili masuala ya maendeleo na Wakenya wenzangu, ila pia sipendi kuponda vitu ilmradi tu nionekane nipo, lazima nihoji taratibu, hatua kwa hatua.

Serikali ya sasa ya Jubilee kwa kweli ina madoa, imeonyesha udhaifu mkubwa sana kwenye masuala ya kupigana na ufisadi, kuna tuhuma za ufisadi hadi huwa nahisi aibu na kuchukia. Lakini pia pamoja na hayo, siwezi kuibuka na kuelekeza kidole kwenye kila kitu kama kichaa, lazima pawe na ishara za ufisadi ndio tukemee wote, lakini sio kukurupuka tu kisa watu wanaponda na hata mimi niponde.

Suala la ufisadi Kenya limekithiri na ni wazi hatupo tayari kupigana nalo, sote tumejaa unafiki na kuelekeza vidole kila maeneo. Alifutwa juzi aliyekua waziri wa ardhi Bi. Charity Ngilu kwa tuhuma za ufisadi, akapokewa na watu wake kama shujaa, akapokewa na wapinzani kama mpambanaji na kulimbikizwa sifa nyingi tu.
Bi. Waiguru leo hii yupo kwenye kinyang'anyiro cha kusaka ugavana.
 
Napenda mijadara Na mwenzangu sana pia Na nakumbaliana Na wewe ufisadi ni kero lakini ino kasumba ya kukubali uovu kwa Sababu x alifanya hivi Na vile is mediocre and backward! I don't care who did what the issue is you convince us to give you atamu za uongozi on particular promises, hence we have to question you against that. Don't tell us ata x ambaye yupo opposition pia yeye alifanya. You won so deliver What you promise!! This goes for whoever wins the coming election.lakini kwangu jubilee on there own word last election they failed big time.
 
Hamna siku nimekua hapa nikitetea Jubilee, wao wapo serikalini na kila wakifanyacho kinawanufaisha wao na jamaa zao. Na pia hamna siku nitamtetea kiongozi yeyote maana kila akifanyacho kibaya kinaniadhiri mimi na familia yangu na vizazi vyangu vya kesho. Hivyo hilo nalifahamu tena kwa kina,

Lakini hata hivyo nashikilia siku zote, haitotokea niponde ilmradi nionekane na mimi nipo. Lazima nihoji kwa hoja zenye mantiki, lazima nihoji pia pande zote mbili, serikali na upinzani maana hata hao upinzani wanashikilia maeneo yanayonihusu binafsi kama vile gavana wa Nairobi, leo hii kila hatua anayochukua inahusu maisha yangu na familia yangu kwa aslimia 100%

Anyway nchi yetu tuipende kwa dhati na tuwe tayari kuilinda kwa ndani na nje, na tuwakemee mafisadi na maadui wa uchumi bila upendeleo.
Asante na kwaheri Mkenya mwenzangu.
 
Nshasahau kichwa cha huu uzi... unasemaje vile?
 
Bongo tushaachana na hayo mambo, tunanunua ndege tu
 
Back
Top Bottom